Lissu jifunze, Huwezi kushika dola kwa kupambana na dola, Never

Mkuu nilidhani na wewe ni mpambanaji kumbe umeambatana na mapandikizi wenzako huko upinzani....

Dola ya kigaidi huwa hakuna mbadala zaidi ya kupambana nao
Mimi bado ni mpambanaji lkn Lissu anatakiwa kuheshimu viongozi na utaratibu alioukuta.
 
Kwenye demokrasia na dola kuheshimu sheria huwezi kulinganisha Marekani na Tanzania, umejionea uchaguzi uliopita msimamizi anaweza kukunyima fomu na usifanye lolote ukilalamika unapigwa risasi peupe.

Unapo dili na dola angalia unapambana na dola ya aina gani kwa hili hata Lissu analijua.
 
Hali inakatisha tamaa sana. Chama kilichojipambanua kwa kupambana na rushwa; na ufisadi leo hii hata haijulikani kinapigania nini. Hata wale waliodhaniwa kuwa ni critical thinkers kumbe nao ni machawa tu wanapambania matumbo yao. The situation is hopelessly hopeless! 🚮

 
Infact,
kupambana na chadema tu kachama kadogo tu kashindwa,

sembuse kupambana na dola ?🐒
 
Maneno yako yanaashiria uelewa wa kiasi fulani, wa Siasa.
Unapokosea, ni pale unapojiaminisha kwamba mwenye uamuzi wa nani atawale, ni Dola.
Katika historia ya Tawala za Dunia, tangu zama za kale, anayeshikilia Dola huondolewa kwa namna mbili tu.
Ama Mtutu wa Bunduki, mathalani Iddi Amini Dada wa Uganda; Mobutu wa Zaire, na majuzi tumeona Assad wa Syria akiikimbia Nchi yake.
Namna ya pili, na ya mwisho, ni Nguvu ya Umma; mathalani Ayatollah Khomeini wa Iran, Hichilema wa Malawi, na kadhalika.
ama Nguvu ya Umma.
Hilo Darasa la Siasa makini, za dialogue na ballot box wakati "Playing Field is not Level" ni ndoto za alinacha.
Hufai wala huwezi kuwa Mshauri wa Siasa, hata kwa Chama Dola.
 
Ndiyo uelewa wa chawa
 

..sasa hivi hakuna dialogue, na hakuna ballot box.

..lazima ufanye harakati ili kutengeneza mazingira ya kwenda kwenye dialogue, na baadae ballot box.

..dola inaheshimu mwanasiasa au mwanaharakati mwenye ushawishi, na anayeungwa mkono na umma.

..tujiulize kati ya Mbowe, na Lissu ni yupi mwenye hoja zenye ushawishi? Ni yupi anaungwa mkono?

..wapigakura wa Chadema wanachagua kwa niaba ya wananchi walio na vyama, na wasio na vyama.

..wapigakura wanapaswa kuchagua mgombea ambaye Watanzania wanamtarajia, anayekidhi ajenda ya mabadiliko.
 

Mkuu bado hujasema, utasema tu. Lisu kamatia hapo hapo.
 
Mabadiliko ya kwenye jamii na siyo mabadiliko binafsi
 
ANC, Mandela Africa Kusini, alikuwa anpambana na nini???

Hongera kwa kuchagua UJINGA 😅
 
Ili ushike dola inabidi uipigie magoti Dola? Aisee.
 
Leo hii Lisu ananangwa JF, kweli maisha yanaenda kasi sana
 

..polisi na wasimamizi ni watu kama mimi na wewe.

..kabla hawajaamua kukunyima fomu, au kukupiga risasi, ni lazima watafakari kama watakuwa salama au la.

..sasa umma ukiwa umeelewa na kuiunga mkono ajenda ya mabadiliko,wasimamizi, na polisi, watakuwa makini zaidi katika kufanya kazi zao.

..Chadema wanatakiwa warudishe vibe walilokuwa nalo mwaka 2015.

..Je, ni mgombea gani kati ya Mbowe, na Lissu, anayeweza kuwarudishia nuru, na imani waloyoipoteza?
 
Mimi nazungumzia modern politics siasa za kistaarabu Ila sipingi aina zako za kuingia madarakani za mapinduzi na nguvu ya umma,

Niambie kati ya hizo aina ipi Lissu anaiweza, mapinduzi? au nguvu ya umma kwa umma upi wa watanzania.
 
pole sana kwa vijana wanaotumika kisiasa/wanaotumiwa na wanasiasa (mdude na wengine...poleni sana),RIP kwa wanaharakati waliopeteza maisha yao wakitetea haki bila kujua wanatumika kisiasa(Mawazo,Alikibao na wengine).Ni huzuni sana.Demokrasia ya Afrika na siasa za Afrika NI MCHEZO MCHAFU..SIASA MCHEZO MCHAFU SANA...USIMUAMINI MWANA SIASA
SI-HASA(NOT-REAL)=SIASA=UONGO.

Mfano kipindi kile LOWASA anagombea CHADEMA ...hii ilitosha kufanya kutokuwaamini wanasiasa.
so sad ...NI HUZUNI ZAIDI kwa wanaowaamini wanasiasa imani yao kwa wanasiasa ni mtaji unofanya watumike vibaya..hata kupoteza uhai wao...NI HUZUNI SANA.
 
Umma upi wa Tanzania, mara ngapi Chadema imeandaa maandamano wangapi walijitokeza.
 
Chadema wangejitambua wangempa Lissu, au CCM ndiyo inayosizitiza asipewe? Akipewa imekula kwao.
 
Una hoja mkuu....

Hawa jamaa wametusaliti toka kitambo
 
Mimi nazungumzia modern politics siasa za kistaarabu Ila sipingi aina zako za kuingia madarakani za mapinduzi na nguvu ya umma,

Niambie kati ya hizo aina ipi Lissu anaiweza, mapinduzi? au nguvu ya umma kwa umma upi wa watanzania.

..siasa ni UMMA / WATU.

..watawala na dola wakiona Chadema ina watu wa kutosha lazima watatoa nafasi kwa dialogue.

..juhudi zinazofanyika sasa hivi ni kuhakikisha Chadema haipati Mwenyekiti atakayekifanya chama hicho kikubalike zaidi na umma.

NB:

..sijui kama uliona kilichotokea NGORONGORO. Wale watu hawakufanya fujo yoyote lakini uliona jinsi DOLA ilivyokuwa na adabu mbele yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…