Longido, Arusha: Vijana 70 wakamatwa na chuo chao kufungwa wakifundishwa karate na mafunzo ya siasa kali

Longido, Arusha: Vijana 70 wakamatwa na chuo chao kufungwa wakifundishwa karate na mafunzo ya siasa kali

Habari hii imerushwa ITV saa 2 hii usiku.

Kamati ya Ulinzi na usalama Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha imekifunga chuo kimoja cha mafunzo ya kiislam kwa kutishia Amani na usalama wa nchi ambapo wamewakuta vijana walioachishwa shule za msingi na sekondari walioenda kufunzwa Imani Kali na mapigano (Karate na judo)

Mkuu wa Wilaya ha Longido amefanya hilo leo baada ya kamati ya usalama kupata taarifa juu ya mafunzo yanayofanywa kwenye chuo hiko kisichosajiliwa.

Kimsingi vyuo hivi vipo sehemu mbalimbali nchini na ni hatari kwa usalama wa nchi kwani vijana hawa huchukuliwa sehemu mbalimbali kwa lengo la kuja kufundishwa dini na itikadi mbali.
Mimi nahisi serikali ya awamu ya sita inacheza mchezo fulani, na kama si hivyo mtanisamehe kwa hisia hizo. Wale mabinti 132 waliokutwa kwenye nyumba moja huko Dodoma walichukuliwa na serikali na kupelekwa katika Makao ya Taifa ya Malezi na Makuzi ya Watoto hapo Dodoma, ambapo wanapewa mafunzo na matunzo kwa gharama ya serikali. Hatukusikia kama mmiliki wa ile nyumba iliyowakusanya akichukuliwa hatua yoyote.
Hawa wa leo wamekutwa wavulana. Usishangae nao wanapelekwa Makao ya Taifa ya Malezi na Makuzi ya Watoto kule Dodoma, na usishangae hakuna hatua itakayochukuliwa dhidi ya hao waliowakusanya watoto

Hisia zangu ni kwamba hii ni njia tu ya kuhalalisha scholarship ya serikali kwa kundi fulani, ukizingatia kuwa hii ni awamu ya sita
 
Wakristo mnategemea waislamu (sio uislamu) wakosee mpate kujisafisha kupitia hilo na hio ni njia pekee ya kupata relief

Any way, wafuasi wa Brian Deacon wamepata Cha kuongea
 

Attachments

  • Screenshot_20240213-212028.jpg
    Screenshot_20240213-212028.jpg
    35.3 KB · Views: 7
Watu msijizime data

Mimi nakiri kweli Kuna madhehebu yenye misimamo hiyo

ila kukosea Kwa watu wenye maslahi yao binafsi isiwe ndio sababu ya kuporomosha chuki mlizo nazo dhidi ya uislamu


Mfano
Yule jamaa wa Kenya aliyewaua watu kwa kukaa na njaa, huwezi kuulaumu ukristo Kwa hilo bali hayo ni makosa ya mtu au watu fulani na sio dini
 
Aki...
Suala la ugaidi limekuwa nyeti sana.

Mamlaka husika zimeshindwa kuthibitisha bila chembe ya wasiwasi kuwa tunalo tatizo la ugaidi Tanzania.
Kwanini sanaa ya Mapigano ifundishwe katika Nyumba za Ibada au taasisi za kidini?

Serikali ithibitishe namna gani, Mkuu wa majeshi anaposema Vijana wetu wanakuwa recruited Kwenda Msumbiji na Congo unahisi ni muongo?
Uganda wanapotangaza wamemuua Kamanda wa magaidi ni Mtanzania unahisi wanatuchafua tu?
Ni kweli hujui haya au unafanya makusudi tu?
 
Aki...
Suala la ugaidi limekuwa nyeti sana.

Mamlaka husika zimeshindwa kuthibitisha bila chembe ya wasiwasi kuwa tunalo tatizo la ugaidi Tanzania.
Shikamoo Babu

Masuala ya ugaidi ni masuala ya ndani ya mtu. Kuna mtu, kavaa kanzu vizuri ila kimoyomoyo anatamani kumchinja mtu kichwa. Au anatamani kuua makafiri, au kujilipua katikati ya watu. Hivyo ni vigumu kumtambua.


Ila hata Rais, alishasema kuwa kuna watanzania wengi kwenye vikundi vya magaidi.



Swali:
Je wale jamaa wa walikuwa wakiua watu Tanga, Kibaha, Vikindu, Mkuranga,Rufiji, Kibiti, Mtwara, hao wote sio magaidi? Au kwa mtazamo wako unawaona walikuwa sahihi kuua "Makafiri"?
 
Kingine kiko kijiji cha kiangara,kata ya kibutuka wilaya ya liwale mkoa wa Lindi,kijiji hapo kuna msikti mkubwa sana, nadhani wilaya nzima hauwezi ukuta tofauti na huo,una simamiwa na wasuni,mwanzilishi wa msikiti huu ni ndugu salimini mbite,kipindi cha magufuli alishughulikiwa sana bwana huyu kwani huwa anaendesha mafunzo ya itikadi kali.

Nasasa ameanza tena mafunzo kwa kukusanya vijana na kuwafunza itikadi kali,serikali ichukue hatua
Naamini umesomeka na wahusika wameliona hilo.
 
Tuweke udini pembeni

Je Watanzania hawapaswi kujifunza karate na judo? Je mbinu za kujilinda ni kinyume na sheria za nchi? Hizi tahariko tunazobabatizwa nazo kila mara kwa jina la ulinzi na usalama, kwa nini serikali isipeleke mamluki wake hapo nao wakajifunza hayo mafunzo ili kuyachuja kama ni hatari kwa jamii? Naona badala yake ni hizi Kamati za Ulinzi na Usalama zimejikita kwenye kupambania taharuki kuliko kutumia weledi na akili kudeal na haya mambo
Kinacholeta utata hapo ni kuchanganya dini pamoja na karate na judo.
 
Back
Top Bottom