TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI
SEHEMU YA 4.
Lissu: Waheshimiwa Majaji, kuhusu kutotoa taarifa wala kuomba mwongozo kwa ZPC, ushahidi huo upo katika ukurasa wa 148 wa rekodi.
Jambo la pili, Waheshimiwa Majaji: PW1 hakuomba wala hakupata ushauri wowote wa kisheria kabla hajafungua faili na baada ya kufungua faili.
(Before and after opening the file, the treason file.)
Na hilo, Waheshimiwa Majaji, nitalirudia: hakuomba wala hakupata any legal advice.
Ushahidi unasemaje? Kwenye ukurasa wa 159:
Kuanzia tarehe 4, siku aliyoonyeshwa video, mpaka tarehe 8 Aprili, anasema alitoa taarifa kwa DPP kuhusu kufunguliwa kwa kesi.
Na katika ukurasa wa 162 anasema hakumtaarifu DPP kuhusu kufunguliwa kwa kesi.
PW1 anatambua sheria inataka nini.
Sheria inataka Mwendesha Mashitaka ajulishwe kwa kesi yoyote inayohusu adhabu ya kifo.
Anasema, “Sikumjulisha.”
Halafu anasema anatambua kwamba Ofisi ya DPP ndiyo inayoratibu upelelezi wa makosa ya namna hii.
Anasema DPP alikuwa anapata taarifa mtandaoni.
Je, alikuwa anapata taarifa namna gani mtandaoni kama hawakumjulisha?
Na, Waheshimiwa Majaji, katika ushahidi wa Mashitaka 17, mimi sikumbuki DPP Mwakitalu au msaidizi wake aje kuthibitisha kwamba alijulishwa kuhusu mashitaka ili aweze kuratibu upelelezi.
Jambo la tatu, Waheshimiwa Majaji, ni kwamba hiyo timu ya wapelelezi wote haikuwa na mwanasheria hata mmoja.
Ilikuwa na polisi tu.
Hawakuwa na mwanasheria wa kuwawezesha kujua kama wanavunja sheria.
Walikaa polisi ambao hawakuwa na uelewa wa sheria.
Ushahidi unasemaje?
Ukurasa wa 158, PW1 ametaja majina ya timu yake ya upelelezi.
Ukiangalia hiyo timu, wote ni polisi na hakuna mwanasheria hata mmoja.
Anasema, ukurasa wa 158:
PW1: “I then formed a team of investigation: Assistant Inspector Michael Kyumi, Assistant Inspector Ibrahim, Assistant Inspector Ruben Mwakabonga, D/Corporal Ibrahim, D/Corporal Ramadhani and myself.”
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.