Lukuvi na Kabudi waitwa Ikulu kumsaidia kazi Rais Samia nje ya Muundo wa Serikali
Salaam Wakuu,

Aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi na Aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, wametakiwa kwenda Ikulu kumsaidia kazi Rais Samia ya kuwasimamia Mawaziri...
Mhh, mara ya kwanza tuliambiwa wanaotolewa ni wale wenye jambo Lao 2025, kulikoni tena leo kauli imegeuka?
 
Mtu kama lukuvi, Waziri zaidi ya miaka 20, bado analilia ajira, hivi huyu ana uwezo wa kuweka sera ya vijana kujiajiri kama yeye anasubiri ajira ya ubunge na uwaziri? Pensheni ya uwaziri kwa miaka zaidi ya 20 aliifanyia nini?
Lukuvi waziri zaidi ya miaka 20? Nonsense acha uongo
 
Ninawaza na kubaki mdomo wazi,Kwanin wazee kama akina Lukuvi na Kabudi wamepewa ofisi ikulu ya kumsaidia mama, huku wakiwasimamia wateule wake!

Hapa napata wasiwasi wa mwingiliano wa majukumu na Katibu mkuu kiongozi.

Wakongwe kama akina Paschal Mayala naomba utujuze.
Samia ni muongo muongo tuu, kasema vile kujisafisha baada ya kukosolewa kila kona ya nchi

Aliwatoa kwa sababu za uongo na anaendelea kuwatungia uongo
 
Rais anawapeleka wabunge kuwafungia Ikulu inaruhusiwa?

Anasema atawapa kazi huko za kusaidia saidia kusimamia mawaziri wakati hawa ni wabunge wanaotakiwa wakawatetee wananchi wao majimboni.

Hapa mimi sijaelewa mama ana mpango gani na maamuzi hayo.

Hawa wabunge wakatae kwenda kudeki na kusafisha vyombo ikulu.
 
Usibabaishwe na majina mkuu. Huyo Lukuvi wanaomjua ni tofauti kabisa na unavyomuongelea wewe.

Usimhukumu mtu kwa jina lake, usikariri majina ya watu ukadhani na ufanisi wao wa kazi utakuwa hivyo hivyo.
Hivi ni kweli alimkaba roba yule mwananchi hadi akaitema hela? [emoji848],,
Binafsi namuona Lukuvi ni radical,. Kitabia hapishani sana na Chuma's....

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Mimi naona kama Mama amewatema kiaina! Bora hata angewapa Ubarozi wakapumzike na kumaliza maisha yao ughaibuni.
 
Ninawaza na kubaki mdomo wazi,Kwanin wazee kama akina Lukuvi na Kabudi wamepewa ofisi ikulu ya kumsaidia mama, huku wakiwasimamia wateule wake!

Hapa napata wasiwasi wa mwingiliano wa majukumu na Katibu mkuu kiongozi.

Wakongwe kama akina Paschal Mayala naomba utujuze.

Paskali bado anaandaa waraka wa kutundika humu jamvini kuhusu hilo aje atwist mambo na kuforce na points ambazo ni aver
 
Jamani mnashindwa kuunganisha matukio?

Hapa mama ametumia cheap propaganda.

Juzi kati alisema kuna watu atawaacha ili wakajiandae na 2025!

Tafsiri yake ni kwamba, hao wakioachwa, ndiyo walikuwa wanajiandaa na 2025.

Muda ni msema ukweli. Baada ya miezi miwili tutamuuliza Kabudi na Lukuvi, vipi mnashirikishwa? "Watajibu ndiyo, tunaendelea na kazi vizuri" hata kama hawashirikishwi, na ndio maana wamepewa vyeo ambavyo havimo kwenye muundo. Wakijibu hapana, ina maana majina yatakatwa 2025.

Siasa ni mchezo mchafu!

Jiulize. Kabudi anapewa cheo ambacho hakipo kwenye muundo, je, atawezaje kwenda kuanzisha majadiliano na wawekezaji wakati kuna watendaji wa wizara husika?

Kwa cheo hicho, tafsiri yake ni kwamba, kwa sasa Kabudi ni mtumishi wa wizara inayohusika na wawekezaji! Na atakuwa anaagizwa na waziri husika!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kwa cheo hicho, tafsiri yake ni kwamba, kwa sasa Kabudi ni mtumishi wa wizara inayohusika na wawekezaji! Na atakuwa anaagizwa na waziri husika!
Wamefanywa kuwa desk officers, huyu mama kweli anatuvurugia nchi yetu. Yaani kweli Nape, Makamba, na Ridhiwani anawaona wa maana?
 
Mtu kama lukuvi, Waziri zaidi ya miaka 20, bado analilia ajira, hivi huyu ana uwezo wa kuweka sera ya vijana kujiajiri kama yeye anasubiri ajira ya ubunge na uwaziri? Pensheni ya uwaziri kwa miaka zaidi ya 20 aliifanyia nini?
Hata ubunge wake anashinda kwa rushwa ya Ulanzi na viberiti

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom