Lissu: Kauli ikiwa haina maana hata kama aliyesema ni Rais haitabadilika kuwa na mantiki

Lissu: Kauli ikiwa haina maana hata kama aliyesema ni Rais haitabadilika kuwa na mantiki

Tulia wewe! Nimesema Lissu hajatumia busara kumtukana Rais! Kulikuwa na njia nyingi za kufikisha ujumbe wala si kwa matusi kama alivyofanya! Unaweza kuwa na akili nyingi lakini ukakosa hekima! Lissu amekosa hekima!
Sasa imegundulika kuwa video clip hiyo, mleta mada ameitengeneza ili kumchafua Lisu. Muda si mrefu usishangae nduguyo kuwa banned.
 
Hiyo ni presidential rubbish!!

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Mama anaongelea tume ya mipango, Lissu analipuka na DPW kwani mama kwenye hotuba yake ni wapi alisema anataka watu waende kusaidia kurekebisha mkataba wa DP world?
 
Nina declare interests. Hata mimi nina thread 2 zinazokosoa makubaliano ya DP WORLD na Tanzania kama:-

(1) Rais Samia unao muda wa kujisahihisha; Pokea maoni ya kuboresha mkataba au futa mkataba wa DP WORLD na thread nyingine ni kama ifuatavyo:

(2) Jebra, Mtobesya na Wanasheria wengine, fungueni kesi dhidi ya Mkataba wa DP World

Sikiliza hii clip ya dakika 5 halafu tathmini kama afya ya akili ya Tundu Lissu iko sawa. Kumbuka Rais Samia akiwa Makamu ndiyo kiongozi pekee wa nafasi ya juu aliyemtembelea kumuona Tundu Lissu akiwa Nairobi hospital.

Kisha akamtembelea Brussels baada ya kuwa Rais. Na akamlipa stahiki ambazo chini ya Magufuli asingeweza kupata. Akamfutia na kesi zake 2 mahakama ya Kisutu

View attachment 2692011
Hapo ndiyo uelewe kwamba JPM alimjua tundu kwa nina sana
 
Sasa imegundulika kuwa video clip hiyo, mleta mada ameitengeneza ili kumchafua Lisu. Muda si mrefu usishangae nduguyo kuwa banned.
Hapana, mimi siyo ndugu yangu huyo apigwe ban tu kama ni kweli! Nilikuwa najiuliza tu Lissu amepata wapi ujasiri wa kumtukana Rais matusi mazito hivyo? Kwa kosa gani? Kwenye hicho kipande mbona Rais alikuwa anaongelea tume ya mipango wala siyo Mkataba?
 
Lisu anatafuta attention na kutaka azingatiwe,hakuna mtu mwenye muda wa kujibishana na chizi hata siku moja.
 
kama aliweza kipindi cha dikteta sahivi atashindwa nini?

Aingie basi tuone,umesahau alikuwa analia lia oooh ili nirudi nchini naomba uhakika wa usalama wangu??

Magu alimnyoosha kisawa sawa,amesahau leo anataka kuleta choko choko,hakuna atakempa airtime chizi huyo.
 
Hayo yamesemwa na Lisu alipokuwa akijadili suala la MKATABA wa BANDARI.

Lisu ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo.
 
Ulikuwa bado hujawa mkubwa! Aliyesema dictator uchwara alikuwa alikuwa nani kipindi mtu hata akilala na mkewe anamsifu Magufuli! Alipoeleza ripot ya Prof. Ossoro kwamba ni professorial rubbish iliyobebwa na utawala wa Magufuli bado ulikuwa unajifunza kuelewa mambo.
Then aliposema hivyo kilimkuta Nini baadae.???

Na pia hakusema directly........

Alipepesa macho tu.

Ila hapo amekosa haya kabisa
 
I
Hizi ndio sababu japo ‘oral agreements’ zina nguvu za kisheria lakini ni ngumu kuthibitisha mahakamani.

‘A’ anaweza kuongelea mto, ‘B’ akatafsiri maporomoko...
Hawezi kuendelea kukausha kama vile it’s business as usual. She needs to address the elephant in the room ambao ni mkataba wa DPW.

Yeye kabakia kutoa vihotuba vyake vya kijinga kila mara anapoapisha wateule wake lakini hana muda kuzungumza na Wananchi kuhusu current relevant and controversial issues.

Yeye ndiyo maporomoko anyafanya kama mfereji au non issues. Awatumie vimemo vya maelekezo hao wateule wake siyo kutupotezea muda na vihotuba ambavyo havituhusu 99.9999% ya wananchi.
 
Back
Top Bottom