Lissu ukirudi Tanzania zingatia hili, kumkashifu Baba wa Taifa ni off limits



Kikatiba Tanzania ni nchi ya kidemokrasia hakuna mtu yeyote ambaye anaweka masharti useme nini na usiseme nini ili mradi unafuata sheria. Kuna tofauti ya kumkashufu mtu binafsi au taasisi Lissu anaongelea Uraisi wa Mwalimu sio Mzee Nyerere kibinafsi. Kumbuka Lissu alienda kuona kaburi la Nyerere. Uraisi ni taasisi sio mtu mmoja
 
Mkuu 'Uzima Tele', nimekusoma kwa makini, na nikarudia kusoma tena mara ya pili baada ya kusikiliza hiyo 'clip' ya video uliyoiweka hapo, ambayo ninakushukuru pia kwa kuiweka.

Mbali ya kutokubaliana na uwasilishaji wa machache katika andiko lako, ninakubaliana nawe katika mengi.

Lakini, kilichonisukuma hasa ni'quote' andiko lako ni kutaka tu kuuliza swali, kama utakuwa na jibu nalo: Hivi Katiba ya Zanzibar iliandikwa na kupitishwa lini? Ningependa kujuwa hilo.

Na wakati nikimaliza kuuliza, nimekumbuka pia swala la nyongeza, kama utakuwa na jibu nalo nitashukuru.

Hivi Muungano wetu ulipoasisiwa, hatua hiyo ndiyo iliyohitimisha kwamba Muungano huo umekuwa kamilifu, au ilitegemewa kwamba patakuwepo na hatua kadhaa kuendelea kuurutubisha zaidi?

Mwisho mkuu wangu 'Uzima Tele', isikuwie rahisi sana kuwadharau waTanzania kuwa ni watu wasiokuwa na akili. Ndiyo, kati yetu, na hasa enzi hizi, pamekuwepo na waTanzania wenzetu wengi ambao unafiki na mambo mengi ya hovyo yamekuwa kama ndiyo tamaduni ya nchi hii.
Ni Mwalimu huyo huyo aliyehimiza watu wjitambue na wajue haki zao, au umesahau?
Kwa hiyo, unapoona kuna waTanzania wanaoheshimu mambo mengi yaliyofanywa na Mwalimu Nyerere, ukadhani wamejitoa akili kichwani bila ya kujua sababu za kumuenzi mwasisi huyo wa taifa letu.
Ni heshima iliyo dhati anayoistahili Mwalimu Nyerere katika mambo mengi sana aliyoyafanya katika uhai wake kama kiongozi wa nchi yetu.

Sasa, tunapotoa heshima hiyo, tafadhali usione kuwa sote ni wanafiki.
 
Pamoja na mazuri yake mengi, kuua mfumo wa vyama vingi kwa takribani miaka 30 ulikuwa ni uamuzi mbaya sana. Mpaka sasa taifa hili bado linakabiliwa na kivuli kizito cha utawala wa chama kimoja kutokana na legacy hiyo.
 
Maovu kama yapo lazima yasemwe ndiyo maana ya upinzani ili wabadilike
 
Wakoloni wa Tanzania hawakutesa watu wakati wa kuutafuta uhuru, walifanya vitimbi vidogo vidogo tu vya hapa na pale kuchelewesha uhuru ili upatikane katika mazingira ambayo yalikuwa na faida kwa pia. Ndio maana huwa nachelea hata kutumia maneno "kuupigania" uhuru.
 
Hili ni doa ambalo haliwezi kufutika. Huwezi kumtukana baba wa taifa. Halafu ubaki salama.
Binafsi sijasikia Tundu Lissu akimtukana Mwalimu, kwa hiyo tusifanye hili jambo liwe kubwa zaidi ya lilivyo.
Hata hivyo, naelewa kwamba Tundu Lissu siyo mtu mjinga, na wala hawezi kuona kuwa anaongeza sifa kwake kwa kutumia ngazi ya kumkashifu Mwalimu. Hilo haliwezekani.
 
Kabla ya nchi kuingizwa kwenye chama kimoja 1965 Tanganyika ilishakuwa na vyama 4 vya siasa na Zanzibar ilishakuwa na vyama 3.
Nitakushukuru ukivitaja vyama hivyo, hasa vilivyokuwa Tanganyika.
 
Pamoja na mazuri yake mengi, kuua mfumo wa vyama vingi kwa takribani miaka 30 ulikuwa ni uamuzi mbaya sana. Mpaka sasa taifa hili bado linakabiliwa na kivuli kizito cha utawala wa chama kimoja kutokana na legacy hiyo.
Utadhani vyama vilifutwa Tanzania pekee, au hujui mtindo wa chama kimoja ulianzia wapi?
 
..unawezaje kuikosoa na kuichambua Katiba ya 1977 bila kumkosoa na kumchambua Mwalimu Nyerere muasisi wa katiba hiyo?

..au unaweza vipi kuukosoa muungano na jinsi ulivyoasisiwa bila kuwa umewagusa waasisi wa muungano Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume?

..naamini Lissu ni kati ya wasomi ambao wanaweza kutoa mchango wenye tija kwa Watanzania wote tunapoelekea kuandika Katiba Mpya na kuunda Tume Huru ya uchaguzi.


..tumpe uhuru Lissu afundishe kuhusu Katiba bora na kutoa elimu ya uraia kwa faida ya Watanzania wote.
 
Ila kuna mungu mtu "Mzungu"
Utabisha....
By the way nchi imeundwa na wakoloni,pia kuna wengi tu walisaidia kuleta uhuru wa kisiasa na sio Nyerere pekee
Wakoloni hawajawahi kuunda Nchi yeyote ile. Ni dhana potofu na upotoshaji Kudai kinyume chake....Nchi zote wamezikuta zikiwa na miundo yao ya Kiserikali, Kijeshi, Kijamii n.k

Walibomoa hawakujenga.

Wakoloni walichokifanya ni kuja kuwagaragasa wenyeji wa nchi hizo, ikiwamo Tanzania. na Hapa uwe mkweli na kusema Nchi zilizobomolewa na Ufalme Dhalimu wa Mabeberu wa Uingereza. Zipo Nchi nyingi hakuna hata haja za kuzitaja.


Ngoja nikunukuu hapa kabla hujaja kusema maneno mengine

"

"Pia ni ujinga kufikiri kwamba kukosoa ni kukashifu,au hauelewi maana ya kashfa na kukosoa?"

Asante kwa mchango wako kwenye Jamii inayojitambua. 'Bongo'.
 
Akili za kijima hizi, akili zako za stone age peleka kwenu, Nyerere alikuwa binadamu kama wengine tuu, sio dhambi na hakuna cha ajabu akikosolewa
 
Unadhani huyu taaahiiria ana lolote la maana wala la mno?
 
Kwani wewe inakuuma nini akitukanwa J k Nyerere?
Basi titamwwmbia amkashifu baba yake mleta hoja Kuna watu wanaonaga Nyerere ni Mungu shida hatusomi hiatoria alikuwa na mapungu yake mengi tu hata huu ujinga ulioko kwa watanzania nyerere anahusika kwa kiasi kikubwa
 
Mtoa mada samahani kuna swali dogo tu hapa. Wewe ndani ya nafsi yako unaamini Nyerere as a human being aliwahi kosea kitu katika maisha yake au alikuwa as perfect as Malaika siku zote za maisha yake?
Mwambieni Lissu, ameshaonywa.
 
Bwashee hivi unategemea kusikia nini kutoka kwa mtu asiyekuwa na akili timamu? Lisu ni hamnazo, sijui kwa nini watu hamulielewi hili?!
 
Kama kamkashifu mpelekeni mahakaman wananchi tutasikiliza hukumu sio mihemko n'a mahaba binafsi kwa mwalimu,lakini kama anamkosoa nankumpinga hilo ndo lengo la sheria ya vyama vingi,hata nyerere hayuko juu ya katiba yy pia aliapa kuilinda ikiwemo kuwalinda wanaomkosoa na kumpinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…