Lukuvi na Kabudi waitwa Ikulu kumsaidia kazi Rais Samia nje ya Muundo wa Serikali
Salaam Wakuu,

William Vangimembe Lukuvi na Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi wametakiwa kwenda Ikulu kumsaidia Rais Samia kuwasimamia Mawaziri
Mmmh! Kuitwa kuwasimamia Mawaziri? Hiki nacho ni cheo gani hiki? Si Mawaziri huwa wanasimamiwa na Waziri Mkuu,au? Mmmh..ngoja niishie kuguna utafikiri nakunya.
 
Akitoa salam kwa viongozi walioapishwa leo ikulu Rais Samia amesema Mh. William Lukuvi hatakuwa spika maana kuna majukumu mengine atakayopangiwa Ikulu.

Ikumbukwe mara baada ya kumuacha ktk baraza la mawaziri baada ya kufanya mabadiliko madogo kulikuwa kuna hisia kuwa huenda Mh Lukuvi ndiye angekuwa spika ila leo Rais amefuta uwezekano huo.

Tutarajie sura mpya kwenye nafasi hiyo maana siyo Lukuvi wala Kabudi
 
Haha! Aliewaweka ye mwenyewe hawaamini teuzi za hangaya bhana..🤣
Wawasimamie kwa makali yapi waliyonayo..?
 
Kwa kauli hii ya Mama Samia kuwa anamvuta Ikulu Lukuvi kuwasimamia na kuwafunda Mawaziri vijana basi kuna mawili aidha kuwa Waziri Mkuu au Katibu Kiongozi. Na ameweka wazi kuwa kuna tetesi atagombea uspika, hatogombea!

Alafu Kabudi anaenda kuwa spika akasimamie vizuri mikataba kwa sababu sio cheo Cha muundo! Ambacho Rais hana mamlaka ya uteuzi. Kwa mujibu wa Mama Samia kuwa hao wana umri mkubwa,atawavuta wamsaidie kazi ikulu.
 
Akitoa salam kwa viongozi walioapishwa leo ikulu Rais Samia amesema Mh. William Lukuvi hatakuwa spika maana kuna majukumu mengine atakayopangiwa ikulu

Ikumbukwe mara baada ya kumuacha ktk baraza la mawaziri baada ya kufanya mabadiliko madogo kulikuwa kuna hisia kuwa huenda Mh Lukuvi ndiye angekuwa spika ila leo Rais amefuta uwezekano huo

Tutarajie sura mpya kwenye nafasi hiyo maana siyo Lukuvi wala Kabudi
Una shangaa nini, Chief Hagaya hajawahi kuwa na mapenzi na Lukuvi, na hataki watu smart na wenye misimamo....yeye wake ni magoi goi wa ndio mzee (sawa mama)
 
Ni hatari sana kazi gani wanazopewa Ikulu wakati hazipo kwenye utaratibu wa Serikali . Hayo siyo matumizi mabaya ya fedha
Kusimamia mawaziri kwani kazi ya waziri mkuu ni ipo. Waziri mkuu naye anahitaji kusimamiwa kwenye kazi yake.
Mikataba ina simamiwa vipi wakati kuna bunge
 
Ni hatari sana kazi gani wanazopewa Ikulu wakati hazipo kwenye utaratibu wa Serikali . Hayo siyo matumizi mabaya ya fedha
Kusimamia mawaziri kwani kazi ya waziri mkuu ni ipo. Waziri mkuu naye anahitaji kusimamiwa kwenye kazi yake.
Mikataba ina simamiwa vipi wakati kuna bunge
Teña ETI wawasimamie mawaziri hahahaha nimecheka sana

USSR
 
Back
Top Bottom