Mabadiliko ya vifurushi kuanza tarehe 02/04/2021

Mabadiliko ya vifurushi kuanza tarehe 02/04/2021

Tigo naona vimeumana, vile combo vya mwezi bado hakuna unafuuu.
IMG_1429.png
 
Hii yote ni hawa TCRA (if it ain't broken why try to Fix it) ?

Bei elekezi bei elekezi...., wanashindwa nini kutengeneza kampuni yao (TTCL) na kushusha bundles tuone kama wengine hawatashusha..., kazi yao kuelekeza tu na sio kujaribu kufanya...

Tunajifanya soko huria wakati hawa jamaa ndio sometimes wanafanya bei ziende juu sababu ya makato yao..., Bure Kabisa hawa jamaa inabidi kila mwaka tuwe tunawachunguza wameleta tija gani kwa taifa kwa mwaka
Au ni ujanja wa TTCL ili waje wayapiku makampuni ya simu
 
Afanye kukaa nao mapema
Lakini waziri mwenye dhamana (Ndugulile) si alishasema atakaa na kampuni za simu wafanye mapitio ya bei za bundles?! Ndo keshakaa nao tayari, na hayo ndo matokeo ya makubaliana yao! Mi mwenzenu hapa nasubiri mambo matamu tu manake leo asubuhi asubuhi TTCL wamenitumia message kuniambia kesho naanza ku-enjoy vifurushi vipya!
 
Si wangesema kabisa kama mabadiliko hayo yanahusu kushuka kwa gharama za vifurushi au lah!!!!.
 
TCRA eneo mnalotaka tuishi ni eneo kandamizi na bahati mbaya nyinyi ndio wachoraji wa hii ramani



IMG_20210401_122950.jpg
IMG_20210401_123031.jpg
 
Back
Top Bottom