Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.
Amini usiamini pana watanzania walikuwapo JKNIA juzi, Uhuru jana na hata watakuwapo Lupaso leo kama wazalendo wa dhati kabisa.
Kongole kwenu, na kwa hakika mmetutoa kimasomaso kweli kweli sisi kama Watanzania dhidi ya maadui zetu wote.
Utawafunza funzo gani Watanzania hawa kuhusu uzalendo?
Lissu na mwana wa nchi hii akirejea kutoka katika kifo. Mpendwa wetu Benjamin Mkapa akirejea nyumbani kwa Baba yetu kwenye makazi yetu ya milele.
Ni huzuni kubwa iliyo changanyika na furaha.
Nimeshindwa kwenda Lupaso.
Tuwakilishane Lupaso.
Apumzike kwa amani mzee wetu Benjamin William Mkapa.
Mungu ibariki Tanzania.