Mahakamani 28 Septemba: Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

Mahakamani 28 Septemba: Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

Hapa anamaana gani? Sijaelewa
Kuna mawakili hapo mwanzo walikuwa wanazuiwa kutokumuon Lissu mahabusu kwasababu zao wenyewe ccm. Sasa kutokana na kwamba mawakili wake hawakuruhusiwa ndio aliamua kujitetea mwenyewe kutoka toka mwanzo ndio maana akasema yote yasingetokea hayo kama hawo mawakili wake wangekuwa wanaruhusiwa kumuona mteja wao ili wamtetee mahakamani, ndio yeye mwenyewe hufanya kazi hiyo na imemfanya kuchukua mda wote wa kujisomea na kuchambua kila kitu kwasababu usaidizi wa kutetewa haukupatikana.

Ndio nilivyofahamu mm kama ulikuwa unafuatilia hii kesi toka mwanzo.
 
Na kwa kweli uamuzi wa kujitetea mwenyewe umefanya utetezi wake uwe bora sana. Siamini kama mawakili wake wangefanya kama alivyofanya yeye kwa ubora huo.
 
Mwanzo wa kesi alikua akienda kizimbani na kiporo cha ubwabwa na maharagwe, wafuasi wake wakamcheka na kumwambia aache njaa kali, kiporo husababisha changamoto za minyoo ndio akaacha,

Baada ya,
heche,amani na brenda kumkaanga na kumsagia kunguni mahakamani, na kuona kabisa kitanzi hiki hapa,

sasa anajikuta ana kiu mbaya sana,
usingizi kama wote,
.Si unajua tena last moments za mja wa Allah akiwa anaelekea ku r.i.p?🐒
Samahan wee jinsia gani?
 
Attachments

  • 550D3528-9DFB-430A-8BD8-CFEB53C06683.jpeg
    550D3528-9DFB-430A-8BD8-CFEB53C06683.jpeg
    218 KB · Views: 9
Uyu jaji Ndunguru ukiangalia ni kama hoja za Lissu zinachoma hivi sema ndio vile Majaji wanateuliwa na Rais Sasa najiuliza hii kesi imefikaje apa kumbe ilikua Haina hata utaratibu mzuri wa kesi

Sasa kesi kubwa Kama hii yaani imeanzishwa kiholela holela tuh Majaji wakiambiwa wana matatizo wanabisha wakati inaonekana wazi kabisa
 
Majaji wako hoi hawajui watende haki, au wafuate maagizo ya watawala dhalimu.

Ni aidha walinde heshima ya mahakama hata hii kdg iliyobaki, au waipoteze na kuitoa kabisa, mmatengo na wenzake ndio wataamua.
Dhana potofu.
 
Uyu jaji Ndunguru ukiangalia ni kama hoja za Lissu zinachoma hivi sema ndio vile Majaji wanateuliwa na Rais Sasa najiuliza hii kesi imefikaje apa kumbe ilikua Haina hata utaratibu mzuri wa kesi

Sasa kesi kubwa Kama hii yaani imeanzishwa kiholela holela tuh Majaji wakiambiwa wana matatizo wanabisha wakati inaonekana wazi kabisa
Jaji anamsikiliza maana hamkawii kusema anaonewa, anaachwa amalize aridhike hukumu awaachie majaji, juzi jaji alimwambia jielekeze kwenye yale ya msingi na alikuwa anamhimiza amalize lkn lissu anadhani kuongea sana ndio kushinda kesi.
 
UCHAMBUZI NA TATHIMINI YANGU

Katika Hatua hii ya Kesi "Final Submission" LISSU akijitetea mwenyewe kwa kufanya Final ya Ushaidi, hoja na Kukosoa miendendo ya Kesi, Mashaidi wa mashtaka na Mengineyo mengi. Linaibuka swali la Kisheria.

Je, maneno yanayodaiwa kusemwa tarehe 3 Aprili 2025 yanaweza kumtia hatiani hasa kwa mujibu wa Kifungu cha 39(2)(d) cha Penal Code. hili kutimiza vipengele vyote vya kosa la uhaini na kama ndiyo, Jamhuri imevithibitisha kwa ushahidi unaotakiwa kisheria?

LISSU
anaonyesha sehemu zote za Sheria za Nchi kwamba Hakuna Sheria unayosema ni Kosa kusema maneno haliyosema. Hoja iliyobaki sasa ni Kuhusu Kifungu cha 39(2)(d), kwamba Je maneno Yale yanaingia kwenye Kifungu hicho.?

Kifungu cha 39 cha Penal Code kinahusu moja ya makosa mazito zaidi katika mfumo wa sheria ya Tanzania. Chini ya 39(2)(d), hoja si kwamba mtu alisema jambo ambalo serikali haikulipenda, Yaani maneno ya Kisiasa yanaweza kukuumiza wewe mpinzani wa Kisiasa lakini je Yana Nguvu ya kisheria.

Sheria inataka kitu maalumu zaidi:
Nia ya kutenda kitendo cha uhaini + Namna nia hiyo ilivyodhihirishwa + Kitendo kinachokidhi matakwa ya sheria. = "Uhaini unakuwa umethibitishwa".

Na kwa sababu hii ni kesi ya jinai, swali halipaswi kuwa:
Je, maneno ya Lissu yanaweza kutafsiriwa kama tishio?

Bali:
Je, Jamhuri imethibitisha kila kipengele kinachounda kosa linalodaiwa, kwa kiwango kinachotakiwa katika kesi ya jinai?

Kifungu cha 39(2) kinahusu mtu mwenye allegiance kwa Jamhuri ya Muungano ambaye anatengeneza nia ya kufanya matendo fulani ya uhaini na anaidhihirisha nia hiyo kwa maandishi, uchapishaji, au overt act/deed.

Katika 39(2)(d), mojawapo ya matendo yaliyotajwa ni:
Intimidation of the Executive, the Legislature or the Judiciary of the United Republic.

Na sheria inaunganisha hilo na requirement ya kuonyesha nia kupitia writing/printing au overt act/deed.

Hapa ndipo tofauti muhimu inapoanzia.
Kuna tofauti kati ya:

A. kusema jambo kali dhidi ya Serikali;
B. kutaka Serikali ibadilike;
C. kutaka uchaguzi usifanyike;
D. kushawishi watu wasishiriki uchaguzi; na
E. kutengeneza nia ya kuishurutisha/kuitisha Executive, Legislature au Judiciary kwa namna ambayo sheria imeifanya kuwa treason.

Mambo yote Hapo juu si vitu vinavyoweza kuchukuliwa kuwa kitu kimoja bila uchambuzi, Ushaidi, na Sheria inavyosema.

Moja ya sehemu nzito sana ya kesi hii ni kama ifuatavyo.
Kwa mujibu wa taarifa za kesi, maneno yanayodaiwa ni pamoja na:
“we will stop the election”
“we will disrupt this election”
“we will mobilise rebellion”

Jamhuri inayaunganisha maneno hayo na nia ya kutishia Serikali. Lakini hapa kuna chain of reasoning ambayo Mahakama inapaswa kuichunguza:
Maneno → Maana iliyokusudiwa → Nia → Kitendo kinachokusudiwa → Target → Intimidation ya taasisi iliyotajwa na 39(2)(d).

Kama kiungo kimoja hakipo, swali linakuwa kama chain nzima imethibitishwa.

Kwa mfano:
“Tutazuia uchaguzi.” Hilo linaweza kuwa kauli ya kisiasa.
Lakini ili liingie kwenye 39(2)(d), lazima ionyeshwe kwa nini kauli hiyo, katika mazingira hayo, ilikuwa manifestation ya nia ya kufanya moja ya matendo yaliyotajwa na kifungu hicho.

Hapo ndipo ushahidi wa mazingira yote ya mkutano unakuwa muhimu.

Pia Hili linaweza kuonekana kama technicality ndogo, Lakini si lazima iwe ndogo.
Katika kesi ya jinai, hati ya mashitaka inapaswa kumpa mshtakiwa taarifa inayomruhusu kuelewa:
“Ninashitakiwa kwa kufanya nini, dhidi ya nani, lini, wapi na kwa namna gani?”

Hii ndiyo logic inayohusishwa na section 132 ya Criminal Procedure Act, inayohitaji charge kutoa particulars zinazohitajika kumpa accused taarifa ya kutosha kuhusu nature ya offence.
Na kuna precedent ya Freeman Aikael Mbowe & Others v Republic, ambako Mahakama ilijadili tatizo la charge kutotaja jamii/persons waliolengwa na kauli zinazodaiwa kuwa za jinai.

Kwa hiyo swali la msingi ni:
“The public” ni nani hasa?
Kwa sababu kama target ni:
• wananchi wote Tanzania,
• wapiga kura,
• wanachama wa CHADEMA,
• waandikishaji wapiga kura,
• Tume ya Uchaguzi,
• Serikali,
• viongozi wa Serikali.

hizo ni categories tofauti kabisa.
Na kila moja inaweza kubadilisha namna ya kutafsiri nia.

Ukisema alikuwa analenga kushawishi Umma (the public) kwamba ni Wananchi wote maana yake hata Rais, Polisi, mwanaJeshi, Jaji, Mwanasiasa, au Mtu mwengine yeyote ni mwananchi, na hapo ndipo ugumu unapotekea kwamba haiwezekani kuchukuwa watu kazaa Kuthibitisha kuwa walichochewa kufanya Jambo Fulani Wakati unaongelea Jambo la Wananchi Wote, Hili linaibuka hoja Je watu Hao Wana Mamlaka ya Kuthibitisha Uhalali wa Wananchi wote kushawishiwa...?

Kwa Maoni yangu Watu wale wa vificho awatoshi Kuthibitisha kwamba hata Mimi, au Mtu mwengine yeyote alishawishiwa Kwa maneno ya LISSU maana Hilo Neno (the public) ni Pana Sana Ndio maana Kifungu cha 39 cha Panel code kimesema kundi la watu, au Mtu na sio Umma wote. Kwasababu Kisheria Kuthibitisha Umma wote ulishawishika na maneno Yale ni ngumu Sana, "Kama uhamuzi utakuwa Neno (the public) ni sahihi Basi Nchi Nzima iulizwe kwamba ilishawishika Kuhusu maneno ya LISSU aliyoyatoa", Mimi sikotayari kuthibitishiwa kwamba nilishawishika au la Kwa Mtu wa kificho.
 
Kuna mawakili hapo mwanzo walikuwa wanazuiwa kutokumuon Lissu mahabusu kwasababu zao wenyewe ccm. Sasa kutokana na kwamba mawakili wake hawakuruhusiwa ndio aliamua kujitetea mwenyewe kutoka toka mwanzo ndio maana akasema yote yasingetokea hayo kama hawo mawakili wake wangekuwa wanaruhusiwa kumuona mteja wao ili wamtetee mahakamani, ndio yeye mwenyewe hufanya kazi hiyo na imemfanya kuchukua mda wote wa kujisomea na kuchambua kila kitu kwasababu usaidizi wa kutetewa haukupatikana.

Ndio nilivyofahamu mm kama ulikuwa unafuatilia hii kesi toka mwanzo.
Hapa nimekupata kijana
 
Jaji anamsikiliza maana hamkawii kusema anaonewa, anaachwa amalize aridhike hukumu awaachie majaji, juzi jaji alimwambia jielekeze kwenye yale ya msingi na alikuwa anamhimiza amalize lkn lissu anadhani kuongea sana ndio kushinda kesi.
Lissu lazima aeleze kwa mapana kwa namna ambavyo haitatoa mwanya wowote kwa wanaomshtaki kwasababu Hana Imani na majaji kwa asilimia zote
 
Back
Top Bottom