Mabegi ya Pesa yaliyokutwa Nyumbani kwa Rais Gabon, funzo kwetu

Marais wa Afrika sijui wamerogwa na nani!! Maana tabia na mienendo yao inafanana kwa kila kitu.

Hakuna aliyewaroga...

Viongozi wanatokea miongoni mwetu, hivyo tabia kama za uizi, udokozi, kutoridhika, ubinafsi n.k ni miongoni mwa tabia ambazo mwafrika huishi nazo, na huzionesha pale.anapopata nafasi ya kufanya hivyo...
 
hata ccm tukiwatoa tutakuta matrillion ya hela hivihivi.
 
Hayo mambo ya kizamani sana, siku hizi watu wanaekaga dola tu
Za madafu huwezi kuzikuta hata siku moja, labda zibadilishwe dola
Kuna siku nipo kwenye sherehe ya kuaga (send-off) binti wa rafiki yangu mmoja,nikaona viongozi fulani wawili wakitunza $ kwa bibi harusi mtarajiwa na maids wake,tena ni mia mia.

Naona huu upungufu wa $ itakuwa pia unachangiwa na watu (hasa viongozi) kuzihifadhi kiasi kikubwa majumbani.
 
Vyombo gani huru vinaweza thibitisha? Hizi ni propaganda za Wajeshi kuhalalisha upuuzi wao.

Msisahau Kuna mabegi ya mabilioni yalikutwa Kwa Marehemu Mwendazake
 
Serikali gani? Hii ya mama Abdul? Abdul atakosekana na mabunda kama haya nyumbani?
 
Marais wa Afrika sijui wamerogwa na nani!! Maana tabia na mienendo yao inafanana kwa kila kitu.
Huyo wa Gabon walimchelewesha tu. Hata yeye alikuwa anatamani kuondolewa kwa mbinyo. Kwanza alikuwa hana ushawishi pia alikuwa hana nguvu yaani ile janja janja ya kulishika jeshi kama wenzie ccm,kagema,m7 wafanyavyo
 
Hapa kwetu Tanzania mabegi kama hayo yanapatikana only kwenye Ripoti ya CAG.
Utasikia Kichere akifoka one point five trilioni hazionekani halafu Tulia Ackson anapoza mambo siku zinaenda

Wananchi huduma muhimu hawapati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…