PreGE2025 Lissu: Nimewekwa gerezani upande wa waliohukumiwa kifo kwa kunyongwa

PreGE2025 Lissu: Nimewekwa gerezani upande wa waliohukumiwa kifo kwa kunyongwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Shida wasomi wengi nchini, na wale wakuu wa idara mbalimbali siku hizi hawaongozi maeneo yao kwa kufuata matakwa ya kitaalam na kikanuni! Badala yake wanaongoza kwa kufuata maelekezo kutoka juu.
 
Kama ni kweli aliyoyasema Lissu leo mahakamani ndivyo ilivyo unakosea sana na ni aibu.

Lisu sio mfungwa. Mpe haki zake kama wengine mahabusu.
Ona sasa siri tumezijua sijui huko uliko unajisikiaje kamanda.

Suala la kuabudu kwamba unaogopa maombi. kwamba mawakili wake wakiongea NAE wewe unateseka ukiwa wapi.

Kwamba Lissu ana nini mpaka mnamlinda kama mtu hatari yaani naona kama mnateseka sana.
Kama kiongozi wao ni huyu unategemea nini kutoka kwa mabwana jela?
Screenshot_20250615-124118~2.png
 
Nazani ameamua kujitetea ili awazalilishe haya aliyoongea leo dunia imeona tulivyo wakatili
 
Jaribu na wewe uvunje sheria halafu upelekwe Magereza. Ile ni dunia nyingine, ina taratibu zake ambazo lazima uziheshimu.

Ni mawazo yangu tu kuwa kwa akili ya Tundu atakuwa amewakwaza mabwana Jela, nao wakamuonyesha makali yao.
Hujajibu swali langu lakini. Ni utaratibu/Sheria ipi Bwana Jela ametumia kumpeleka Lisu kwenye chumba watu wanaotakiwa kunyongwa?
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, ameeleza kwa masikitiko makubwa kuwa licha ya kutohukumiwa kosa lolote hadi sasa, amekuwa akiwekwa katika mazingira kama ya wafungwa wa kifo gerezani, jambo analoliona kuwa ni ukiukwaji wa haki zake za msingi.

Akizungumza leo Jumatatu, Juni 16, 2025, mbele ya Hakimu Mfawidhi Franco Kiswaga katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Lissu alifichua kuwa tangu Ijumaa Kuu, amekuwa akishikiliwa katika "special room" (chumba maalumu) ndani ya Gereza la Ukonga, sehemu maalum inayohifadhi wafungwa waliokwishahukumiwa kunyongwa.

“Gerezani, gereza la Ukonga kuna sehemu moja inaitwa special room (chumba maalumu), eneo maalum ambalo wanakaa wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kifo kwa kunyongwa, mimi ninakaa hiyo sehemu wanayokaa wanaosubiri kunyongwa (death row).

Sasa Mheshimiwa ukiwa death row maana yake ni nini?” alihoji Lissu mbele ya Mahakama. Akiendelea kueleza, Lissu alisema kuwa anafuatwa na kuongozwa na askari wawili kila anapotoka kuonana na mawakili au ndugu zake, hali sawa na ile ya wafungwa waliokwishahukumiwa kunyongwa, licha ya yeye bado kuwa mshitakiwa asiyehukumiwa.

“Ninalindwa muda wote, usiku na mchana, mimi sijahukumiwa kifo lakini ninakaa death row. Pamoja na kuwa death row, bado una haki kwa mfano, haki ya kuabudu"...alilalamika Lissu kuwa hapewi haki hiyo ya kuabudu.

Katika hatua nyingine ya kushtua, Lissu aliieleza Mahakama kuwa ameomba rasmi kuwaondoa mawakili wake na kuamua kujitetea mwenyewe katika kesi ya uhaini inayomkabili.

Alisema sababu kuu ya uamuzi huo ni kutoruhusiwa kuzungumza na mawakili wake kwa faragha kwa zaidi ya siku 68 akiwa mahabusu. “Mawakili wangu walifanya kazi yao kwa ustadi na kwa moyo. Lakini kutokana na mazingira haya ya kutopewa nafasi ya faragha kuwasiliana nao, ninaichukua hii kesi mikononi mwangu. Kuanzia sasa mimi mwenyewe nitakabiliana na mawakili wa serikali,” alisema.

Hakimu Mfawidhi Franco Kiswaga alikubali ombi hilo, akisema Mahakama itamruhusu Lissu kujitetea mwenyewe hadi pale atakapowasilisha maombi ya kuwarejesha mawakili wake.

Kesi hiyo ya uhaini imeahirishwa hadi Julai 1, 2025, ambapo Lissu anatarajiwa kuendelea na utetezi wake binafsi dhidi ya mashtaka yanayomkabili, ikiwemo pia kesi nyingine ya kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni.
 
Huko ndiyo kumamfaa ili apate uzoefu wa waliohukumiwa kunyongwa. Inawezekanaje kweli mtu kutaka kuanzisha uasi kwa nchi tulivu na ya amani kama Tanzania?

Mwambieni aendelee kula mtori nyama ziko chini!! Uahidi kuanzisha uasi kuharibu uchaguzi halafu SERIKALI ikuchekee tu??? No way
Hawa ndio vijana bongo!
 
Akiongea mahakamani leo Tundu Lissu ameeleza kuwa licha ya kuwa hajahukumiwa lakini anakaa upande wa watu waliohukumiwa kifo katika gereza la ukonga.

"Gereza la Ukonga lina sehemu mbili, kuna sehemu amabayo wafungwa wote waiohukumia miaka 30, mahabusu...... wanatakiwa wakae. Halafu kuna eneo moja linaitwa special wing ambalo wanakaa wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kifo kwa kunyongwa.

Mimi nakaa kwenye hiyo sehemu wanaokaa hao wanaotakiwa kunyongwa"

anataka kumaanisha kwamba, pamoja na kwamba hajahukumiwa, ila wameshamuandaa kumnyonga.
 
Kama unaweza ona aibu kujitambulisha wewe ni Taifa gani, sintoshangaa kusikia kuwa unaona aibu hata kuwatambulisha wazazi wako kwa marafiki zako
Mkuu hujawah ona watu wanashindwa kujitambulisha makabila yao?.
Scenerio aliyo iongelea inaeleweka waz. Kikubwa tuu asiichukir nchi yake mazima.
 
Ishi kwa amani bila kufanya jinai, tii amri bila shuruti, heshimu mamlaka zikizopo, ninaamini huwezi kuingia kwenye hizo rumande. Hiyo ndiyo njia pekee
Mkuu punguza uongo ndugu yangu hivi unatak kusema kwamba wote walio jela ni wahalifu au wameikosoa serikali?.
Hivi unadhani huko rumande kuna watoto wangap wa viongoz?

Japokuwa ushauri wako ni mzuri kwamba tujiepushe na makosa as kong as tunaakili timamu.
 
Mwambie atulize makalio, rumande siyo parokiani unachagua kiti cha kukaa. Rumande siyo Makao Makuu ya CHADEMA unakaa kwenye kiti cha kuzunguka na AC. Rumande siyo hoteli unakaa na kuhudumiwa.

Ukiamua kuwa MWANAHARAKATI mropokaji JIANDAE na mazingira yote utakayokutana nayo.
Kwani mwanaharakati mripokaji hana haki zake zilizowekwa kisheria?
 
Hawa Mabalozi mnawa OVERATE sana uwezo wao na kuwatwisha majukumu ambayo siyo yao.

Hivi mnadhani watafanya nini? Kuikaripia Serikali? Au kushawishi misaada isije? Kwa ajili ya Tundu tu?? Acheni UNDEZI wenu.

Kuna wafungwa na watuhumiwa wengi tu Magereza, Tundu ni nani mpaka apewe VIP treatment.
Not VIP treatment, haki zake za kisheria
 
Hawa Mabalozi mnawa OVERATE sana uwezo wao na kuwatwisha majukumu ambayo siyo yao.

Hivi mnadhani watafanya nini? Kuikaripia Serikali? Au kushawishi misaada isije? Kwa ajili ya Tundu tu?? Acheni UNDEZI wenu.

Kuna wafungwa na watuhumiwa wengi tu Magereza, Tundu ni nani mpaka apewe VIP treatment.
Acha kujifanya bwege fungwa ww uone kama kuna mtu atakuulizia sababu you're nothing to any one
hujulikani na yeyote zaid ya bibi yako
 
Utakufa wewe kwa malaria na Samia wala hiyo shaba hatapigwa. Kila mnapomuombea mabaya mnamuongezea uhai. Amefanya mema mengi kwa kanda ya ziwa. Vichaa kama wewe peno hasegawa hawapo huko
Angalia hii nguruwe eti mengi kumbe umaskini mtupu,,,mbususu wewe
 
Mjinga yuko huko Ukonga wakati wajanja wanagawana Tonetone huku njebo
Boss una wivu mkubwa sana kwa lissu jichinguze chuki yote hiyo inatokana na nini hasa au mnafahamiana face to face, Maana anayopigania ni mambo mema tu
make sure unajitazama vema au alikudonyolea wife wako
 
Kwa karibaa yetu sisi waafrica hususan wabantu,tunatikiwa kujua kuwa, tuna deni kubwa sana ambalo ni kupendana, umoja wa kitaifa na kuwa wazalendo na watiifu wa mataifa yetu kulingana na katiba zetu na sio kwa watu wenye ushawishi au wenye nyazifa.

Yaani ukisha kuujua utaratibu sahihi ambao jambo flan linapaswa kufanyika basi, huo ufahamu tuutumie kupima mbivu na mbichi huku tukivumiliana.

Ni hatarii sana kuwatumania au kuwashabikia viongoz au wanaharakati wa kiafrika kiasi cha kuhatarisha usalama wa mataifa yetu.
Vinginevyo iwe kwa ajili ya kuitaka haki inayotugusa moja kwa moja na sio kushawishiwa kutetea nafasi ya mtu mmoja.
 
Back
Top Bottom