Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Simbachawene ahamishiwa Utumishi na Utawala Bora, Jenista arejeshwa Sera, Bunge na Uratibu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri kama ifuatavyo:

Amemteua Mhe. Jenista Joakim Mhagama (Mb) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu). Mhe. Mhagama anachukua nafasi ya Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb). Kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Amemteua Bw. George Boniface Simbachawene (Mb) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Mhe. Simbachawene anachukua nafasi ya Mhe. Jenista J. Mhagama (Mb). Kabla ya uteuzi huo Mhe. Simbachawene alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).

Uteuzi huu umeanza tarehe 01 Aprili, 2023.

Mawaziri wateule wataapishwa tarehe 02 Aprili, 2023 saa 3 asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam.

View attachment 2573265
Haya sasa Watu wa TISS mmeletewa Boss mpya bila shaka mtampa Ushirikiano mkubwa japo kwa sasa Wasukuma wanaonekana ni Maadui na hawaipendi Awamu ya Sita ya Kilazima.

RAI yangu Kwako Simbachawene hiyo Docket umepewa Kimtego ili upashindwe na sababu ya kukutoa rasmi iwepo.

Pia umeteuliwa hapo Kimkakati zaidi ili uweze Kukidhibiti vyema Chama Kipya ( kinachojiandaa Kimya Kimya ) chenye Pro Hayati Msubi wa Chato wengi kisije kuwa Kikwazo Kiushawishi na Kisiasa kwa Aliyekuteua.

Kuwa makini sana katika hiyo Docket.
 
Hawa Mawaziri kila Mabadiliko wamo inaonyesha uwezo wao wa kudumu kwenye Wizara moja hawajiwezi nadhani Mama angewapumzisha tu mbona kuna Watanzania Mil.60
 
Haya sasa Watu wa TISS mmeletewa Boss mpya bila shaka mtampa Ushirikiano mkubwa japo kwa sasa Wasukuma wanaonekana ni Maadui na hawaipendi Awamu ya Sita ya Kilazima.

RAI yangu Kwako Simbachawene hiyo Docket umepewa Kimtego ili upashindwe na sababu ya kukutoa rasmi iwepo.

Pia umeteuliwa hapo Kimkakati zaidi ili uweze Kukidhibiti vyema Chama Kipya ( kinachojiandaa Kimya Kimya ) chenye Pro Hayati Msubi wa Chato wengi kisije kuwa Kikwazo Kiushawishi na Kisiasa kwa Aliyekuteua.

Kuwa makini sana katika hiyo Docket.
Naona wengi mnawaza tofauti na mimi....mi niliwaza huenda amerudishwa kwenye hiyo wizara ili ajibu vizuri hoja za report ya CAG itakapofikishwa bungeni
Hisia zako kali
 
Jenista amerudishwa kule kule, yaan huyu mama mganga wake ni kibokoooo,. Khaaah

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kaoga mzizi wa mninga uliochanganywa na mzizi wa mkuyu,akachinjiwa kondoo mweusi.Mkojani hapindui ufundi wa Jenista!
 
Thubutuuu 🤣🤣🤣🏃 atacheza na bit ya mwenye nchi
Sasa SimbaChawene kashughulike kisawasawa na Watumishi wote wanaokutwa na makosa ya kuiba..

Usiwahamishe bali waondoe kazini. Jenista alikaa kimya tu na kucheka cheka nao. Hata kuwahamisha alishindwa.

Simbachawene umeaminiwa na sasa kawaondoe wote wenye kashfa.
 
TISS si iko chini ya mzee mzima Mkuchika?
Ama Mkuchika anashughulikia mafaili yepi?
Mkuchika alipokuwa Utumishi,alikuwa anaongoza TISS. Kama amehama nayo ,sijui.
Hapa labda kuna mvutano. Labda hiyo wizara inagombaniwa
 
Naomba nitoe unabii
Wapo ambao wataukosa uwaziri kwa siku zijazo na ikitokea hivyo, wapiga Kura wao huko ktk Majimbo yao watakesha kwa nderemo na vifijo, huku wakijipongeza kwa ulabu.

Unabii huu unatokana na baadhi yao kutumia nafasi zao kwa kuwakomoa wanyonge, wasio na lolote wala chochote!
Mungu mpe jicho la Tatu Rais wetu kuwabaini hao.

Mwisho wa Unabii.
 
Back
Top Bottom