Lissu: Kauli ikiwa haina maana hata kama aliyesema ni Rais haitabadilika kuwa na mantiki

Baba yako mzazi iyekulea, ikitokea akabaka mtoto wa jirani, hutamuambia ukweli? Hutamuona ni kichaa?

Kumtendea mtu mema haimaanishi ukifanya ujinga basi akuache
 
Lisu amekosea, kwa mtu alie na akili timamu huwezi fanya alichofanya hapa. Hata kama ni mtanzania wa kawaida huwezi sema alichoongea ni matope. Kulikuwa na ubaya gani angeitwa na kutoa maoni yake kama Raisi alivyo sema. Upinzani wa aina hii ndo unaoirudisha hii nchi nyuma. Leo hii kwa aina hii ya kuropoka hata kama anamchango kwa Taifa kwenye masuala ya Sheria bado hataweza kuutoa kwani anaonyesha hayupo tayari.

Kukosoa kuwe na mipaka pamoja na staha. Amemvunjia Raisi heshima kwa kiwango kikubwa sana.
Tunataka upinzani imara kama wa USA na Kenya raisi anapigwa spana aswaa[emoji16]
 
Sikiliza hii clip ya dakika 5 halafu tathmini kama afya ya akili ya Tundu Lissu iko sawa. Kumbuka Rais Samia akiwa Makamu ndiyo kiongozi pekee wa nafasi ya juu aliyemtembelea kumuona Tundu Lissu akiwa Nairobi hospital.

Kisha akamtembelea Brussels baada ya kuwa Rais. Na akamlipa stahiki ambazo chini ya Magufuli asingeweza kupata. Akamfutia na kesi zake 2 mahakama ya Kisutu
Ninachokiona hapa ni huyu anayehoji "afya ya akili ya Tundu Lissu kama iko sawa." Kuwa pengine ya kwake ndiyo yenye matatizo.

Sababu ya kuhoji hivyo ni haya aliyoweka hapa kuyaweka kuwa kama fadhira alizofanyiwa Lissu, ambazo zinatakiwa zimfunge akili yake asifikiri vinginevyo kwa huyo aliyemfanyia fadhira.
Hii siyo akili unayoweza kusema ni akili isiyokuwa na matatizo

Lissu hakupewa fadhira kwa kutembelewa na watu hao hao waliotaka kumwondoa duniani. haya ya mafao yake, ni haki yake, na siyo msaada aliopewa kana kwamba hakustahiri kupewa.

Sasa swali la kujiuliza hapa, haya yalifanyika ikiwa kama rushwa aliyopewa Lissu asitoe mawazo yake juu ya haya yanayoendelea sasa hivi?

Huu mtindo wa uongozi wa kupuliza puliza na kupoza, huku kuumiza kukiendelea chinichini, eti watu wasiseme; unadhani watu bado hawajaungundua ujuha huo?

Mbowe na CHADEMA walishaingizwa huko, sasa wametambua kwamba kumbe ni hadaa na kiini macho.

Acha Tundu Lissu aseme kwa njia yoyote itakayowasilisha ujumbe halisi.
 
Samia alijiona mwema mbele ya chizi. Haya ni malipo sahihi ya wema wake. Mnafiki hula unafiki wake. Atukanwe tu.
Aiseee!

Nimekusoma mara ya kwanza, nikafikiri bado sijaelewa maana unayolenga na ujumbe huu.

Nikasoma tena mara ya pili kwa uangalifu zaidi...

"Samia alijiona mwema mbele ya chizi" Chizi hapa ni Lissu, nilivyoelewa mimi..

"Haya ni malipo sahihi ya wema wake" yaani wema wa Samia.

"Mnafiki hula unafiki wake" Mnafiki hapa ni nani kati ya Samia na Lissu?. Mimi nimeelewa kuwa ni Samia.

"Atukanwe tu". Anayetukanwa ni Samia, au anaambiwa ukweli?

Kwa hiyo, kuyaweka haya pamoja inakuwa kama ifuatavyo>

Lissu ni "chizi" anayelipwa wema aliofanyiwa na Samia, ambaye ni mnafiki anayestahili kutukanwa na kuambiwa ukweli na chizi.

Huyu chizi kwa bahati nzuri akili zimemwingia kichwani za kumwezesha kusema ukweli!

bado sielewi lengo lako hasa lilikuwa ni lipi ulipoandika haya maneno.
 
N
Kwanza hakuna nchi iliyouzwa bali kuna mkataba wenye vipengere vya HOVYO. Kwa binadamu mwenye akili sawa ambaye ametendewa MEMA na Samia kama alivyotendewa Lissu angechagua lugha ya kutumia.

Kamtendea mema gani?.

Kwamba kaenda hospitali kumuoba hiyo ndo iwe tiketi ya kunyamaziwa akifanya mambo ya hovyo katika nchi? - Nonsense.

Kwanza Samia si ndo alimkebehi Lissu kuwa Askari wa bongo hawakosei target?. Wewe unajua hiyo kauli inauma kiasi gani kwa mhanga kama yule?

Acha apewe maneno yanayomstahili, tumechekeana kiasi cha kutosha ndiyo maana wanauza nchi.

Hizi ndizo lugha zinazostahili madalali wote wa kuuza nchi yetu.
 
Hizi ndio sababu japo ‘oral agreements’ zina nguvu za kisheria lakini ni ngumu kuthibitisha mahakamani.

‘A’ anaweza kuongelea mto, ‘B’ akatafsiri maporomoko.

Raisi alikuwa anaongelea kuweka critics kama sehemu ya civil servants (full-time employees) kwenye wizara ya mipango wasaidie kwenye maswala ya kuandaa na kushauri government policy strategies maana kuna mijitu kazi yao kukosoa tu.

Hakuna sehemu kazungumzia maswala ya tume inayohusu mambo ya bandari. Mpaka mtu unashangaa ukisoma tafsiri za mitandaoni, jamani si ata context yenyewe ilikuwa kuhusu wizara mpya akasema kabisa na jina Mafuru lifanyie kazi hilo ndani ya wizara na ukiona watu sahihi peleka majina wafanyiwe vetting.

Sasa sijui wengine wametoa wapi tafsiri zao. Mtu unabaki unajiuliza shida ni lack of ‘listening skills’ au ‘upotoshaji’ ni tatizo kiasi kikubwa hivyo; on this one I think it’s the former.

Tanzania kuna watu wengi sana wana ‘bias listening’ mizizi yake ni permeated social culture ya majungu, wivu na jamii ya watu waongo waongo; mpaka imekuwa tabia inayokubalika ndani ya jamii.
Context matters. Context ya ukosoaji kwa wakati huu ni Mkataba wa DP World. Rais anasema mmesikia wanatukosoa huku, kule kila mahali. Yeyote anayesikia ukosoaji anaelewa DP World inahusika.

Tunaelewa kuwa Rais hakumaanisha huo mkataba pekee, kwani Huwezi kuingiza watu serikalini kwa kigezo Kimoja tu cha ukosoaji wa mkataba mmoja mbovu kama huu wa DPworld.

Lakini ukosoaji wa kisiasa hauwezi kuwa namna bora ya kuingiza watu kwenye utumishi wa serikali. Siasa iachwe ichukue mkondo wake na mambo ya kitaalamu yaachwe yachukue njia yake.

Bado kuna faulty logic kwenye maelekezo ya Mh. Rais. Aambiwe tu kuwa yatafanyiwa kazi. Na hao akina Lissu nao waendelee kuyapinga kwa lugha kali kabisa yale mauchafu yanayoletwa kinyume na sheria za nchi.
 
Nina declare interests. Hata mimi nina thread 2 zinazokosoa makubaliano ya DP WORLD na Tanzania kama:-

(1) Rais Samia unao muda wa kujisahihisha; Pokea maoni ya kuboresha mkataba au futa mkataba wa DP WORLD na thread nyingine ni kama ifuatavyo:

(2) Jebra, Mtobesya na Wanasheria wengine, fungueni kesi dhidi ya Mkataba wa DP World

Sikiliza hii clip ya dakika 5 halafu tathmini kama afya ya akili ya Tundu Lissu iko sawa. Kumbuka Rais Samia akiwa Makamu ndiyo kiongozi pekee wa nafasi ya juu aliyemtembelea kumuona Tundu Lissu akiwa Nairobi hospital.

Kisha akamtembelea Brussels baada ya kuwa Rais. Na akamlipa stahiki ambazo chini ya Magufuli asingeweza kupata. Akamfutia na kesi zake 2 mahakama ya Kisutu

View attachment 2692011
Kwani Samia kumtembelea Lissu Nairobi na Brussels ndiyo kunafanya kauli ya rais isiyo na mantiki iwe na mantiki?

This logical fallacy is called logical non sequitur.
 
Ninachokiona hapa ni huyu anayehoji "afya ya akili ya Tundu Lissu kama iko sawa." Kuwa pengine ya kwake ndiyo yenye matatizo.

Sababu ya kuhoji hivyo ni haya aliyoweka hapa kuyaweka kuwa kama fadhira alizofanyiwa Lissu, ambazo zinatakiwa zimfunge akili yake asifikiri vinginevyo kwa huyo aliyemfanyia fadhira.
Hii siyo akili unayoweza kusema ni akili isiyokuwa na matatizo

Lissu hakupewa fadhira kwa kutembelewa na watu hao hao waliotaka kumwondoa duniani. haya ya mafao yake, ni haki yake, na siyo msaada aliopewa kana kwamba hakustahiri kupewa.

Sasa swali la kujiuliza hapa, haya yalifanyika ikiwa kama rushwa aliyopewa Lissu asitoe mawazo yake juu ya haya yanayoendelea sasa hivi?

Huu mtindo wa uongozi wa kupuliza puliza na kupoza, huku kuumiza kukiendelea chinichini, eti watu wasiseme; unadhani watu bado hawajaungundua ujuha huo?

Mbowe na CHADEMA walishaingizwa huko, sasa wametambua kwamba kumbe ni hadaa na kiini macho.

Acha Tundu Lissu aseme kwa njia yoyote itakayowasilisha ujumbe halisi.
Kwenye Kiswahili hakuna neno "fadhira" bali kuna "fadhila".

Mwenye afya ya akili hawezi kuongea vile
 
Kwani Samia kumtembelea Lissu Nairobi na Brussels ndiyo kunafanya kauli ya rais isiyo na mantiki iwe na mantiki?

This logical fallacy is called logical non sequitur.
Mbona wewe unakosoa kwa lugha ya staha japo waitwa "kiranga" ni hilo tu
 
Kisha akamtembelea Brussels baada ya kuwa Rais. Na akamlipa stahiki ambazo chini ya Magufuli asingeweza kupata. Akamfutia na kesi zake 2 mahakama ya Kisutu
kwa hiyo unataka kusemaje hapa, au ndiyo matope yenyewe na wewe unazidi kuyaleta.
 
N

Kamtendea mema gani?.

Kwamba kaenda hospitali kumuoba hiyo ndo iwe tiketi ya kunyamaziwa akifanya mambo ya hovyo katika nchi? - Nonsense.

Kwanza Samia si ndo alimkebehi Lissu kuwa Askari wa bongo hawakosei target?. Wewe unajua hiyo kauli inauma kiasi gani kwa mhanga kama yule?

Acha apewe maneno yanayomstahili, tumechekeana kiasi cha kutosha ndiyo maana wanauza nchi.

Hizi ndizo lugha zinazostahili madalali wote wa kuuza nchi yetu.
Nasimama palepale, binadamu mwenye afya nzuri ya akili asingeweza kutoa matamko kama ya Lissu. Wasikilize akina Warioba, Tubaijuka, Prof Shivji nk.

Huyu Lissu ni mgonjwa, shughulikieni hilo
 
kwa hiyo unataka kusemaje hapa, au ndiyo matope yenyewe na wewe unazidi kuyaleta.
Mnamjaza ujinga Lissu naye anajaa na kujiona shujaa. Ila aliyepinda miguu na kujaa vyuma nwilini ni yeye
 
Uchafu ni uchafu na matope ni matope tu hata kama yatatoka kwa baba yako mzazi, tunasemaje...? matope ni matope hat yakitoka kwa mkuu wa nchi, Lissu upo sahihi babaa !!.
 
Nina declare interests. Hata mimi nina thread 2 zinazokosoa makubaliano ya DP WORLD na Tanzania kama:-

(1) Rais Samia unao muda wa kujisahihisha; Pokea maoni ya kuboresha mkataba au futa mkataba wa DP WORLD na thread nyingine ni kama ifuatavyo:

(2) Jebra, Mtobesya na Wanasheria wengine, fungueni kesi dhidi ya Mkataba wa DP World

Sikiliza hii clip ya dakika 5 halafu tathmini kama afya ya akili ya Tundu Lissu iko sawa. Kumbuka Rais Samia akiwa Makamu ndiyo kiongozi pekee wa nafasi ya juu aliyemtembelea kumuona Tundu Lissu akiwa Nairobi hospital.

Kisha akamtembelea Brussels baada ya kuwa Rais. Na akamlipa stahiki ambazo chini ya Magufuli asingeweza kupata. Akamfutia na kesi zake 2 mahakama ya Kisutu

View attachment 2692011
Nikurekebishe kidogo,hakumlipa stahiki zake kama fadhila,bali walilipa stahiki ambazo serikali ilitaka kupora na kuiba,
 
Nina declare interests. Hata mimi nina thread 2 zinazokosoa makubaliano ya DP WORLD na Tanzania kama:-

(1) Rais Samia unao muda wa kujisahihisha; Pokea maoni ya kuboresha mkataba au futa mkataba wa DP WORLD na thread nyingine ni kama ifuatavyo:

(2) Jebra, Mtobesya na Wanasheria wengine, fungueni kesi dhidi ya Mkataba wa DP World

Sikiliza hii clip ya dakika 5 halafu tathmini kama afya ya akili ya Tundu Lissu iko sawa. Kumbuka Rais Samia akiwa Makamu ndiyo kiongozi pekee wa nafasi ya juu aliyemtembelea kumuona Tundu Lissu akiwa Nairobi hospital.

Kisha akamtembelea Brussels baada ya kuwa Rais. Na akamlipa stahiki ambazo chini ya Magufuli asingeweza kupata. Akamfutia na kesi zake 2 mahakama ya Kisutu

View attachment 2692011
Sioni ubaya wowote aliouzungumza Lissu hapo. Alichokisema ndio ukweli wenyewe
 
Back
Top Bottom