Mahakama yavunja ndoa iliyodumu miaka 21 bila wanandoa kushiriki tendo la ndoa

Mahakama yavunja ndoa iliyodumu miaka 21 bila wanandoa kushiriki tendo la ndoa

Huyo mke aliwahi kuhojiwa alisema alikuwa chokoraa jamaa akamchukua. Inaonyesha maybe kavumilia kwa kutegemea maombi. Au labda kwa sasa anatamani mtoto ila inasikitisha kwa huyo baba
 
Ina maana huyo mzee hajtom. ba kwa miaka yote hiyo anakula ugali tu wa bure
 
Dar es Salaam. Mahakama ya Mwanzo Buguruni imevunja ndoa ya mwimbaji wa nyimbo za injili, Rebecca Magaba na Zabron Maselege baada ya wanandoa hao kutoshiriki tendo la ndoa kwa zaidi ya miaka 18.

Pia, Mahakama hiyo imetoa amri mali zote walizochuma wanandoa hao, ikiwamo shamba la eka 10 lililopo Bagamoyo, maduka mawili yaliyopo Bonyokwa na Mahengo na shamba la miti ya mikaratusi lililopo Kigoma zichukuliwe na Maselege na kiwanja kilichopo Madale kitabaki kwa Rebecca.

Hakimu Mkazi, Mwinyiheri Kondo alisema Mahakama imevunja ndoa hiyo baada ya kuona wanandoa hao wanafanya matendo ya ndoa ambayo si ya kawaida.

Kondo alisema katika ushahidi uliotolewa na Rebecca alidai hawakuwahi kufanya tendo la ndoa tangu wafunge ndoa kutokana na mume wake kutokuwa na korodani.

Alisema kutokana na hilo, Mahakama hiyo imevunja ndoa hiyo, hivyo ndani ya siku 45 haki ya kukata rufaa kwa mdaiwa ipo wazi.

Katika kesi hiyo, Rebecca aliiomba Mahakama hiyo ivunje ndoa hiyo kisheria baada ya kuishi na mume wake kwa miaka 21 bila ya kushiriki tendo la ndoa.


Mwananchi
Dah
 
Imekuaje mpaka mkaja kuweka hii siri hadharani?

Si mgesema tu serikali imevunja ndoa ya Bwn flani na Bi flani?

Mbona imekuwa siri kwa miaka yote 21?

Kazi umbea tu.
 
Mkuu Hivi umesoma kilichoandikwa au nawewe umeamua kuja na nadharia zako tu?,pameandikwa ndoa imevunjwa baada ya kutofanya tendo la ndoa kwa miaka zaidi ya 18,wewe unasema amepelekewa moto akachoka ndo akaamua kuvunja ndoa,bure kabisa.
Mkuu vp kumbe upo??
Nlijua umezikwa na jiwe pamoja
Maana ulikua unalipenda Sana jiwe letu
 
Mkuu vp kumbe upo??
Nlijua umezikwa na jiwe pamoja
Maana ulikua unalipenda Sana jiwe letu
Mkuu nipo bado Allah ananijalia uzima,Mwache mh.apumzike salama,sioni busara kumsema sema.
 
Na bi Rebecca akawa anavumilia tu, ndio maana kuna umuhimu wa kukaguana kabla ili kuona efficiency ya viungo vinavyofanya uwe mke na mume
 
Huyo Rebecca anastahili pongezi kwa uvumilivu, miaka yote hiyo na njaa siyo mchezo. Kilangila.
 
Kawaida ilitakiwa baada tu ya kufunga ndoa kesho yake hiyo ndoa ivunjwe kwa mwanaume kudanganya kuwa ni mwanaume wakati siyo

Rebecca anatakiwa adai fidia kwa kutapeliwa

Vyeti vya ndoa husomeka kuwa wewe ni.mwanaume au mwanamke maaba yaje uko.kikr vizuri au kiume vizuri? ukijibu mimi.mwanau.e au mwanamke ikafika uwa huwezi kitandani maumbile huna ya kike au kiume ndoa inavunjwa na unashitakiwa kea utapeli
 
Na bi Rebecca akawa anavumilia tu, ndio maana kuna umuhimu wa kukaguana kabla ili kuona efficiency ya viungo vinavyofanya uwe mke na mume
Si kukaguana au kulalana keanza kunatakiwa tu kuwa mjweki huyo mwanaume alikuwa tapeli Rebecca alitakiwa amburuze mahakamani na amdai fidia siku ya pili tu toka waoane
 
Back
Top Bottom