Lukuvi na Kabudi waitwa Ikulu kumsaidia kazi Rais Samia nje ya Muundo wa Serikali
Mawaziri wasiokuwa na wizara maalumu kama alivyokuwa Kingunge enzi za mchonga.
Wamekula kiapo? Maana huruhusiwi kuingia kwenye baraza la mawaziri kama hujala kiapo hadharani
 
Shida ya hii nchi ni kuongozwa na failures, hasa pale kwenye Executive.
 
Ni hatari sana kazi gani wanazopewa Ikulu wakati hazipo kwenye utaratibu wa Serikali . Hayo siyo matumizi mabaya ya fedha
Kusimamia mawaziri kwani kazi ya waziri mkuu ni ipo. Waziri mkuu naye anahitaji kusimamiwa kwenye kazi yake.
Mikataba ina simamiwa vipi wakati kuna bunge
Hili ni tatizo la kikatiba kuendelea kumlaumu huyu mama kwa anayoyafanya mnamuonea tuu katiba imempa nguvu kubwa sana.
 
Salaam Wakuu,

Aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi na Aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, wametakiwa kwenda Ikulu kumsaidia kazi Rais Samia ya kuwasimamia Mawaziri.
View attachment 2075769
Rais Samia kasema watu Wasimpake matope Lukuvi. Wala Wasimsingizie kwamba anaenda kugombea Uspika bali Wamuache amsaidie kazi Ikulu ya Kusimamia hawa Mawaziri Vijana aliowateua.

"Wengine wameanza kumletea [William Lukuvi] meseji za ajabu ajabu wakijua atagombea Uspika, hatogombea. Ana kazi na mimi. Kaka yangu Lukuvi, yeye ana kazi na mimi, mtaisikia baadaye. Lakini namvuta Ikulu, kazi yetu ni kuwasimamia nyinyi.kasema Rais Samia

Rais Samia amesema Kabudi atakuwa na Kazi moja tu Ikulu, Kusimamia kupitia na Kushughulikia Mikataba yote ambayo Serikali inaingia.

"Kabudi amefanya kazi nzuri sana kusimamia majadiliano ya serikali na mashirika, na ndiyo kazi ninayotaka nimkabidhi sasa kindakindaki...Mashirika yote, kazi zote zitakazoingia ubia na serikali, Kabudi ataongoza hiyo timu. Kwa hiyo yeye ni baba mikataba." amesema Rais Samia Suluhu

Amesema hizi kazi hazipo kwenye Muundo wa Serikali lakini anaona ni Msaada Mkubwa Kwake.

MY TAKE:

Je, Kassim Majaliwa na Mkuchika Wameshindwa kumsaidia rais? Kwanini Lukuvi na Kabudi wawe juu yao?

Kapteni George Huruma Mkuchika yeye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) na Waziri Mkuu ni msimamizi wa shughuli zote za serikali katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anawakilisha serikali katika bunge la taifa. Yuko chini ya mamlaka ya rais.
Hawataki Lukuvi Awe Spika wamemtafutia pa kumficha

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
CCM wataendelea na hizi sarakasi na hii midundo mpaka 2025.... mtashangaa wanakwenda kwenye chaguzi wakiwa nguvu moja wanashinda tunaanza tena oooooh tumeibiwa kura...
 
Kinachomponza Samia ni kusoma sana mitandaoni!

Alafu sasa ile sababu ya kuwatoa aliyoisema kumbe ilikuwa ya uongo?

Ok.. Swali kwa machadema, je hao tena si sukuma gang
Wewe mjane wa pombe unaiwaza chadema kuliko hata unavyomuwaza mume wako.

Baada ya the gang kutupwa pembeni umepiga u-turn moja matata mnoo 🤣
 
Mama alisema kuna watu wana mawazo ya uraisi 2025 nawaondoa wakapate nafasi ya kujiandaa ni akina nani?
 
Mnaweza kudanganywa hapo tena Chama kimepasuka....karibu na 2024 Lukuvi anapewa fungu anajitoa CCM na kujiunga CDM na watu kadhaa anakuwa mgombea Urais wa CDM...
 
Kweli Rais ana madaraka makubwa. Kwa hiyo anacreate ajira special kwa hawa wazee wawili. Halafu Samia yupo addicted na mitandao. Anasoma sana mitandao. Lukuvi atakuwa mshauri wa Rais ama?Kabudi tumeambiwa anaongonza majadiliano ya mikataba. Stupid.Wakifa na kaburini awafuate. Maana as if bila wao nchi haiendi. Stupid
Mbona Watanzania hatuna jema? Juzi na jana watu walikuwa wanahoji kuachwa hawa viongozi wetu. Leo Rais kasema sababu za kuwaacha na kwamba atawatumia maeneo mengine zimeibuka sarakasi nyingine! Tumuache Rais afanye kazi. Dah!🙏🙏
 
Je, ni akina nani wamepewa nafasi ya kujiandaa na 2025? Ikiwa kabudi na lukuvi wamepewa kazi maalum? Je, wasiotajwa ndio wapinzani wa mama?
 
Back
Top Bottom