Ninachokiona hapa ni huyu anayehoji "afya ya akili ya Tundu Lissu kama iko sawa." Kuwa pengine ya kwake ndiyo yenye matatizo.
Sababu ya kuhoji hivyo ni haya aliyoweka hapa kuyaweka kuwa kama fadhira alizofanyiwa Lissu, ambazo zinatakiwa zimfunge akili yake asifikiri vinginevyo kwa huyo aliyemfanyia fadhira.
Hii siyo akili unayoweza kusema ni akili isiyokuwa na matatizo
Lissu hakupewa fadhira kwa kutembelewa na watu hao hao waliotaka kumwondoa duniani. haya ya mafao yake, ni haki yake, na siyo msaada aliopewa kana kwamba hakustahiri kupewa.
Sasa swali la kujiuliza hapa, haya yalifanyika ikiwa kama rushwa aliyopewa Lissu asitoe mawazo yake juu ya haya yanayoendelea sasa hivi?
Huu mtindo wa uongozi wa kupuliza puliza na kupoza, huku kuumiza kukiendelea chinichini, eti watu wasiseme; unadhani watu bado hawajaungundua ujuha huo?
Mbowe na CHADEMA walishaingizwa huko, sasa wametambua kwamba kumbe ni hadaa na kiini macho.
Acha Tundu Lissu aseme kwa njia yoyote itakayowasilisha ujumbe halisi.