Mahakamani 28 Septemba: Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI

SEHEMU 7.

Lissu: β€œThe undercover witnesses were arrested by the Police because they were engaging in violence…”

β€œIt’s true, upon the arrest, they admitted…”

β€œThese acts indeed…”

β€œWhen they were brought before the Court…”

Kwamba waliwakamatwa kwa sababu walikuwa wanapanga kufanya vitendo vya uhalifu.

Walikiri kwa maandishi kwenye vituo vya polisi.

Walipelekwa Mahakamani na wakakiri Mahakamani kwamba walikuwa wanapanga vitendo vya uhalifu.

Halafu baadaye tukazungumza na ma-RCO kwamba hao walikuwa wanapanga vitendo vya uhalifu kwa sababu wamechochewa na Tundu Lissu.

Na kama wamechochewa na Lissu na wamekiri hapa Mahakamani, hawa hawana kesi. Kwa sababu hawana kosa, wafutieni kesi.

Je, wangekuja kuwakana hawa waliowafutia kesi hapa Mahakamani?

Ni mashahidi wa namna gani, ambao wamefutiwa kesi na polisi, waje kutoa ushahidi Mahakamani?

Mnategemea nini? Waje kusema ukweli Mahakamani?

Waheshimiwa Majaji, ukurasa wa 448, PW16 aliiambia Mahakama kwamba:

Mwanzoni alikuwa amewaelekeza subordinates wake kwamba: β€œRudisheni hayo mafaili mikoani.”

β€œWatafuteni hao watu, wakamateni, waandikisheni maelezo yao upya kama mashahidi kwenye kesi hii.”

Kwa hiyo, mashahidi wa mafichoni ni mashahidi waliokamatwa, baada ya kuachiliwa wakaandikiwa maelezo, wakaja kutoa ushahidi.

Ndiyo maana, Waheshimiwa Majaji, kila mmoja hapa alikuwa HAPANA, HAPANA, HAPANA, kwamba hawa mashahidi wametishiwa.

Kumbe hawajatishiwa na mtu yeyote.

Hao ndiyo mashahidi wa kesi ya uhaini ambao wanategemewa, Waheshimiwa Majaji, mnikute na hatia.

Sheria inasemaje kuhusu mashahidi wa namna hii?

Waheshimiwa Majaji, Mahakama zetu za juu kwa muda mrefu zimetambua hatari ya kutegemea ushahidi wa mashahidi wa namna hiyo.

Mashahidi wenye maslahi ambao wanaambiwa: β€œTutakufutia kesi ukikubali kutoa ushahidi, tumfunge yule.”

Waheshimiwa Majaji, nawaalikeni kwenye kesi ya Abraham Sagulani dhidi ya Jamhuri, 1991 TLR 265.

Mahakama ya Rufani katika kesi hii iliamua yafuatayo kuhusu mashahidi wenye maslahi:

Ushahidi wa shahidi huyo mwenye maslahi unatakiwa kuangaliwa kwa umakini mkubwa.

Na hautakiwi kutumiwa isipokuwa tu umethibitishwa na mashahidi wengine walio huru.

Msimamo huo upo pia katika kesi ya Asia Iddi dhidi ya Jamhuri, 1999 TLR 174.

Na kesi ya Jamhuri dhidi ya Justice Rumima (Supra), pamoja na kesi ya Basilio John Mlayi dhidi ya Jamhuri, Criminal Appeal No. 306 of 2018, Court of Appeal, Arusha, October 2022, ukurasa wa 25.

Vilevile, kesi hizo zimezungumzia hiyo dhana ya mashahidi wenye maslahi.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Hello gentleman,
umesahau busara ya kutukana kwa mtiririko ambao wadau wa Jf wanakufahamu nao,

vipi umekombolewa kutoka kwenye giza la kuporomosha matusi jukwaani na hatimae kua kiumbe kipya kwenye nuru ya hekima na busara?

au ni drama na unafiki wako tu wa kiwango cha juu sana jukwaani?πŸ’
 
Gentleman,
napigania huyo mtuhumiwa wa uhaini apewa maji ya kunywa ya kutosha kizimbani,

si unajua tena last za safari ya mwisho kiu kinaongezeka?πŸ’
 
TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI

SEHEMU YA 8.

Lissu: Ushahidi wenye maslahi ni ushahidi wa uongo.

Kwa msingi huo nilioutaja, ushahidi wa mashahidi wa mafichoni usitumiwe kabisa, kwa sababu ni ushahidi wenye maslahi na haujathibitishwa.

Waheshimiwa Majaji, ushahidi wa PW5: Mtakumbuka, ndiyo ushahidi wa yule aliyedanganya kuhusu dini yake.

Mahakamani amekula kiapo kama Mkristo, na katika maelezo yake ni Muislamu, Kielelezo D4, ukurasa wa 342 wa rekodi.

Shahidi huyo pia alidanganya kuhusu uanachama wake.

Shahidi mwingine ni PW7, Waheshimiwa Majaji.

Huyu alisema uongo kuhusu kupelekwa Kituo cha Polisi Songea, ukurasa wa 358.

Pia alidanganya kuhusu uanachama wake wa CHADEMA, ukurasa wa 359.

Waheshimiwa Majaji, PW8: Ushahidi wake upo ukurasa wa 363 hadi 364, na ushahidi wote ni mikanganyiko, contradictions, discrepancies and lies.

Waheshimiwa Majaji, PW10: Alidanganya kuhusu maelezo yake polisi, ukurasa wa 377 hadi 378, na alidanganya vilevile kwa maneno yake:

β€œMshtakiwa alisema, β€˜Tumejipanga kufanya fujo kuzuia uchaguzi.’”

Ukurasa wa 376 na 379.

PW11, Waheshimiwa Majaji: Ushahidi wake ulijaa contradictions, discrepancies and untruths.

Upo ukurasa wa 386 hadi 388.

Waheshimiwa Majaji, PW13: Huyu alidanganya juu ya uanachama wake wa CHADEMA.

Katika maelezo yake kizimbani alisema, β€œMimi ni mwanachama wa CHADEMA.”

Alipoambiwa, β€œTuelezee uanachama wako,” akasema, β€œBado sijawa mwanachama,” ukurasa wa 369.

Shahidi wa mwisho ni PW14: Alidanganya kuhusiana na kazi yake.

Kule polisi, katika maelezo yake, alisema yeye ni mkulima katika eneo la Mwakibete.

Na hapa Mahakamani akasema yeye ni fundi umeme wa Jiji la Mbeya.

Anasema nimesema kwamba, β€œLazima tulichafue.”

Shitaka linasema nimesema, β€œLazima tukinukishe,” yeye akasema, β€œLazima tukichafua.”

Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, katika mashahidi tisa wa mafichoni, mashahidi saba ushahidi wao ni wa uongo na hautakiwi kuguswa bila kuthibitishwa.

Na hakuna ushahidi ulioletwa nje ya polisi.

Maana yake ni kwamba huo ushahidi hautakiwi kuchukuliwa.

Unabaki ushahidi wa PW17, ambao wote umeniunga mkono.

Waheshimiwa Majaji, as a matter of general principle, evidence is required relatively rather than…

Nuzah Viking @ Babu Seya dhidi ya Jamhuri (Supra) na Oscar Lwela.

Ushahidi unapaswa upimwe kwa ujumla wake.

Nimezungumzia ushahidi wa mashitaka kwa ujumla wake na individual components.

Waheshimiwa Majaji, swali la kujiuliza: Ushahidi wa mashitaka unalinganaje na ule wa utetezi?

Waheshimiwa Majaji, ushahidi wa upande wa mashitaka upo tofauti na ushahidi wa upande wa utetezi na mashahidi wake.

Nianze na mashahidi wa utetezi. Ni mashahidi wa namna gani?

Mashahidi wa upande wa utetezi wote walikuwa ni viongozi wa juu, wanaojulikana, wenye uzoefu wa kisiasa na viongozi wenye sifa njema.

Ndiyo waliokuja kutoa ushahidi wa utetezi.

DWI mimi mwenyewe, Waheshimiwa Majaji.

Mwanaharakati anayejulikana kimataifa kwa kupigania demokrasia na haki za binadamu.

Na internationally respected.

National Chairman of the Opposition Party (the largest opposition party).

Jaji Ndunguru: Ni lazima uwataje wote?

Lissu: I am only summarising. Labda niseme kwenye rekodi za Mahakama ushahidi wake upo wapi.

Ukurasa wa 559 hadi 563, na 566 hadi 577.

Hizo sehemu mbili zinazungumzia wasifu wa Shahidi Na. 1 wa utetezi.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
(PW1) Bagyemu alifunguwa shauri kana kwamba kesi ni ya wizi wa maembe, pia hakuchukuwa Muongozo kutoka kwa ZPC wa kanda yake. Yaani kajichukulia maamuzi binafsi toka mwanzo, amekuwa juu ya wakuu wake.
Hahahaha, Dah nakumbuka nilipitia ushaidi wote wa kesi hii, Ushaidi wa mashitaka na utetezi lakini sikuwai kuwaza kama alivyo waza lissu hapa. Yaani PW1 anasema hapakuwa na Mwanasheria yeyote lakini baadae sana baada ya mashaidi wengine kuletwa PW16 anasema kulikuwa na afisa kutoka ofisi ya DPP na akashindwa kumtaja jina kwa kisinhizio cha jina lake ni gumu sana and then at the same time DPP alikuwa hajui kuhusu shauri hilo kwamba PW1 anasema mawasiliano yalikuwepo mtaandaoni kwamba hatakuwa alikuwa anajua bila kuambiwa alafu tena hapo hapo afisa kutoka kwenye ofisi yake yupo kwenye upelelezi wa shauri hilo.

Kwa maoni yangu PW1 aliunda kesi, akaifunguwa, hakupokea muongozo kutoka kwa ZPC wake wa kanda, Akumueleza DPP, hakuwa na mwanasheria yeyeto kwenye upelelezi. DPP hajui lakini wanaisi atakuwa anajua kwasabu kila kitu kilikuwepo mtandaoni. Kisha wanavutana wao kwa wao kwenye ushaidi wao yaani PW1 anasema hapakuwa na mwanasheria wala DPP hakuambiwa. Kisha baada ya siku kazaa baadae PW16 anasema Afisa wa ofisi ya DPP alikuwepo lakini jina hatumjui.
 
πŸ˜…
 
TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI

SEHEMU YA 9.

LISSU: Waheshimiwa Majaji, DW2 ni Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Kipekee wa CHADEMA.

Wasifu wake upo katika ukurasa wa 658, 682 hadi 685, 706 hadi 707 na 725 wa rekodi ya Mahakama.

Mtaina wasifu wa Shahidi namba 2.

Waheshimiwa Majaji, DW3 ni Amani Sam Golugwa, Deputy Secretary General of CHADEMA, Kiongozi wa Pekee wa CHADEMA.

Wasifu wake upo katika ukurasa wa 730, 754 hadi 759 na 764 wa rekodi ya Mahakama.

DW4 ni Director of Communication and Publication.

Wasifu wake upo katika ukurasa wa 798, 807 hadi 810, 814, 821, 827 hadi 828.

DW5 ni John Wegesa Heche, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Kiongozi wa Juu na Mbunge wa Kipekee wa CHADEMA.

Wasifu wake upo katika ukurasa wa 835 hadi 837, 839 hadi 845, 855 hadi 856 na 892 hadi 896.

Hao ndiyo watu waliokuja kutoa ushahidi.

Watu wa maana kabisa.

Watu wanaojulikana, si watu wa mafichoni.

Waheshimiwa Majaji, mashahidi wote wa Upande wa Utetezi walikuwa ni mashahidi wa kuona.

Ukililinganisha na mashahidi wa Upande wa Mashitaka, wote isipokuwa mmoja hawakuwepo, isipokuwa mmoja aliyekuwepo na yeye ameungana na mashahidi wa Utetezi wote.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…