Mafanikio ya Rais Magufuli 2015 - 2021
Tatizo la Magu,alidhani atakuwa Rais wa Tanzania milele.miradi mingi utadhani aliambiwa hawatakuja watu wengine kufanya.haya mambo ni kupokezana vijiti unajikuna unapoweza unaachia wengine nao wataendeleza hakujifunza kuwa alianza kuyafanya nyerere na hakuweza kumaliza.
Hii miradi mingine ilimalizwa haraka ili iwe promotion ya mitano ya nyongeza. Alishajiona anaweza kupata miaka 10 mingine ya nyongeza.
 
1. Mabweni ya Chuo Kikuu Cha DAR ES SALAAM
2. Tazara flyover
3. Ubungo flyover
4. Mv. Hapa Kazi TU
5. Mv Mbeya
6. Daraja la Mkupita
Jamani leo ikiwa ni siku ya mazishi yake haki yake tumpeni kila mradi alioukamisha tuutaje
Kufufua reli ya kutoka Dar es salaam-Tanga-Kilimanjaro-Arusha

Upanuzi wa Bandari ya Dar, Tanga, Mtwara

Ujenzi wa gati Mafia

Ukarabati wa vivuko, Mv Pangani, New Mv Butiama hapa kazi Tu, nakadhalika

Mradi wa rada airport ya Dar, Mwanza, Songwe, KIA ....

Elimu bila ada

Vituo vya afya vya kila halmashauri

Hospitali za wilaya, mikoa, na kanda: Serengeti, Hospitali ya kumbuku ya Mwalimu Nyerere, Uhuru Dodoma, nakadhalika

Barabara za mitaa Dar na katika majiji mengine, na miji mingine

Ujenzi wa kota za gorofa Magomeni

Ujenzi wa masoko makubwa: Soko la Job Ndugai Dodoma, Chief Kingalu Morogoro, soko la Kisutu, soko la Magomeni, soko la Mbagala, na ya mikoa na wilaya nyingine

Ujenzi wa standi za kisasa: Mbezi Lous, Dodoma, Morogoro, Korogwe, nakadhalika

Ujenzi wa majengo ya makao makuu ya Halmashauri: Kigamboni, Mkalama, nakadhalika

Daraja la mto Kilombero, na mengine mengi

Madaraja ya waenda kwa miguu: Dar na Mwanza

Ukarabati shule kongwe na vyuo: Pugu, Galanos, Tunduru, Msalato Girls, nakadhalika
 
Tatizo la Magu,alidhani atakuwa Rais wa Tanzania milele.miradi mingi utadhani aliambiwa hawatakuja watu wengine kufanya.haya mambo ni kupokezana vijiti unajikuna unapoweza unaachia wengine nao wataendeleza hakujifunza kuwa alianza kuyafanya nyerere na hakuweza kumaliza.
Mkuu ukipewa nafasi fanya kwa sehemu yako bila kufikiria kuwa Kuna mwingine atakuja. Otherwise wewe una itilafu kichwani Kuna fyuzi imelegea.
 
1. Mabweni ya Chuo Kikuu Cha DAR ES SALAAM
2. Tazara flyover
3. Ubungo flyover
4. Mv. Hapa Kazi TU
5. Mv Mbeya
6. Daraja la Mkupita
Jamani leo ikiwa ni siku ya mazishi yake haki yake tumpeni kila mradi alioukamisha tuutaje
Namba 2 hapo hakuuanza yeye. JK alishauanza na ulikuwa almost done.
 
Kwakweli vituo vya afya kila kata ni msingi mzuri wa community health. Vikipata maji ya uhakika na umeme, mafridge ya kuhifadhia dawa na wataalamu wenye sifa. Mzigo mkubwa kwenye hospitali za rufaa utapungua.

RIP Magufuli.
 
Katika kusoma wasifu wake sikuona sehemu yoyote ile Kabudi akitaja ujenzi wa Tanzania ya viwanda, sambamba na kuanzishwa kwa viwanda vipya zaidi ya 3,000 vilivyotapakaa nchi nzima.
 
Katika kusoma wasifu wake sikuona sehemu yoyote ile Kabudi akitaja ujenzi wa Tanzania ya viwanda, sambamba na kuanzishwa kwa viwanda vipya zaidi ya 3,000 vilivyotapakaa nchi nzima.
Hii ndiyo Tanzania Bwana.
 
Tazara flyover siyo mradi wa awamu ya tano ulikuwa wa awamu ya nne kwa hiyo uundolewe

Jambo jingine ni elimu bure
Malipo kwa control no
Ununuzi wa ndege mpya
Mradi kabla ya kufikia level ya detailed project design , bado upo katika barua ya uchumba (kutongoza), fly over ya Tazara imejengwa na Magufuli.

Bora ungesema reli ya SGR ni Kikwete kwa sababu level ya Detailed Project Design tayari ulifikia na kuombewa pesa (mradi mimba)
 
Back
Top Bottom