Lissu: Kauli ikiwa haina maana hata kama aliyesema ni Rais haitabadilika kuwa na mantiki

Lissu: Kauli ikiwa haina maana hata kama aliyesema ni Rais haitabadilika kuwa na mantiki

Hizi lugha ndio Nape kawakatazeni!
Kama Rais kaziba masikio, unadhani kina Lissu na sisi wengine ambao hatukubaliani na nchi yetu kuuzwa kwa bei chee tutafanyaje ili atusikie hata kama kaziba masikio yake?! Lazima tutukane na tuongee kwa sauti kubwa.
Na asipotusikiliza, tunamhakikishia kuchukua hatua kali zaidi.
Ngoja aendelee kuziba masikio.
 
Mtu auze nchi halafu unataka achekewe chekewe?
Wewe mleta mada unaongea kitu gani?
Rais alitumia neno stupid!
Mbona hujaja hapa kumuanzishia mada?
Kwanza hakuna nchi iliyouzwa bali kuna mkataba wenye vipengere vya HOVYO. Kwa binadamu mwenye akili sawa ambaye ametendewa MEMA na Samia kama alivyotendewa Lissu angechagua lugha ya kutumia.
 
Hivi Lisu kulipwa stahiki zake, na kufutiwa kesi yake, vilikuwa ni rushwa ya kumfanya Lisu asiseme hata akiona mambo ya hovyo yanatendeka?
Mkuu sijapingana na kukosoa mkataba, bali ni ukali wa maneno ya Lissu. Jamaa hama mshipa wa aibu wala chembe ya shukrani
 
Matusi yapo wapi hapo?Tatizo Tz hatuupendi ukweli na ndo maana tunafeli kila Nyanja tunayoenda
Mkuu mbona wewe unaandika vizuri na tunaelewa!! Lakini huyu jamaa anamwita Rais ni akili au matope?? Sidhani hata kama familia yake inakubaliana kwenye hili
 
Nina declare interests. Hata mimi nina thread 2 zinazokosoa makubaliano ya DP WORLD na Tanzania kama:-

(1) Rais Samia unao muda wa kujisahihisha; Pokea maoni ya kuboresha mkataba au futa mkataba wa DP WORLD na thread nyingine ni kama ifuatavyo:

(2) Jebra, Mtobesya na Wanasheria wengine, fungueni kesi dhidi ya Mkataba wa DP World

Sikiliza hii clip ya dakika 5 halafu tathmini kama afya ya akili ya Tundu Lissu iko sawa. Kumbuka Rais Samia akiwa Makamu ndiyo kiongozi pekee wa nafasi ya juu aliyemtembelea kumuona Tundu Lissu akiwa Nairobi hospital.

Kisha akamtembelea Brussels baada ya kuwa Rais. Na akamlipa stahiki ambazo chini ya Magufuli asingeweza kupata. Akamfutia na kesi zake 2 mahakama ya Kisutu

View attachment 2692011

Waliompiga Lisu risasi wako hapa hapa nchini na wanafahamika. Samia kwa nafasi yake ya urais anaweza kuwasaka na kuwatia ndani. Hafanyi hivyo kwakuwa hana wema huo unaotaka aonekane anao. Pesa alizomlipa Lisu ni za umma na kwa mujibu wa sheria na sio hisani.

Hayo yote aliyofanya hakuna popote yanampa uhalali wa kuingia mikataba ya kihuni ya raslimali za taifa. Na Lisu anafahamika kuwa ni mtetezi wa raslimali za taifa, na hana simile na yoyote anayeingia mikataba mibovu ya mali za umma. Haijalishi kama alimuongezea damu huko hospitalini au la.
 
Mkuu sijapingana na kukosoa mkataba, bali ni ukali wa maneno ya Lissu. Jamaa hama mshipa wa aibu wala chembe ya shukrani
Lugha kali ni kawaida ya Lisu, na hizo ndio lugha zinazoeleweka vizuri kwa viongozi wezi. Subiri siku Samia apigwe risasi kama Lisu ataacha kwenda kumtembelea, ama Lisu akiwa rais kama atamnyima Samia stahiki zake, hapo ndio utasema Lisu hana shukurani, sio kukalia kimya uuzwaji wa raslimali za umma.
 
Huna hoja ,urafiki upo palele , ila kwenye mambo ya kitaifa hakuna msalia mtume, kwamba kisa u rafiki ndo uje nyumbani kwangu kujimwambafai , ujinga mtupu , mleta pumbavu
Kwa binadamu mwenye akili sawa ambaye ametendewa MEMA na Samia kama alivyotendewa Lissu angechagua lugha ya kutumia
 
Waliompiga Lisu risasi wako hapa hapa nchini na wanafahamika. Samia kwa nafasi yake ya urais anaweza kuwasaka na kuwatia ndani. Hafanyi hivyo kwakuwa hana wema huo unaotaka aonekane anao. Pesa alizomlipa Lisu ni za umma na kwa mujibu wa sheria na sio hisani.

Hayo yote aliyofanya hakuna popote yanampa uhalali wa kuingia mikataba ya kihuni ya raslimali za taifa. Na Lisu anafahamika kuwa ni mtetezi wa raslimali za taifa, na hana simile na yoyote anayeingia mikataba mibovu ya mali za umma. Haijalishi kama alimuongezea damu huko hospitalini au la.
Mbona wewe mkuu pamoja na kutumia disgused ID mbona lugha yako nyepesi tu !! Kubali tu mapungufu ya Lissu kuwa yako kwenye kauli
 
Mbona wewe mkuu pamoja na kutumia disgused ID mbona lugha yako nyepesi tu !! Kubali tu mapungufu ya Lissu kuwa yako kwenye kauli
Hilo la kuwa Lisu ana lugha kali kila mara tunalisema hapa. Lakini kwa bahati mbaya ndio lugha inayoeleweka na watawala kuliko hizo lugha ziitwazo za staha, na kujinyenyekeza.
 
Lisu amekosea, kwa mtu alie na akili timamu huwezi fanya alichofanya hapa. Hata kama ni mtanzania wa kawaida huwezi sema alichoongea ni matope. Kulikuwa na ubaya gani angeitwa na kutoa maoni yake kama Raisi alivyo sema. Upinzani wa aina hii ndo unaoirudisha hii nchi nyuma. Leo hii kwa aina hii ya kuropoka hata kama anamchango kwa Taifa kwenye masuala ya Sheria bado hataweza kuutoa kwani anaonyesha hayupo tayari.

Kukosoa kuwe na mipaka pamoja na staha. Amemvunjia Raisi heshima kwa kiwango kikubwa sana.
 
Back
Top Bottom