Lissu ukirudi Tanzania zingatia hili, kumkashifu Baba wa Taifa ni off limits

Nyerere, Yesu, and Muhamad walikuwa binadamu tu! Ni pilitics push ndiyo zikawafanya wafikie hapo walipo! Mwisho wa siku ni FK them all
 
SAWA.

Na ninakubaliana nawe kuhusu nafasi ya Lissu, hasa nyakati hizi za leo.

Yaliyofanyika wakati wa Mwalimu mengi yalikuwa na sababu za kufanyika yalivyofanyika kwa wakati huo, kwa hiyo tunapojadili upungufu unaoonekana leo katika hali ya leo, tusisahau 'context' hiyo.

Muungano ulio asisiwa haukuwa kamilifu ulipoanzishwa, hilo linajulikana na lilizungumziwa waziwazi.

Makosa mengi yaliyoendelea kujitokeza na mengine kuongezwa, ni mapungufu ya walioendelea kuulea muungano huo, wakiutumia kwa manufaa yao. Hawakushughulika tena na kuuboresha muungano, bali kuwaridhisha/kuwahonga wapiga kelele waliotishia muungano, wakidhani kelele zitakwisha kwa hongo.
 
Mada niliyoileta iko wazi, na inaeleweka vizuri sana.
Kuna kukosoa sera na kukashifu mtu.
Mtu kama Lissu kwa kupenda sifa za kijinga aliwahi kuchagua kukashifu, tena vibaya.
Hilo halikubaliki.
Kumkashifu kiingizi na muasisi wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Lissu akirudia tena, si tu hataeleweka, lakini ataoata madhara asiyoyatarajia.
Lissu pamoja na wenzake wanatakiwa walete sera mbadala za kiuchumi na kijamii ili kuimarisha Taifa.
 

..Na wanaomtukana Lissu matusi makubwa-kubwa inakubalika? Mtawachukulia hatua gani?
 
Ni kweli ni vzr kukosoana maana ndio kujenga, bila challenges hakuna maendeleo,na kumkosoa mwl.Nyerere sio kosa kabisa.Mm nadhani sisi kama watanzania tungejihoji maswali ya msingi labda yangetusaidia sana na labda tungetoka na fikra za juu zaidi maana lalamiko letu kubwa kabisa ni Umaskini wa watanzania na afrika kwa ujumla wake ambao kila mtanzania na mwafrika anaumizwa nao.labda tungejiuliza yafuatayo.
1.kwa nn nchi za Afrika na Tanzania ikiwemo bado ni tegemezi kwa asilimia 90 pamoja na kuwa na rasilimali nyingi.
2.Mwalimu nyerere alijitahi kulinda rasilimali kwa manufaa ya watanzania lkn kwa nn rasilimali hizo haziwasaidii watanzania.
3.kwa nini sisi waafrika wa leo na watanzania ni waoga kutetea mambo tunayoyaamini kwa manufaa yetu wenyewe.
4.kwa nini tumekuwa na akili ngumu ya kuwatambua wanasiasa tulionao.
5.kwa nini wanasiasa wetu hawajali wafuasi wao ambao wanapoteza uhai kwa ajili yao wakiwapigania na wako rahisi kabisa kujiunga au kurudi
kwenye vyama hasimu.
6.kwa nn baadhi ya watanzania wachache na wanasiasa wanadhani tutafanikiwa kuiondoa CCM jirahisi kutoka mamlakani.
7.Leo tunampokea mtoto wetu na ndugu yetu mtanzania Tundu Antipas Lissu akitokea Ubelgiji alikokuwa amekimbilia swali je anaweza kutukomboa katika hali ngumu yoyote tunayoweza kupitia.
8.Je mkombozi wa kweli ktk Taifa ni nani? Ni mtanzania mwenyewe au ni nani?
9.Je ni vizuri kuwashabikia wanasiasa wanaokimbilia ughaibuni na kuwadharau hawa wanaobaki nchini na kupambana na kila hali inayotokea ktk Taifa.
NB.Kwa tulipofika watanzania tunahitaji kutumia akili zaidi kuliko Elimu tuliyonayo,maana akili itatupa utambuzi zaidi.
 
Ww huna akili, kumkosoa Nyerere si kunitukana, hata Nyerere alijikosoa mwenyewe, kasome kitabu Cha TUJISAHIHISHE Cha Mwalimu mwenyewe

Alafu mie pia binafsi, sikubalian na Sera ya ujamaa, yaan hamna kitu sipend Kama UJAMAA
 
Ww huna akili, kumkosoa Nyerere si kunitukana, hata Nyerere alijikosoa mwenyewe, kasome kitabu Cha TUJISAHIHISHE Cha Mwalimu mwenyewe

Alafu mie pia binafsi, sikubalian na Sera ya ujamaa, yaan hamna kitu sipend Kama UJAMAA
Ulivyo na kutu kichwani hujui hata mada inasemaje.
Soma tena au kama hujui kusoma tafuta mtu akusomee na akueleze tofafauti kati ya kukashifu na kukosoa.
 
Unamzungumzia Tundu huyu aliyesema Serikali itafungwa jela sababu ya makinikia...Tundu huyu anayetetea ushoga..au Kuna mwingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…