Mahakamani 29 Septemba 2026: Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

Mahakamani 29 Septemba 2026: Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

Mashahidi walisema walihamasika kufanya vurugu ila hawapo kwenye mashitaka yoyote bali ni mashahidi wa Jamhuri. Hii nchi imejaa upumbavu mwingi sana.

Serikali ya Sisiemu ni serikali ya kishenzi inatufanya watanzania wote tuonekane wajinga mbele za watu.
 
hii itakuwa fundisho kwenu maana mliwaona mbowe, lipumba, maalim, cheyo, slaa wajinga
 
... Kwa ushauri huo, mahakama haina budi kwrnda na option ya miaka sifuri maana ni mojawapo kati ya adhabu mbili tu za kosa la uhaini - kunyongwa au kuachiwa huru (miaka sifuri)! In fact ndicho alichosema Lissu.
Umeelewa maana ya miaka 0? Akifungwa miezi kati 1-11 ndio maana yake. Ila kafungwa
 
SEHEMU YA 11.

Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, ni wazi sasa kwamba muone kupitia haya maneno kwenye hati ya mashitaka na ushahidi uliotolewa upande wa utetezi, ni wazi kwamba hoja yetu ya pili, kama mshtakiwa ali-form intention to instigate or for the purposes of instigating the Executive...

Ni wazi kwamba tunathibitisha kwamba maneno haya yalilenga kutishia Serikali.

Uchaguzi upo chini ya sheria. Kutishia kuvuruga ni kutishia Serikali.

Ushahidi huo uliungwa mkono na DW2, DW3 na DW4 kwamba muhimili wenye jukumu la kusimamia sheria ni Serikali.

Maneno haya pia yanathibitishwa na PW16 kwamba maneno haya ya kuchochea uasi, kuvuruga uchaguzi, kama ambavyo mpelelezi wa kesi anaeleza, yalikuwa na chuki ya kiwango cha juu, kutishia amani na utulivu wa nchi.

Ambapo DW4 anasema “kukinikisha” ni maneno ya kikundi fulani.

Kitu ambacho PW16 anasema wenye jukumu la kulinda amani na utulivu ni Executive.

Maneno haya yanaungwa mkono na DW1 mwenyewe. Katika ukurasa wa 619 anasema kwamba Serikali ndiyo msimamizi wa sheria.

Chombo ambacho ni responsible to maintain peace and order ni Serikali.

Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, ushahidi wa PW16 unaungwa mkono na DW1 katika ukurasa wa 622 na ukurasa wa 800.

DW4, Brenda, anaunga mkono kwamba Polisi ndiyo wasimamizi wa sheria.

Anakubali kwamba jukumu hili lipo kwa Serikali la maintain peace and order.

Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, ni rahisi sasa kuona kwamba kumbe kutishia, kuchochea umma, kuvunja amani, unakuwa umemtisha mwenye jukumu hilo.

Si Bunge, si Mahakama.

Waheshimiwa, jukumu la Executive katika ensuring public safety and peace limekuwa vested katika Katiba, Ibara ya 30(2).

Lakini pia, Waheshimiwa Majaji, Ibara ya 147(2).

Ni kwa ajili ya watu Watanzania.

Lakini Waheshimiwa Majaji, siyo hayo tu. Ushahidi wa PW16 unaungwa mkono na Kifungu cha 5 cha Sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi Wasidizi, kwamba ni jukumu la Serikali kulinda amani.

Sheria hii inaunga mkono ushahidi wa PW1 na PW16 kwamba Serikali ndiyo yenye jukumu la kusimamia ulinzi na usalama.

Kwa nini mashahidi 3 kati ya 17 ndiyo wameeleza kwamba kwa nini hapa kuna uhaini?

Waheshimiwa, Kifungu cha 152 cha Sheria ya Ushahidi kinasema hakuna namba mahususi ya mashahidi inayotakiwa kutumika kuthibitisha uhaini.

Hata akiwa mmoja anatosha. Hakuna namba fulani; cha msingi awe anajitosheleza.
 
What...! Hivi jamani mbona aibu naona mie, katuga mbona unatuzalilisha wataalamu wa sheria jamani. Yaani anachokisema hapa ni kwamba unaweza kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kesi ya bangi na usiambiwe kabra kwamba kesi yako ni ya bangi.. alafu baadae ujitete kwenye ushaidi wa mastaka. Mfano wa ushaidi huo tuseme hivi Ulibeba gunia tatu za bangi na kumpa Juma na zingine kuzificha kwako, je mnaziuzaga kwa nani bangi hizo?

Alafu wewe ujitete hapo kweli.....
Jamani hii kesi imekaa kisiasa lakini mimi nipo hapa kwa misingi ya kisheria kwaiyo mtu akisema namtetea lissu, please embu fikiria kwanza kuhusu kufunguliwa kesi kabra ya kuijua hiyo kesi yenyewe inahusu nini, yaani unafikisha kizimbani kwa Mauwaji alafu ndo ujitete yaani hata maelezo yako ukuchukuliwa si ndio maana yake.?

Nilishasema toka mwanzo kwenye reply yangu hii kwamba, Katuga kasema kwamba Jamhuri iliandaa hati ya mashtaka kwa kifungu cha 135 cha CPA lakini nikasema kifungu hicho hakimpa accused Taarifa ya kutosha kuhusu Nature ya Offense now anatetea hati yake ya mashtaka kwa kusema kwamba Unaweza kuambiwa baadae kuhusu hilo baada ya kesi kuanza sio lazima kabra ya shauri kufunguliwa.

Ibara ya 34(2) inatoa mamlaka kwa serikali kuhifadhi katiba na mambo yanayotungwa na bunge lakini imeweka mipaka kwa vyombo njee ya bunge. Kwanini hoja hii kwamba "Serikali kazi yake kulinda sheria sio sahihi", kwasababu.

1. Kuchanganya "kutunza sheria" na "kutishia Serikali"
Ingawa Serikali ina wajibu wa kutunza sheria, uhaini chini ya Kifungu cha 39(2)(d) unahusu vitendo vinavyolenga muundo wa kikatiba au usalama wa taifa, si maandamano ya kisiasa kuhusu uchaguzi. "Kutunza sheria" ni wajibu wa kiutawala, si kigezo cha kupanua upeo wa uhaini.

2. Kutegemea mashahidi badala ya vigezo vya kisheria
Ushahidi wa PW1 na PW16 kwamba "maneno yanatishia Serikali" ni maoni ya mashahidi (opinion evidence), si ushahidi wa ukweli wa kisheria. Mahakama haiwezi kutegemea maoni ya mashahidi ili kubaini kama kosa la uhaini limefanyika; ni lazima vigezo vya kisheria vilivyowekwa katika kesi za Grey Likungu na Hatibu Gandhi vitimizwe.
Katuga hapo yuko kwa kazi maalumu na ameahidiwa zawadi nzuri mnoo. Msidhani hajui anajua anachokifanya.
 
Waheshimiwa, mtaona upande wa utetezi hawajauteteresha hata kidogo, zaidi ya “sijui”, “sikumbuki” kuwa nyingi.

Waheshimiwa Majaji, kifungu ambacho tumekirejea cha 3(2)(a) kinataka kuthibitisha beyond reasonable doubt.

Waheshimiwa, ku-prove beyond reasonable doubt haimaanishi kuthibitisha pasipo kuacha kivuli.
Inachekesha na kufurahisha sana!
 
SEHEMU YA 12.

Waheshimiwa Majaji, naomba nihitimishe kwamba tumethibitisha intention.

Hakuna dispute kwamba mshtakiwa alitamka maneno haya.

Hoja iliyobakia hapa ni je, mshtakiwa alisambaza au alichapisha?

Waheshimiwa Majaji, ukiangalia ushahidi, manifestation yake ilifanyika by deed.

Waheshimiwa Majaji, mashitaka yetu ni kwa kutoa na kusambaza, kuyafanya yawe hadharani.

Kutoa maneno hakuna dispute kwa ushahidi wa utetezi na mashitaka.

Waheshimiwa, kuhusu kusambaza, hapa kuna aina mbili za publication.

Kusambaza hii nia.

Kwanza, maneno haya yalisambazwa moja kwa moja kwa watu waliokuwepo kwenye mkutano, akiwemo PW17.

Ambaye yeye katika ukurasa wa 491 anasema alimsikia mshtakiwa akisema, “Tutazuia uchaguzi na tutakinukisha.”

Ilikuwa communicated kwa huyu shahidi.

Ni ushahidi wa utetezi unaoibeba Jamhuri kupitia DW2.

The same na DW3, DW4 na DW5, ambao huu ushahidi ni the best evidence.

Mahakama inapata jibu kwamba hii nia haikubaki kichwani kwake.

Waheshimiwa, take note kwamba shahidi anayesifiwa kuwa ni mkweli ni PW17, ambaye alikuwepo na alisikia.

Niombe Mahakama imuamini PW17 kama ambavyo mshtakiwa anamuamini.

Kwa hiyo, Waheshimiwa, publication na communication, haya maneno yalikuwa tayari moja kwa moja kwa watu waliokuwa katika mkutano.

Maneno haya pia yalisambazwa na social media, kama ambavyo mashahidi wamekuwa wakieleza, P3, P5 na P8.

Waheshimiwa Majaji, maneno haya ambayo yanatuhumiwa kusambazwa na social media ya YouTube kupitia Jambo TV...

Ushahidi huu umeungwa mkono na mashahidi wote.

Na cha kuongeza, PW17 ameiambia Mahakama kwamba ni yeye ambaye amekuwa akirusha kwa kufanya livestreaming.

Waheshimiwa Majaji, kumekuwa na hoja wakati wa utetezi:

“Who exactly published?”

Ikatengenezwa hoja kwamba PW17 ndiye aliyesambaza na ikatengenezwa hoja kwamba si mshtakiwa aliyeitisha kikao na siyo mshtakiwa aliyewaalika waandishi wa habari.

Waheshimiwa, ukisoma ushahidi wa PW17 katika ukurasa wa 497, shahidi huyo anasema, “We live streamed through you.”

Swala la kwamba si mimi niliyeitisha mkutano is immaterial. Swala la msingi ni: alisambaza au hakusambaza?

Aliandaliwa speech au la?

Waheshimiwa Majaji, ni ushahidi wa ukurasa wa 590, mshtakiwa akijitetea anasema tarehe 23 Aprili 2025, “Tulifanya mkutano,” halafu anaenda mbele anasema, “Mkutano siyo mimi na mkutano mimi ni msemaji mkuu.”
 
Nassoro Katuga kaamua kuwa mfasiri wa kamusi za TUKI Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili UDSM na ile ya Oxford Dictionary badala ya kujikita kujenga hoja ya ushawishi kisheria
View attachment 3680372
Uhaini wa kutafuta maana kwenye Kamusi badala ya kutuletea ushahidi mikakati wa kabambe iliyopangwa ili kufanikisha huo uhaini, ni kichekesho kwa wapenda haki.
 
SEHEMU YA 12.

Waheshimiwa Majaji, naomba nihitimishe kwamba tumethibitisha intention.

Hakuna dispute kwamba mshtakiwa alitamka maneno haya.

Hoja iliyobakia hapa ni je, mshtakiwa alisambaza au alichapisha?

Waheshimiwa Majaji, ukiangalia ushahidi, manifestation yake ilifanyika by deed.

Waheshimiwa Majaji, mashitaka yetu ni kwa kutoa na kusambaza, kuyafanya yawe hadharani.

Kutoa maneno hakuna dispute kwa ushahidi wa utetezi na mashitaka.

Waheshimiwa, kuhusu kusambaza, hapa kuna aina mbili za publication.

Kusambaza hii nia.

Kwanza, maneno haya yalisambazwa moja kwa moja kwa watu waliokuwepo kwenye mkutano, akiwemo PW17.

Ambaye yeye katika ukurasa wa 491 anasema alimsikia mshtakiwa akisema, “Tutazuia uchaguzi na tutakinukisha.”

Ilikuwa communicated kwa huyu shahidi.

Ni ushahidi wa utetezi unaoibeba Jamhuri kupitia DW2.

The same na DW3, DW4 na DW5, ambao huu ushahidi ni the best evidence.

Mahakama inapata jibu kwamba hii nia haikubaki kichwani kwake.

Waheshimiwa, take note kwamba shahidi anayesifiwa kuwa ni mkweli ni PW17, ambaye alikuwepo na alisikia.

Niombe Mahakama imuamini PW17 kama ambavyo mshtakiwa anamuamini.

Kwa hiyo, Waheshimiwa, publication na communication, haya maneno yalikuwa tayari moja kwa moja kwa watu waliokuwa katika mkutano.

Maneno haya pia yalisambazwa na social media, kama ambavyo mashahidi wamekuwa wakieleza, P3, P5 na P8.

Waheshimiwa Majaji, maneno haya ambayo yanatuhumiwa kusambazwa na social media ya YouTube kupitia Jambo TV...

Ushahidi huu umeungwa mkono na mashahidi wote.

Na cha kuongeza, PW17 ameiambia Mahakama kwamba ni yeye ambaye amekuwa akirusha kwa kufanya livestreaming.

Waheshimiwa Majaji, kumekuwa na hoja wakati wa utetezi:

“Who exactly published?”

Ikatengenezwa hoja kwamba PW17 ndiye aliyesambaza na ikatengenezwa hoja kwamba si mshtakiwa aliyeitisha kikao na siyo mshtakiwa aliyewaalika waandishi wa habari.

Waheshimiwa, ukisoma ushahidi wa PW17 katika ukurasa wa 497, shahidi huyo anasema, “We live streamed through you.”

Swala la kwamba si mimi niliyeitisha mkutano is immaterial. Swala la msingi ni: alisambaza au hakusambaza?

Aliandaliwa speech au la?

Waheshimiwa Majaji, ni ushahidi wa ukurasa wa 590, mshtakiwa akijitetea anasema tarehe 23 Aprili 2025, “Tulifanya mkutano,” halafu anaenda mbele anasema, “Mkutano siyo mimi na mkutano mimi ni msemaji mkuu.”
Katuga anapiga kwenye mshono
 
Wakati kesi inaanza mliponda hivi hivi mwisho wa siku mwamba akakutwa na kesi ya kujibu ....ukimsoma Katuga kiufipa kweli utasema anapuyanga lakini ukimsoma kisheria anatumia vifungu kumjibu Lisu kuhusu hati ya mashitaka
Majaji walisema wamemkuta na Kesi ya kujibu bila kujali uzito wa hoja
 
..mauaji hayana faida kwa upande wowote.

..Mama amechafuka kwa damu za wasio na hatia kwa kufuata mtizamo kama huo ulionao.
mama anaendelea na shughuli zake, magu na kikwete mlivyowachafua waliua? wangekuwa na adabu wasingechoma vituo vya mafuta, mabasi, nyumba, ofisi wangeuliwa?
 
SEHEMU YA 13.

Waheshimiwa Majaji, yeye ni mmoja ya waliofanya mkutano na huku akijua anaongea mbele ya waandishi wa habari.

Waheshimiwa Majaji, katika ukurasa wa 628, mshtakiwa anaendelea mbele anasema:

“Pale ambapo tunataka mambo yetu yawafikie umma huwa tunawaalika waandishi wa habari, na pale ambapo hatutaki iwafikie umma tunawataka waandishi wa habari watoke.”

Huu ushahidi unaunga mkono ushahidi wa PW17, ambaye anasema pale walipotaka mambo mengine yasiende public, waliwatoa waandishi wa habari.

Swali ni: Je, nani alitangaza mkutano?

Mkutano ulikuwa live streamed.

Waheshimiwa Majaji, utagundua tunatafsiri sheria kiupande upande.

Waheshimiwa Majaji, kwa ushahidi huu ni wazi mshtakiwa alisambaza nia yake kwa umma ya kutishia Serikali.

Hoja ya kusambaza tunasema imethibitishwa pasipo kuacha shaka.

DW3 anasema mshtakiwa alitaka speech yake iwafikie umma kupitia waandishi wa habari.

Ushahidi wa utetezi ndiyo the best evidence.

Mshtakiwa alitaka habari iwafikie umma.

Waweze kuchocheka, wakachocheka, wakapanga uasi, tukawakamata baadaye tukawaleta mahakamani.

Hata hao mashahidi anaosema waliona video, hiyo video ipo wapi?

Waheshimiwa Majaji, kwa mujibu wa Kifungu cha 3 cha Sheria ya Ushahidi...

Kwanza niweke hivi kwamba video ni moja ya electronic evidence.

Na hii ni kwa mujibu wa sheria, na kwa mujibu wa sheria ni document.

Na hii, Waheshimiwa Majaji, ni kwa mujibu wa Kifungu cha 3, CAP 6, cha Sheria ya Ushahidi, ambacho kinatamka kwamba electronic evidence ni document.

Ikimaanisha kuna oral testimony na kuna real evidence; hizi zinategemea na nature of the case.

Documentary evidence haiwezi kuwa kubwa kuliko oral testimony.

The absence of video recording, Waheshimiwa Majaji, haimaanishi kwamba ukweli kwamba video ile ilisambazwa kupitia video uliwawezesha mashahidi wa Jamhuri kuisikia na kuiona.
 
Back
Top Bottom