Mahakamani 29 Septemba 2026: Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

Anataka pia kupendekeza vijiadhabu vidogo vidogo ili tu kumuondolea TAL credibility kwenye kugombea madaraka ya umma. Yeye alishasema hakuna hiyo! Ni ama umnyonge au umuachie huru. Katuga asilete Ukatuga (Ukilaza) wake kuturubuni hapa.
Ilikuwa auawe kwa risasi ili asishiriki siasa kabisa akapona kwa sasa wanataka afungwe kabisa,huu wote ni woga laa!
 
Final submission ni namna wanavyoshawishiwa majaji na kila upande, majaji wanajua wanachokifanya tutulie kama hana hatia au anayo kwa namna majaji watakavyoona itaamuliwa ufurahi au uchukie, wakati mtu wenu anaelezea tulitulia kaachwa kasema kamaliza siku 4 sasa zamu ya katuga kuelezea kuweni wavumilivu, utawala wa sheria unachukua mkondo wake.
 
Halafu huyo "katuga" mbona hamalizi hiyo submission wakati alisema atachukua muda mfupi au ameenda kusikiliza maoni kutoka CCM?
 
..UHAINI ni kosa ambalo liko very clear.

..kama kweli uhaini umetendeka Katuga asingelazimika kutumia maarifa na ubunifu mkubwa kujaribu kuifafanulia mahakama.
hata lissu asingetumia siku 4 kujitetea.
 
Huyu katuga mbona mimi simuelewi wakuu
 
..UHAINI ni kosa ambalo liko very clear.

..kama kweli uhaini umetendeka Katuga asingelazimika kutumia maarifa na ubunifu mkubwa kujaribu kuifafanulia mahakama.
Lissu alitumia zaidi ya siku mbili, acheni nao watumie haki yao
 
Mi naona upande wa serikali wanazunguka tu
moja kwenye kifungu cha 39(2)(d) hakuna mambo ya uttering.Pili ili uweze kumkuta na hatia lazima uthibitishe instigation swali linakuja nani alikuwa instigated,how was that person instigated? When was that group or person instigated and where? Story za kusema Public ilikuwa instigated ni dying horse.

Ukiangalia charge haisemi kama kwenye statement alikuwa anawaambia watu au kuwashawishi cha kufanya bali ni reference ambaye Lissu anamzungumzia anonymous kuwa "wanasema msimamo huu.....Neno tutavuruga uchaguzi au tutakinukisha hayaonyeshi instigation au intimidation bali utterance tu ambayo inahusu mambo ya uchaguzi kama kulikuwa na kosa tume ya uchaguzi au wadau wa uchaguzi ndio walipaswa kulalamika.Jamhuri ilipaswa kuthibisha ni vipi umma ungeathirika au kuathirika kwa uchaguzi kuvurugika au kuvurugwa na stake holders mmoja adhabu zake zipo kwenye sheria ya vyama vya siasa.
 
‪Jamhuri inajaribu kuleta tafsiri au mabadiliko ya kisheria kwamba Mahakama ina utashi (discretion) wa kutoa adhabu ndogo zaidi

Aidha anyongwe au aachwe huru.
Alisha sema muhusika mwenyewe.
... wanaishauri mahakama itoe adhabu mbadala kinyume na sheria inavyoelekeza kuhusiana na kosa aliloshtakiwa nalo 🤣🤣🤣.
 
MAHAKAMA IMEREJEA KUTOKA MAPUMZIKO NASSARO KATUGA ANAENDELEA

SEHEMU YA 9.

MAHAKAMA IMEREJEA

Baada ya mapumziko, shauri linaendelea. Upande wa mashtaka unaendelea kufanya majumuisho.

Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, upande wa mashtaka unathibitisha kuwa mshtakiwa alithibitisha nia kwa kuitisha Serikali ili ifanye yale aliyoyataka.

Hii inatokana na maneno yaliyotamkwa na mshtakiwa na upande wa mashtaka kuyakuu kwenye hati ya mashitaka. Maneno hayo, Waheshimiwa Majaji, bila kuwachosha kwa kuyarejea mara kwa mara, mshtakiwa anasema: kuzuia uchaguzi, kuhamasisha uasi, kukinukisha na ni namna ya kuyapata mabadiliko.

Maneno hayo, namna yalivyokaa, yakithibitishwa kuwa yalitamkwa na mshtakiwa, yanathibitisha kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali.

Kabla ya kuthibitisha kuwa mshtakiwa alitengeneza nia ya kuitishia Serikali, ninawaalika Waheshimiwa Majaji kuiangalia kesi ya Mahendra vs State of Nalkataka and Another, Criminal Appeal No. 18/1238 ya mwaka 2002, katika aya ya 23, ambapo Supreme Court ya India ilitafsiri neno to instigate kuwa ni to provoke, to incite, or encourage the commission of an act to satisfy the requirement of instigation, ingawa si lazima maneno halisi yatumiwe kwa maana hiyo; mwenendo wa uchochezi lazima upendekeze matokeo yanayoweza kutokea kwa mtu mwenye akili ya kawaida.

Nassoro Katuga: Unaweza kuwa uchochezi wa maneno au uchochezi wenye madhara unaojitosheleza, na uchochezi huo uwe una uwezo wa kuwekwa hadharani.

Maneno haya tunaweza kuyapima katika hati ya mashitaka ambayo ni kuchochea umma.

Tunaomba Mahakama hii Tukufu inote maneno haya.

Maneno haya hayakukataliwa wakati wa preliminary hearing, wakati wa undisputed.

Wakati wa Jamhuri kupitia mashahidi wake, ukimtoa PW3, ambaye ni mtaalamu wa ushahidi wa kielektroniki, mashahidi wote walieleza kumsikia mshtakiwa akitamka maneno yaliyonukuliwa kwenye hati ya mashitaka siku ya tarehe 23 Aprili 2025.

Waheshimiwa Majaji, hao mashahidi wote wa upande wa Jamhuri walitumia YouTube channel ya Jambo TV.

Na PW17, ambaye anasema alishuhudia kwa kuwepo eneo la tukio, huyu ndiye yule shahidi wa moja kwa moja.

Waheshimiwa Majaji, wakati wa maswali ya dodoso, hoja kuhusu kutamka maneno hayo, mshtakiwa hakuidodosa.

Ila tu aliibua hoja ya: Je, maneno hayo yanatengeneza kosa?

Waheshimiwa Majaji, tunasema ushahidi huu Mahakama yenu inapaswa kuunote kuwa undisputed, kwa kuwa umeungwa mkono na ushahidi wa mashahidi wote wa upande wa utetezi.

Ushahidi kwamba mshtakiwa alitamka maneno hayo tarehe 23 Aprili 2025 haukudodoshwa. Uliungwa mkono na mashahidi wote, lakini pia uliungwa mkono na mshtakiwa mwenyewe kwamba ni kweli; haya maneno hayakatai.

Lakini anachokipinga ni kwamba yeye hakuyasambaza kwa umma.

Ni maneno ambayo pia yanaungwa mkono na DW2, DW3, DW4 na DW5, wote walikuwepo katika mkutano na wamekiri kusikia matamshi haya.

Ushahidi huu umeungwa mkono na ushahidi wa utetezi.

Ni wazi kuwa hakuna dispute kuhusu mshtakiwa kutamka maneno haya mnamo tarehe 23 Aprili 2025.

Sasa, Waheshimiwa Majaji, wakati mnajiuliza kama haya maneno yanaweza kumchochea mtu au kundi la watu kwa ujumla...

Ni submission ya upande wa Jamhuri kwamba haya maneno, yaliyotokana na hotuba ndefu ya mshtakiwa aliyoitoa tarehe 23 Aprili 2025, ni maneno yenye sentensi timilifu na yenye kueleweka.

Waheshimiwa, ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa Jamhuri umepokea na kuyaeleza haya maneno na kueleza nia ya mshtakiwa.

Ni maneno yaliyokamilika na kueleweka na mashahidi wa upande wa Jamhuri.

Waliotoa ushahidi wao, ambapo ukimchukua PW1, alieleza kwamba maneno haya yalilenga kuitishia Serikali.

Waheshimiwa Majaji, mbali na ushahidi wa upande wa Jamhuri kwamba yale maneno walikuwa wameyaelewa na kuyatafsiri walivyoyatafsiri, bado ushahidi wao unaungwa mkono na ushahidi wa DW3.

Ambaye naye anaunga mkono kwamba maneno yaliyonukuliwa katika hati ya mashitaka ni maneno yaliyotimilika na yanaleta maana.

DW4 pia anaunga mkono kuwa maneno yaliyo katika hati ya mashitaka ni maneno yaliyokamilika na yenye kuleta maana.

Waheshimiwa Majaji, sasa tuyatafsiri basi maneno yenyewe tuone yana maana au hayana maana.

Waheshimiwa Majaji, neno uasi lililotumika hapo limetafsiriwa kwenye Kamusi Kuu ya Kiswahili.

Kwa kumaanisha kwamba uasi ni kitendo cha uvunjaji wa sheria kinachofanywa na kikundi cha watu kwa lengo la kubadili mfumo wa kisiasa wa nchi yao.

Tafsiri ya pili ya neno uasi ni kitendo cha kuwapinga wenye mamlaka au sheria dhidi ya taasisi au chama, kisawe chake ni uhalifu.

Mazingira ya kesi yetu yanatupeleka kuchukua tafsiri ya neno uasi (a).

Ni ushahidi wa DW3 katika ukurasa wa 829 kwamba slogan ya “No Reforms, No Election” ilikuwa na nia ya kuleta mabadiliko kwenye siasa za nchi.

Na Waheshimiwa, kwa shahidi huyu aliposema sentensi zilizotumika kutoka kwenye hati ya mashitaka ni sentensi zilizokamilika na zenye kuleta maana, ukurasa wa 822.

Na katika ukurasa wa 829, shahidi huyu DW3...

Ndiyo jukumu la upande wa utetezi kuthibitisha shitaka la upande wa Jamhuri.

Lakini Waheshimiwa, ni msimamo wa sheria kwamba ushahidi wa Defence unaweza kuibeba mbele kesi ya Jamhuri.

Waheshimiwa, msimamo huu wa kisheria upo katika kesi ya Khamis Chuma @ Hando Muhoja vs Jamhuri, Criminal Appeal No. 36 of 2018, iliyoripotiwa TanzLII tarehe 23 Agosti 2021.

Ukurasa namba 19, ikirejea kesi ya Haruna Mohammed Tupeni and Another vs Jamhuri.

Mahakama ya Rufani ilisema: “If the accused person gives the evidence which carries...”

Kwa hiyo, Waheshimiwa, japo ninawaalika kwenye hii kesi kupitia ushahidi wa Brenda...

Kwa hiyo, tafsiri halisi ya neno uasi tunaipata kwenye maana (a): kikundi cha watu wanaotaka mabadiliko.

Walisema hawakukusudia kwenda Mahakamani, bali Mwenyekiti alikusudia kuanzisha uasi kuleta mabadiliko na hawakujipanga kwenda Mahakamani.

Tafsiri ya neno uasi hapo ilikuwa ni kuanzisha vurugu ili kuleta mabadiliko.

Lakini Waheshimiwa, treasonable intention ya mshtakiwa inathibitishwa kwa kauli zake alizotoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…