Maeneo yenye baridi la kufa mtu Tanzania

Mbona umepasahau na Manzese Dar es Salaam na kwenyewe kuna Baridi hakuna Mfano.
 
Niliwahi kuishi Mahenge Mkoani Morogoro, nako si haba kwa baridi. Tena ni ya mwaka nzima haina msimu.
 
Mleta mada na washirika wako naona bado hamjakanyaga Sumbawanga na inaonesha wengi hamjui hali ya kule. Msimamo ni huu hapa

1. Njombe
2. Iringa
3. Mbeya
4. Sumbawanga
5. Arusha

Tembeeni jamani
 
Sehemu zenye bardi ni
1.Njombe hasa makete
2.Ruvuma hasa mbinga
3. Mufindi iringa
4.Mbeya
5. Rukwa eg Sumbawanga
6.Manyara ( Kateshi ) & some part of Singida
7. Arusha & na baadhi ya maeneo ya Kilimanjaro eg Rombo, Sanya juu
8. Lushoto Tanga
9.Kigoma ndani ndani huko
 
Naona mnaitajataja Arusha kwa dharau ila wenyewe wenye uzoefu na baridi wanasema baridi ya Mbeya haichomi, niko na mzaliwa wa Mbeya hapa Karatu anatamani kurudi kwao.

Hata watu wa Arusha hawajui km Karatu kuna baridi la hatari, njooni mfanye utalii wa ndani mkasimulie.
 
Umesahau kuiweka tanga...lushoto
Na sehemu za korogwe huko milima ya usambara mzee huko juu sahv
Ni giza kuna wakati inagonga mpaka 7,8

Ova
 
Baridi ya Njombe ukitaka Kuoga maji unachemsha Maji ya moto halafu unachemsha Mengine ya Vuguvugu kwa ajiri ya kupoozea ndio uoge sasa....😂😂
 
Joto halipo Dar tu
Hata Moro Kuna mazao kibao yanalimwa na yanawahi kukomaa sababu ya joto.

Baridi ya Njombe ukitaka Kuoga maji unachemsha Maji ya moto halafu unachemsha Mengine ya Vuguvugu kwa ajiri ya kupoozea ndio uoge sasa....😂😂
Mimi nipo Njombe na kila siku naoga maji ya baridi. Asubuhi hii nimeoga maji ya baridi najisikia vizuri sana. Ni kujiendekeza tu kuoga maji ya moto
 
Nimeishi Mufindi, Mbeya na Arusha,
Kuhusu Njombe na Mufindi wala sina shaka ndizo sehemu zinazoongozoea kwa baridi.

Baridi ya Mbeya ikifika mwezi wa 6 huwa ni kali kiasi kuliko ya Arusha.

List iwe hivi

1.Njombe
2.Iringa
3.Mbeya
4.Arusha
Njombe
Marangu
Mbeya
Iringa
Arusha
°°°°°°°°°°°°
 
Kimsingi njombe ndio alfa na omega kwa mikoa ya baridi hapa nchini.


Best place kwangu kuishi ni mikoa ya ukanda wa pwani na kanda ya ziwa.

Baridi siliwezi kabisa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…