sawa Delilah,Sitashangaa tena baada ya leo
Sawa Samson π π
πTUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI
SEHEMU YA 4.
Lissu: Waheshimiwa Majaji, kuhusu kutotoa taarifa wala kuomba mwongozo kwa ZPC, ushahidi huo upo katika ukurasa wa 148 wa rekodi.
Jambo la pili, Waheshimiwa Majaji: PW1 hakuomba wala hakupata ushauri wowote wa kisheria kabla hajafungua faili na baada ya kufungua faili.
(Before and after opening the file, the treason file.)
Na hilo, Waheshimiwa Majaji, nitalirudia: hakuomba wala hakupata any legal advice.
Ushahidi unasemaje? Kwenye ukurasa wa 159:
Kuanzia tarehe 4, siku aliyoonyeshwa video, mpaka tarehe 8 Aprili, anasema alitoa taarifa kwa DPP kuhusu kufunguliwa kwa kesi.
Na katika ukurasa wa 162 anasema hakumtaarifu DPP kuhusu kufunguliwa kwa kesi.
PW1 anatambua sheria inataka nini.
Sheria inataka Mwendesha Mashitaka ajulishwe kwa kesi yoyote inayohusu adhabu ya kifo.
Anasema, βSikumjulisha.β
Halafu anasema anatambua kwamba Ofisi ya DPP ndiyo inayoratibu upelelezi wa makosa ya namna hii.
Anasema DPP alikuwa anapata taarifa mtandaoni.
Je, alikuwa anapata taarifa namna gani mtandaoni kama hawakumjulisha?
Na, Waheshimiwa Majaji, katika ushahidi wa Mashitaka 17, mimi sikumbuki DPP Mwakitalu au msaidizi wake aje kuthibitisha kwamba alijulishwa kuhusu mashitaka ili aweze kuratibu upelelezi.
Jambo la tatu, Waheshimiwa Majaji, ni kwamba hiyo timu ya wapelelezi wote haikuwa na mwanasheria hata mmoja.
Ilikuwa na polisi tu.
Hawakuwa na mwanasheria wa kuwawezesha kujua kama wanavunja sheria.
Walikaa polisi ambao hawakuwa na uelewa wa sheria.
Ushahidi unasemaje?
Ukurasa wa 158, PW1 ametaja majina ya timu yake ya upelelezi.
Ukiangalia hiyo timu, wote ni polisi na hakuna mwanasheria hata mmoja.
Anasema, ukurasa wa 158:
PW1: βI then formed a team of investigation: Assistant Inspector Michael Kyumi, Assistant Inspector Ibrahim, Assistant Inspector Ruben Mwakabonga, D/Corporal Ibrahim, D/Corporal Ramadhani and myself.β
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
Si ndio anafunga kila kitu leo, napenda anapokazia sehemu ambayo kina Katuga wangeanzia nayo. Yeye anasawazisha kila kitu.Kipande Cha leo Lissu amekusanya nukta(points) muhimu za ushindi.
Yaani Lissu ni mbabe sana kwenye sheria. The guy knowsSi ndio anafunga kila kitu leo, napenda anapokazia sehemu ambayo kina Katuga wangeanzia nayo. Yeye anasawazisha kila kitu.
Lissu ana balaa.
MAHAKAMA IMEANZA TUNDU LISSU ANABISHANA KIDOGO NA MAJAJI KISHA ANAENDELEA.
SEHEMU YA 1. TAREHE 28.9.2026.
MAHAKAMA INAANZA HAPA
Ameingia Lissu, kisha wakafuatia Majaji kwa pamoja.
Karani wa Mahakama: Anaanza kusoma Criminal Session, Kesi Na. 19605 ya mwaka 2025, Jamhuri dhidi ya Tundu Antipas Lissu.
Anasimama Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga.
Nassoro Katuga: Iwapendeze Mahakama hii Tukufu, Waheshimiwa Majaji wa Mahakama hii Kuu. Naitwa Nassoro Katuga, Wakili wa Serikali Mkuu. Nipo pamoja na:
1. Job Mrema, Wakili wa Serikali Mkuu
2. Ignas Mwinuka, Wakili wa Serikali Mkuu
3. Tawabu Issa, Wakili Mwandamizi
4. Cuthbert Mbilinyi, Wakili wa Serikali
5. Winniwa Kasara, Wakili wa Serikali
Waheshimiwa, jopo la mawakili sita linaiwakilisha Jamhuri, na mshtakiwa yupo kizimbani.
Shauri limekuja kwa ajili ya mawasilisho ya mshtakiwa.
Sisi upande wa Jamhuri tupo tayari. Sijui mwenzetu.
Jaji Ndunguru: Mshtakiwa?
Lissu: Nipo tayari, Mheshimiwa Jaji.
Jaji Ndunguru: Tuendelee.
Unakumbuka Ijumaa wakati tunahairisha ulikuwa umemaliza hoja ya saba. Tuanze ya nane.
Lissu: Waheshimiwa Majaji, nawashukuru sana.
Waheshimiwa Majaji, kabla sijazungumza ya leo, naomba niseme yafuatayo.
Na haya nayazungumza kwa sababu leo namaliza hoja yangu ya mawasilisho.
Jaji Ndunguru: Katika session hii ya asubuhi?
Lissu: Hilo siwezi kusema.
Kwa sababu leo namalizia kuwasilisha, kuna maneno ambayo naweza nisiyazungumze tena.
Naomba sasa kusema mbele ya Majaji yale ambayo nilitaka kusema.
Jaji Ndunguru: Kwanini usiyaweke mwisho, tukupe muda ili twende kwa mtiririko?
Lissu: Hilo nalo ni gumu. Kwa kweli, naomba muda niweze kusema.
Lissu: Hoja ya nane inauliza kama, kwa kuzingatia majibu ya hoja saba zilizotangulia, upande wa mashitaka umethibitisha mashitaka yake kwa kiwango cha uthibitisho kinachotakiwa na sheria.
Kiwango cha uthibitisho kinachotakiwa na sheria katika kesi ya jinai kama hii ni uthibitisho usioacha shaka yoyote ya msingi β Proof Beyond Reasonable Doubt.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
Hakika kabisa na haipingwi.Yaani Lissu ni mbabe sana kwenye sheria. The guy knows
Hiyo picha ya pro, inachekesha ni nani huyo? Nikamfuatilie.yule bi kizee, lazima aanguke na kukimbizwa kwa waganga
Hii inastaajabisha sana hata kwa alfabet walishindwa!akashindwa kumtaja jina kwa kisinhizio cha jina lake ni gumu sana
Nachoelewa haki ni moja tu, dushe ndani ya rinda!Lete updates tuko hapa, hadi Haki ipatikane.
Watu wanakana mpaka dini zao kisa mihamala dah! Mtu kama huyu si anaweza kuvua hata ubingwa wake hii Hali inatisha kwa kweliKwa maoni yangu: PW5 nae ni shaidi wa mchongo.
Sijawai kuona mtu aneweza kuikana dini yake, yani hata uniamshe usingizini nitasema dini yangu ni fulani tu, hata iweje siwezi kujiingiza kwenye sehemu isiyo yangu. Huyu ni shaidi muongo
Lissu kaamua kufika mbali huko kwasababu kaona pesa inaweza kununua utu wa mtu ndio maana kawakaba kila Kona ili waone soni kwenye maamuziMajaji wamenyimwa sababu ya kutotenda haki, alichokifanya Lissu ni kuwasaidia jinsi ya kuandika Hukumu ya Kesiβ¦kwa kifupi amefanya kazi ya Majaji, uamuzi ni wao kuendelea kuwa MAJAJI au kuanza kuitwa MAJAGI.
Ifike mahala watu wakubali tu kwamba jamaa ni next levelLissu kaamua kufika mbali huko kwasababu kaona pesa inaweza kununua utu wa mtu ndio maana kawakaba kila Kona ili waone soni kwenye maamuzi