Mabenki yaanza kukusanya Tozo za Serikali kwenye miamala wanayofanya wateja

Mabenki yaanza kukusanya Tozo za Serikali kwenye miamala wanayofanya wateja

yaani serikali inachukua savings za watu hivihivi. Sijui kwa nini inakuwa greedy!

Mbona kodi kibao za miamala ya kibenki tunalipa tayari, sasa hii mambo ya serikali kuingiza mkono wake kwenye savings zetu na kutwaa pesa tunapofanya miamala maana yake nini?
 
Watu wameanza kuletewa meseji kwenye simu kuhusu tozo wanazotozwa pindi wakifanya miamala ya kibenki.

Naona serikali imeamua sasa kutwaa fedha za wananchi kupitia tozo.

Sasa kinachofanyika, wananchi wanailipa serikali kodi za kawaida kama vile VAT n.k, halafu inakuja on top of that inakwangua pesa za watu kwa jina la tozo
Kwa kwenli tozo ni kama unyang'anyi wa wazi.

Mfano wa meseji ambao watu wanapata ni

Ndugu Mteja, tunakusanya tozo ya serikali kwenye akaunti yako kwa miamala ya tarehe 8 Sep 2021 mpaka 6 Oct 2021. Unaweza hakiki kupitia taarifa ya akaunti.
Hata mimi wamenitumia, cha ajabu makato ya kila muamala ni makubwa sana mfano juzi nilituma 200000 toka nmb kwenda airtel wamekata 7000 halafu wanakuja na ishu ya tozo tena
 
Hizi kodi za mshikamano mimi nataka mama aziongeze kila sehemu, hawa watu wakikamuliwa vizuri kwenye chaguzi akili zitaanza kuamka!
Chichiemu hawaogopi tena chaguzi.

Bunduki, Tume, Wakurugenzi, na usalama ndiyo turufu zao.

Mwananchi unapoteza muda wako tu kuungua na jua kupiga kura!
 
Wanasiasa ndo wazandiki, raia hawana cha kujitetea maana sheria zimepitishwa na walisiojali wananchi wao
Wananchi wangekuwa macho hizo sheria wanasiasa wasingepitisha. Au wangezifuta kwa lazima. Lakini watanzania ni maiti
 
Mtoa Mada ameminya taarifa Kwa Makusudi au kwa umbumbumbu wa kutojua hivyo wachangiaji wengi kupotoshwa.
Ifahamike kwamba tozo za miamala ya simu zinatumika Kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine, lakini pia zinatumika Kutoka bank kwenda kwenye akaunti za simu

Hivyo makato ya tozo ya bank ni Yale yanayohusisha bank -simu na si vinginevyo.
Tulipe Kodi tupate haki ya kukosoa, kulaumu, kupayuka na kuandamana ikibidi
 
Hizi kodi za mshikamano mimi nataka mama aziongeze kila sehemu, hawa watu wakikamuliwa vizuri kwenye chaguzi akili zitaanza kuamka!

Mkuu shida ni kwamba hizo CHAGUZI hazipo! Kilichopo ni UCHAFUZI - wanao tangazwa kushinda sio waliopigiwa kura!
 
Huyu mama sijui nini kimempata yaan gafra amegeuka kuwa mtu tofauti hana hata huruma ba wananchi wenye kipato cha chini.

Mpaka anatoka tutaona mengi.
 
CHADEMA mlisema JPM akifa mtapata Uhuru nadhani hapa Mungu anawajibu kupitia Samia ,wanasema ukiomba mama wa kambo afe anakufa mamako na ndio unaipata fresh

Tulieni dawa iingie so mlitaka demokrasia ndio hii Sasa tena ya kiuchumi kizalendo

USSR

Kama wanaoathirika ni CHADEMA peke yao, basi si tatizo kubwa. Tozo ziendelee.
 
Kwan ninavyosikiaha hii nchi inautajiri wa mafuta, gesi , madini n.k

Kwanin tusichimbe na kutengeneza pesa kuibadiri tz kuwa kama Dubai, kazi kukomaa na wananchi tu. Serikali izo rasilimali hamzioni
 
Nakaribia kulazimika kuamini kuwa kumbe kina mama ni wakatili!! Mshahara wangu nimeulipia kodi, nikalipwa kupitia benki, huduma za kibenki stahiki nikalipa, na bado aliyenilipa ujira wangu kupitia benki anazifuata huko tena na kuzikata kodi mara ya pili kwa msamiati wa tozo!! No!! huu ni unyang'anyi!! Hakuna namna ya kusema vinginevyo!!
 
Ccm inapenda kuona siku zote raia wake hasa wa kipato cha chini wakiteseka!

Nyie wote wa kipato cha chini mnafahamika kama CHADEMA. Yaani kazi yenu ni kupinga na kulalamika. Wenzenu CCM wameshaunga mkono tozo zote; hawaoni shida. Nani awasikilize?
 
Watu wameanza kuletewa meseji kwenye simu kuhusu tozo wanazotozwa pindi wakifanya miamala ya kibenki.

Naona serikali imeamua sasa kutwaa fedha za wananchi kupitia tozo.

Sasa kinachofanyika, wananchi wanailipa serikali kodi za kawaida kama vile VAT n.k, halafu inakuja on top of that inakwangua pesa za watu kwa jina la tozo
Kwa kwenli tozo ni kama unyang'anyi wa wazi.

Mfano wa meseji ambao watu wanapata ni

Ndugu Mteja, tunakusanya tozo ya serikali kwenye akaunti yako kwa miamala ya tarehe 8 Sep 2021 mpaka 6 Oct 2021. Unaweza hakiki kupitia taarifa ya akaunti.

Huo ni wizi on day light.
 
CHADEMA mlisema JPM akifa mtapata Uhuru nadhani hapa Mungu anawajibu kupitia Samia ,wanasema ukiomba mama wa kambo afe anakufa mamako na ndio unaipata fresh

Tulieni dawa iingie so mlitaka demokrasia ndio hii Sasa tena ya kiuchumi kizalendo

USSR
Kwa hiyo kodi ya majengo wanatozwa chadema, tozo za miamala ya simu wanatozwa chadema na tozo za miamala ya mabenki wanatozwa chadema na sio wananchi au sio!? Hili uliloandika linaakisi kiasi gani wewe ni punguani.
 
Mtoa Mada ameminya taarifa Kwa Makusudi au kwa umbumbumbu wa kutojua hivyo wachangiaji wengi kupotoshwa.
Ifahamike kwamba tozo za miamala ya simu zinatumika Kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine, lakini pia zinatumika Kutoka bank kwenda kwenye akaunti za simu

Hivyo makato ya tozo ya bank ni Yale yanayohusisha bank -simu na si vinginevyo.
Tulipe Kodi tupate haki ya kukosoa, kulaumu, kupayuka na kuandamana ikibidi
Hata kama ni hivyo, baco ni unyang'anyi maana hiyo ni modality tu ya mhusika kuchukua pesa yake!! Vinginevyo unamlazimisha aende ATM yamkini kwa mazingira yake hiyo itamgharimu pesa nyingi zaidi na muda zaidi!!
 
Back
Top Bottom