Hivi kuna mtu anafatiliaga mazishi ya haya majamaa kweli?

Kama ulikuaga haupo kwenye mioyo ya wananchi bwana,ndio mtatumia mabajeti na maguvu meeengi kuomba wananchi waje,of which,you have failed..huwezi lazimisha watu!
 
Amechelewa misa kaamua asije kabisa hadi mda wa kuzika
Sasa inawezekanaje yeye Jiwe, akiwa ndiye "main character" wa tukio zima la leo ndiye achelewe?

Hivi si nyinyi mliamua jana kutowaruhusu viongozi wa Chadema, wasiingie uwanja wa Uhuru, kwa madai ya kuwa ni watovu wa nidhamu, kwa kutozingatia protokali?
 
Poleni kwa msiba mzito wa Rais wetu mstaafu.

Nimekuwa nikizunguka hapa na pale katika mkusanyiko huu wa kumuaga mzee Mkapa wananchi wamekuwa wakijadiliana mbona Rais Magufuli hayupo.

Hakuna hata taarifa kama yupo njian ama amepata dharura za majukumu?

Jana Rais Magufuli aliwasili mkoani Mtwara salama kabisa na kwenda kupumzika.

Natoa pole kwa rais Magufuli najua anapitia hali ngumu ya msiba huu. Sisi wananchi wako tunakupa shime uzishinde hali ngumu. Daima tupo pamoja.

Updates:

Rais Magufuli aanza safari rasmi ya kutoka Mtwara. Muda wowote atawasili.
 
Bado kuna ka umbali mtwara to Lupaso labda atumie choppa ije itue hapo msibani
 
 
Samahani kama mwananchi natamani kufahamu na kujua kama marehemu rais wa awamu ya tatu alikuwa na familia yaani watoto.

Kwa sababu toka msiba uko Dar hadi unagika kijijini kuzikwa sijabahatika kusikia wala kuwaona wanaoitwa watoto wa marehemu Mkapa.

Naomba mwenye ufahamu anisaidie
 
Watanzania wenzangu nimesikitishwa jinsi shughuli ya kumuaga shujaa wetu na muasisi wa wa Tanazania mpya baada ya ile ya Mwl Nyerere.,Ndugu Mkapa. Nahisi watu wa potokali hawajui au kwa makusudi hawakutaka kuwapa watanzania nafasi ya kumuaga Mh Mkapa.

Jna ilikuwa siku ya kumuaga Mh Mkapa kitaifa, nilitegemea kuona makundi mali mbalimali, watu mashuhuri , wasomi wanasiasa jamii ya kimataifa na hata wanafamifilia wakipewa nafasi ya kutoa hotuba za kumuenzi na kuelezea maisha ya Mh. Mkapa. lakini tumeshuhudia mtu mmoja tu akiongea yani raisi Magufuli. Je magufuli anawakilisha mawazo ya watu wote kuhusu hayati Mkapa. Pia maombolezo yametawa;iwa na Ibada kwa kiasi kikubwa , si jambambo kumfanyia ibada, lakini naona imezidi kama vile mkapa alikuwa Kasisi. Ibada hizo zimechukua nasi amboyo ingetumika kuwapa nafasi wanachi kumzungumzia mheshimiwa mkapa.
 
kuna mtoto wake mmoja wa kiume amesuka rasta, yuko ulaya sijui kama amekuja
 
Mkuu, hukusikia Wasifu uliosomwa na Profesa Kabudi jana? Hayati Mkapa ana watoto wawili. Kujionyeshaonyesha, labda, si hulka yao. RIP Mzee Mkapa!
 
Umewaona sasa mkuu au bado?

Maana kama unafuatilia misa Lupaso wala huhitaji utambulisho. Walifanikiwa kumrithi sio tu ufupi ila mpaka miwani zao.

Wewe utakuwa kizazi cha JK, unadhani kila mtoto wa mkubwa ni sampuli ya Riz1.
 
Wafuasi wa cdm wanaopinga pinga kila kitu nadhan mmejifunza kitu lupaso mna kazi sana kuwanyakua hao wapiga kura. Nyomi kama lote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…