Jamani mnashindwa kuunganisha matukio?
Hapa mama ametumia cheap propaganda.
Juzi kati alisema kuna watu atawaacha ili wakajiandae na 2025!
Tafsiri yake ni kwamba, hao wakioachwa, ndiyo walikuwa wanajiandaa na 2025.
Muda ni msema ukweli. Baada ya miezi miwili tutamuuliza Kabudi na Lukuvi, vipi mnashirikishwa? "Watajibu ndiyo, tunaendelea na kazi vizuri" hata kama hawashirikishwi, na ndio maana wamepewa vyeo ambavyo havimo kwenye muundo. Wakijibu hapana, ina maana majina yatakatwa 2025.
Siasa ni mchezo mchafu!
Jiulize. Kabudi anapewa cheo ambacho hakipo kwenye muundo, je, atawezaje kwenda kuanzisha majadiliano na wawekezaji wakati kuna watendaji wa wizara husika?
Kwa cheo hicho, tafsiri yake ni kwamba, kwa sasa Kabudi ni mtumishi wa wizara inayohusika na wawekezaji! Na atakuwa anaagizwa na waziri husika!
Sent from my TECNO F1 using
JamiiForums mobile app