Mahakamani 29 Septemba 2026: Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

Mahakamani 29 Septemba 2026: Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

Hatukumbatii ukatuga sisi. Upumbavu wenu masisiemu bakini nao huko huko shimoni
“Pale ambapo tunataka mambo yetu yawafikie umma huwa tunawaalika waandishi wa habari, na pale ambapo hatutaki iwafikie umma tunawataka waandishi wa habari watoke.” Lissu. Huyu safari hii ameyakanyaga alizoea kuwasumbua kikwete na magu
 
Uhaini wa kutafuta maana kwenye Kamusi badala ya kutuletea ushahidi mikakati wa kabambe iliyopangwa ili kufanikisha huo uhaini, ni kichekesho kwa wapenda haki.

Nassoro Katuga kaamua kuwa mfasiri wa kamusi za TUKI Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili UDSM na ile ya Oxford Dictionary badala ya kujikita kujenga hoja ya ushawishi kisheria
1790689876554.png


Nassoro Katuga kaja na toleo la 2026 la msamiati wa maneno kwa kutumia kamusi yao maalum ya lugha ya kiswahili iliyoandaliwa mtaa wa Lumumba Ofisi ndogo ya CCM wanaipeleka Mahakama Kuu ya Tanzania

Serikali ya CCM inahagaika sana kujisafisha inakumbusha kazi ya mtunzi wa riwaya George Orwell na kitabu chake maarufu duniani kiendacho kwa jina 1984 ambapo kuna wizara ya ukweli.

Ni nini kinashangaza kuhusu jina la Wizara ya Ukweli? (ya CCM) itakayowaleta waziri Paul Christian Makonda, mkuu wa oganizesheni CCM Paul Chacha na mkurugenzi wa mashtaka DPP na kwenu wananchi kuzungumzia HAKI katika mfumo wa mahakama

Wizara kubwa na muhimu kupita zote ni Wizara ya Ukweli. Hapa ndipo Winston (kinara waziri Wassira) anafanya kazi. Kinachoshangaza ni kwamba, Wizara ya Ukweli imejikita katika kuunda uwongo. Wafanyikazi katika idara ya Winston hutumia siku yao kubadilisha rekodi za kihistoria ili ziakisi chochote kinachotokea wakati huo .


Je, kazi ya Winston kada wa chama katika nukuu ya Wizara ya Ukweli ni ipi?
Winston anaenda kufanya kazi katika idara ya kumbukumbu ya Wizara ya Ukweli. Anakaa kwenye meza yake, akiangalia maandishi yake, mashine ambayo huandika kile anachozungumza ndani yake. Kazi yake ni kusasisha taarifa zozote za maandishi ambazo zimethibitishwa kuwa si sahihi au zenye madhara kwa Chama - George Orwell 1984



Je, Wizara ya Ukweli inatumia msemo gani? Wizara ya Ukweli ina kauli mbiu tatu: "Vita ni Amani," "Uhuru ni Utumwa," na "Ujinga ni Nguvu." Mistari hii mitatu imeandikwa nje ya jengo ya Ofisi Ndogo ya Chama mtaa wa Lumumba . - George Orwell


George Orwell :

Je, ni nukuu gani kuhusu ukweli na uongo George Orwell 1984?
"Na ikiwa wengine wote walikubali uwongo ambao Chama kiliweka - ikiwa rekodi zote zilisema hadithi moja - basi uwongo huo ulipitishwa katika historia na kuwa ukweli. 'Ni nani anayedhibiti yaliyopita' aliendesha kauli mbiu ya Chama, 'anadhibiti siku zijazo: ni nani anayedhibiti sasa anadhibiti yaliyopita. '” - George Orwell

'The Ministry of Truth: A Biography of George Orwell's "1984"
 
Leo ni siku ambayo kesi ya Lissu inaendelea mahakamani. Tunaomba Manyanza utuletee hiyo Update.

MAHAKAMA IMEANZA MAWAKILI WA SERIKALI WANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO.

SEHEMU YA 1.

Jumanne, Septemba 29, 2026

Lissu ameingia kwa kushangiliwa sana.

Majaji nao wameingia.

Mawakili wa Serikali wawili leo siwaoni. Hayupo Ajuaye Zegeli na Job Mrema.

Karani wa Mahakama anajiandaa kusoma kesi: Criminal Session, Kesi Na. 19605 ya 2025, Jamhuri dhidi ya Tundu Antipas Lissu.

Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga, anasimama.

Nassoro Katuga:
“Waheshimiwa Majaji wa Mahakama hii Tukufu, iw apendeze, naitwa Nassoro Katuga, nipo pamoja na:

1. Ignasi Mwinuka, Wakili wa Serikali Mkuu;
2. Tawabu Issa, Wakili Mwandamizi;
3. Cuthbert Mbilinyi, Wakili wa Serikali;
4. Winiwa Kasara, Wakili wa Serikali.

Sisi kwa pamoja tunaiwakilisha Jamhuri.

Mshtakiwa yupo mbele yenu.

Waheshimiwa Majaji, shauri leo limekuja kwa ajili ya kuleta mawasilisho, specific kwa upande wa Jamhuri kuleta mawasilisho.

Upande wa Jamhuri tupo tayari.”

Jaji Ndunguru:
“Mshtakiwa?”

Lissu:
“Waheshimiwa Majaji, nipo tayari.”

Jaji:
“Tuendelee upande wa Mashitaka.”

Nassoro Katuga:
“Naomba kutoa ahadi, Waheshimiwa Majaji, kwamba tutakuwa na mawasiliano ambayo si marefu.

Tuta-focus na shauri lililopo mbele yetu.

Waheshimiwa Majaji, nitaanza tu submission. Naitwa Nassoro Katuga.

Waheshimiwa Majaji, mshtakiwa ameshtakiwa kwa kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, Urekebu wa Mwaka 2022.

Ambapo, Waheshimiwa Majaji, kuhusiana na taarifa ya shitaka hili, inaelezwa kwamba tarehe 23 Aprili 2025, ndani ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa chini ya utii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alitengeneza nia ya kuchochea umma kuweza kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, kwa nia ya kuitisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (for the purpose of intimidating the Executive), kwa kudhihirisha nia hiyo kwa kutoa maneno yafuatayo:

‘Wanasema kitu kimoja sahihi hapa, wanasema hivi: Msimamo huu unaashiria uasi, ni kweli, ni kweli kwa sababu tutazuia uchaguzi, hiyo ndiyo namna ya kupata mabadiliko. Kwa hiyo tunaenda kukinukisha, huu uchaguzi tutauvuruga, tutauvuruga kwa sababu tunaenda kukinukisha vibaya sana.’

Haya maneno ndiyo Jamhuri imeleta mbele yenu, mbele ya sheria kuyaangalia.

Kwamba maneno haya ndiyo, Waheshimiwa Majaji, tunatuhumu au kutafsiri in favour of the Republic.

Kwamba mshtakiwa alitoa maneno haya kwa nia ya kuitisha Serikali ili apate mabadiliko, ambayo aliyetafsiri ni ‘mabadiliko’.

Waheshimiwa Majaji, kifungu ambacho nimekirejea cha 39(2), upande wa Jamhuri tulikifanyia research kama Mahakama ilishawahi kuki-test.

Tafiti zilionyesha kwamba Mahakama zetu katika mashauri ya uhaini ni mashauri ambayo yalishitakiwa chini ya kifungu cha 39(a).

Waheshimiwa Majaji, samahani, kama itawapendeza, naomba nimuingize Job Mrema katika kolamu ya upande wa Jamhuri. Alikuwa amepata dharura, sasa amefika.

Waheshimiwa Majaji, kwa kuwa tumejiridhisha kwamba haijawahi kutumika katika Mahakama zetu, tuweze sasa kutafsiri hati ya mashitaka pamoja na kifungu kilichotumika cha 39.

Ili kuweza kuona ni vitu gani Mahakama yenu Tukufu ilianza kuangalia ushahidi, basi ni kitu gani upande wa Jamhuri ulipaswa kuthibitisha.

Naomba kwa kuanza kuwaalika katika kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu.

Kifungu chenyewe kinasema:

‘Mtu yeyote ambaye yupo chini ya utii, awe Tanzania au nje ya Tanzania, atengeneze nia either kufanyika au kusababisha kufanyika au kutengeneza nia ya kuchochea.’

Kwa mujibu wa kifungu cha 135 cha CPA, Sura ya 20, Urekebu wa Mwaka 2023, kinaelezea kwamba mashitaka lazima yawe na maelezo ya kosa la shitaka husika pamoja na maelezo ya shitaka.

Ambayo sheria inasema hayo maelezo lazima yatie information ya jinsi shitaka lilivyofanyika.

Lakini kifungu cha 138(a)(iii) kinaelekeza kwamba technical terms hazitakiwi kutumika.

Inatakiwa itumike ordinary language, lugha ya kawaida.

Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, mtaona kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d), kinaelekeza kwamba ili mtu ashitakiwe kwa kosa la uhaini la aina hii:

Kwanza ni lazima awe mtu mwenye utii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwetu ilichukua mshtakiwa ni mtu wa Jamhuri ya Tanzania akiwa Tanzania, tukaacha ‘elsewhere’.

Hati yetu ya mashitaka ikachukua ‘forms an intention to instigate’ — nia ya kuchochea.

Tukaachana na maneno ‘forms’ zingine za ‘intention to defect’.

Ikaachana na ‘intention to persuade’, ‘to counsel’, ‘to...’

‘Intention to instigate the public’ — umma kwa ujumla wake, nitaeleza hapa kwa nini.

Hati ya mashitaka ikaeleza watu wamechochewa kufanya nini.

Mshtakiwa akichochea umma kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 — General Election, Waheshimiwa.

Waheshimiwa Majaji, hati yetu ya mashitaka imeachana na neno ‘deed’, ikachukua neno ‘for the purpose of intimidating the Executive’.

Na hapa ikaachana na maneno ‘intimidating Legislature’ na ikachukua ‘intimidating the Executive’.

Ukiendelea na hati ya mashitaka, ile nia ya mshtakiwa kudhihirisha nia yake...

Hati ya mashitaka ikaachana na maneno ‘manifestation ya hiyo nia by publication by overt act’, ikaachwa.

Lakini ikachukuliwa ‘manifestation by his deed’ — alidhihirisha nia kwa kitendo chake.

Kitendo gani, Waheshimiwa?

Kutoa maneno ambayo nimeshayatoa, Waheshimiwa.

Waheshimiwa Majaji, sehemu zote ambazo nilikuwa naiambia Mahakama Tukufu kwamba hati ya mashitaka imeacha haya, imechukua haya.

Imeacha ‘manifestation by publication’, ikachukua ‘manifestation by deed’ kwa mujibu wa kifungu cha 39.

Neno lililotumika ni ‘or’.

Kwa tafsiri nyepesi, pale ambapo inatumika ‘or’, hayo maneno siyo similar.

Kwa maana nyingine, yanatumika disjunctively; huwezi kuyachukua yote kama kiroba ukapachika katika hati ya mashitaka.

Inamaanisha ulichukua yote hayo ukayaweka, hiyo act inakuwa defective.

Ili maneno haya kuwa sawa, kama kuna ‘or’, lazima kuna maneno yaongezwe kuyafanya yawe similar, mfano neno ‘similar’ lenyewe au maneno mengine yanayoonyesha similarity.

Unless ilitumika ‘or’, kuna sheria inatumika kutaka yaongezwe.

Ukiyaweka yote, hiyo hati ya mashitaka inakuwa defective.

Waheshimiwa Majaji, haya tunayozungumza siyo maneno yetu.

Pale ambapo ‘or’ inatumika, siyo maneno yetu bali maneno ya Bungeni na kutungwa sheria.

Sheria ya Tafsiri ya Sheria, Sura ya Kwanza, na Urekebu wa 2023, kifungu cha 13.

Kwa ridhaa yenu, kifungu kinasomeka hivi...

Haya ndiyo maneno ambayo nimeyakopa katika submission.

Ndiyo maana hati yetu ya mashitaka iliruka baadhi ya maneno ili kufanya hati yetu isiwe defective na iwe yenye kueleweka.

Hati ya mashitaka ni nyaraka muhimu inayomfahamisha mshtakiwa mashitaka anayoshitakiwa nayo na kumweka sasa katika position ya kujitetea.”

SEHEMU YA 2

Nassoro Katuga anaendelea:

“Waheshimiwa Majaji, kifungu cha 39(2)(d) kimeanza kwa neno ‘any person who, being under...’

Waheshimiwa Majaji, hili neno ‘any person’ halijam-exclude mtu yeyote, unless ana immunity kisheria.

Mtu mwingine anaweza kusema yeye ana cheo fulani au ni kiongozi wa chama cha siasa.

Kifungu hicho hakijachagua huyo ‘any person’ anatokea wapi.

Ndiyo maana kwanza tumeanza kuchambua.

Waheshimiwa Majaji, narudi kwenye kifungu cha 39(2)(d), kinasema mtu yeyote akichochea, lakini hati yetu imetumia neno ‘public’.

Kuna neno ‘any person’, lakini Jamhuri imetumia neno ‘public’.

Waheshimiwa Majaji, hati ya mashitaka kwa upande wa Jamhuri imetumia neno ‘public’ kuweka clarity, kufanya hati ya mashitaka ieleweke kuendana na ushahidi wa upande wa Jamhuri ulioutoa.

Hii inafanyika kuendana na kifungu cha 135 cha CPA.

Waheshimiwa Majaji, tumetumia neno ‘to instigate the public’ kuendana na kifungu cha 135, kufanya hati ya mashitaka kueleweka kuendana na ushahidi wa upande wa Jamhuri ulioutoa.

Waheshimiwa Majaji, kama tulivyoeleza awali, kifungu cha 135 kinataka maelezo ya kosa yaeleweke katika kiwango ambacho mshtakiwa aweze kujitetea na in conformity na ushahidi uliotolewa.

Waheshimiwa Majaji, neno ‘any person’ linafanana na neno ‘public’.

Waheshimiwa, ‘any person’ na ‘a group of people’ yamekuwa included kwenye ‘public’.

Yametafsiriwa katika kifungu cha 5 cha Kanuni ya Adhabu, Waheshimiwa.

Siyo tu akimaanisha watu wote wa Tanzania Bara, lakini hata yule mkazi au anayetumia eneo fulani na any number of those people.

Kwa hiyo, ‘public’ inazungumzia watu.

Na Waheshimiwa Majaji, katika kuandaa taarifa za mashitaka, kama ‘any person’ refers to a person, you have to mention.

Kama unataka ku-refer maneno yako yaende kwa ‘any person’, lazima utaje huyo person.

Na kama hati yako itarefer ‘group of people’, lazima utaje hilo group.

So, neno ambalo linajumuisha kama alikuwa amechochea mtu mmoja au kikundi fulani, neno sahihi kutumia ni ‘public’.

Na hii, Waheshimiwa Majaji, ni kwa mujibu wa kifungu cha 5.

Waheshimiwa Majaji, kwa ushahidi wa Jamhuri ulivyokuwa, Jamhuri inamtuhumu kuchochea umma.

Mshtakiwa wakati anachochea hakulenga kikundi fulani na hakumlenga mtu fulani ambaye sasa upande wa Jamhuri amtaje, na hakumlenga.

Ndiyo inakuja sasa tafsiri ambayo ni whether a person or a group of people.

Waheshimiwa Majaji, hakuna namba kamili inayoweza kutoa tafsiri ya ‘a group of people’.

Kwa hiyo, umma utakuwa ni ‘a group of people’.

Na hii sasa tunaipata kwenye tafsiri ya hilo neno lilivyotumika.

Waheshimiwa Majaji, tukirudi kwenye swala zima la kudhihirisha (manifestation) kwa mujibu wa kifungu cha 39:

Nia ya kutenda uhaini inadhihirishwa vipi?

Kwa mujibu wa kifungu hiki, manifestation inaweza kusababishwa kwa kusambaza maandishi au michoro.”
Kwenye dunia iliyostaarabika mwanasheria akileta na kukomaa na kesi isiyokuwa na kichwa wala miguu mahakamani anaweza kuwa sanctioned.
 
Sitaki Lisu ahukumiwe kwa sababu ile ilikuwa siasa. Sasa usiniparamie kihivyo!
Nikuelimishe kidogo kwa faida ya wengi. Jibu la hii kitu imejificha kwenye ''nia'' wakati nafanya jambo, nia ya hili jambo ni nini? Hapo kwenye jibu ndio penye uzito[points]
Nikupe mfano mwingine nje ya kesi inayofuatiliwa.
Kubaka ni kosa. Na tuchukuliee kumtisha mtu ni kosa. Nikisema, ''nitakubaka cocastc kavukavu''
Hapa ikithibitika ulitishika basi nitakuwa nimetenda kosa la kukutisha, ila sio kosa la kubaka (halijatendeka) ambalo kitendo chake ni kukula uloda upende usipende. Mfano huu wa viwanja vile utakuwa umeelewa somo.
Ndo sasa Jamhuri imeshindwa kuthibitisha kwasababu waliotakiwa kuthibitisha imekataa wasije mahakamani ...walijipiga risasi wenyewe. Jambo lolote kabla kuhukumiwa lazima lithibitishwe ndo mtu apewe hukumu leo hii unaweza ukaua mchana kweupeee lakini kama haijathibitishwa utaachwa hapo ndo ugumu wa kuendesha kesi na upelelezi unapokuepo ndo maana kuna watu wanajulikana ni washenzi lakini sheria imeshindwa kuwatia hatiani kwasababu haijathibitishwa.
 
Katuga anacho kizungumza hata hakimake sense, ni hoja za uongo, blah blah na zisizo na mashiko anazileta hapa. Upuuzi mtupu.
kama uongo na blaa blaa itawasaidia lissu kuachiwa huru.
 
Nassoro Katuga kaamua kuwa mfasiri wa kamusi za TUKI Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili UDSM na ile ya Oxford Dictionary badala ya kujikita kujenga hoja ya ushawishi kisheria
View attachment 3680415

Nassoro Katuga kaja na toleo la 2026 la msamiati wa maneno kwa kutumia kamusi yao maalum ya lugha ya kiswahili iliyoandaliwa mtaa wa Lumumba Ofisi ndogo ya CCM wanaipeleka Mahakama Kuu ya Tanzania

Serikali ya CCM inahagaika sana kujisafisha inakumbusha kazi ya mtunzi wa riwaya George Orwell na kitabu chake maarufu duniani kiendacho kwa jina 1984 ambapo kuna wizara ya ukweli.

Ni nini kinashangaza kuhusu jina la Wizara ya Ukweli? (ya CCM) itakayowaleta waziri Paul Christian Makonda, mkuu wa oganizesheni CCM Paul Chacha na mkurugenzi wa mashtaka DPP na kwenu wananchi kuzungumzia HAKI katika mfumo wa mahakama

Wizara kubwa na muhimu kupita zote ni Wizara ya Ukweli. Hapa ndipo Winston (kinara waziri Wassira) anafanya kazi. Kinachoshangaza ni kwamba, Wizara ya Ukweli imejikita katika kuunda uwongo. Wafanyikazi katika idara ya Winston hutumia siku yao kubadilisha rekodi za kihistoria ili ziakisi chochote kinachotokea wakati huo .


Je, kazi ya Winston kada wa chama katika nukuu ya Wizara ya Ukweli ni ipi?
Winston anaenda kufanya kazi katika idara ya kumbukumbu ya Wizara ya Ukweli. Anakaa kwenye meza yake, akiangalia maandishi yake, mashine ambayo huandika kile anachozungumza ndani yake. Kazi yake ni kusasisha taarifa zozote za maandishi ambazo zimethibitishwa kuwa si sahihi au zenye madhara kwa Chama - George Orwell 1984



Je, Wizara ya Ukweli inatumia msemo gani? Wizara ya Ukweli ina kauli mbiu tatu: "Vita ni Amani," "Uhuru ni Utumwa," na "Ujinga ni Nguvu." Mistari hii mitatu imeandikwa nje ya jengo ya Ofisi Ndogo ya Chama mtaa wa Lumumba . - George Orwell


George Orwell :

Je, ni nukuu gani kuhusu ukweli na uongo George Orwell 1984?
"Na ikiwa wengine wote walikubali uwongo ambao Chama kiliweka - ikiwa rekodi zote zilisema hadithi moja - basi uwongo huo ulipitishwa katika historia na kuwa ukweli. 'Ni nani anayedhibiti yaliyopita' aliendesha kauli mbiu ya Chama, 'anadhibiti siku zijazo: ni nani anayedhibiti sasa anadhibiti yaliyopita. '” - George Orwell
Na hilo bichwa lake km Boga la kiangazi au cabbage iliyokomaa.
Baba hovyo hili, mxxxiiieeew
 
SEHEMU YA 14.

Hawawezi kuthibitisha hoja kwamba walisikia maneno yale ya hicho kipande cha video.

Haimaanishi kwamba kutokuwepo kwa video basi mashahidi hao hawaaminiki.

Waheshimiwa Majaji, kila shahidi ana haki ya kuaminiwa.

Maneno ya kwamba kila shahidi anastahili kuaminiwa yamesemwa sana katika kesi ya Goodluck Kiando.

Maneno ambayo mshtakiwa hakatai.

Mahakama hii Tukufu iwe na reasons ya kuchukua ushahidi huu.

Imeelezwa kwenye kesi ya mtu anaitwa Abbas Kondo Gede vs Jamhuri, Criminal Appeal No. 472 of 2017, iliyoripotiwa TanzLII tarehe 10 Agosti 2020.

Katika ukurasa wa 21 wa shauri hili, Waheshimiwa, kulikuwa na maneno haya.

Mahakama ya Rufani ilikuwa na haya ya kusema kwamba:

“The access of video” haimaanishi kwamba kuna usambazaji wa hayo maneno kwenye video.

Video ya nini kama mashahidi 15, wakiwemo wa utetezi, wanaunga mkono ushahidi wa Jamhuri?

Ushahidi wa Jamhuri umeungwa mkono bila hata kutoa ushahidi wa video.

Ni hoja yetu kwamba manifestation imethibitishwa bila kutoa video, ikiwemo na mashahidi wa upande wa utetezi na mshtakiwa mwenyewe.

Waheshimiwa, tunajua ni jukumu letu kuthibitisha shitaka pasipo kuacha shaka.

Katika wasilisho letu tumewarejesha katika ushahidi ambao umebeba hoja.

Lakini pia ni busara kwa upande wa Jamhuri ku-consider utetezi wa mshtakiwa.

Lakini kwa harakaharaka, utetezi wa mshtakiwa umeshindwa kabisa ku-raise doubt.

Umebaki kuwa intact.

Lakini katika kujaribu kuweka matundu katika prosecution case, upande wa utetezi umejaribu kuonyesha kwamba katika ushahidi wa mashahidi palikuwa na mapungufu.

Waheshimiwa Majaji, mapungufu ambayo yalikuwa yanajaribiwa kuonyeshwa na upande wa utetezi ni mapungufu ambayo hayana madhara.

Waheshimiwa Majaji, minor contradictions ni vitu ambavyo haviepukiki wakati wa trial, kwa sababu kila shahidi anatoa ushahidi kwa jinsi alivyoona, kusikia au perceive.

Waheshimiwa Majaji, minor contradictions and discrepancies zinaithibitishia Mahakama kwamba, kwa msimamo wa kisheria, hawa mashahidi si mashahidi ambao wamekuwa coached kutoa ushahidi.

Kulingana na nature ya ushahidi wao.

Waheshimiwa, ni msimamo wa kisheria kwamba contradiction ambayo haiendi to the root haina madhara.
 
Waheshimiwa Majaji, minor contradictions and discrepancies zinaithibitishia Mahakama kwamba, kwa msimamo wa kisheria, hawa mashahidi si mashahidi ambao wamekuwa coached kutoa ushahidi. Katuga.

Kwani kama ushahidi una "Contradictions and discrepancies (minor?) anataka mahakama iamue vipi?
 
mama anaendelea na shughuli zake, magu na kikwete mlivyowachafua waliua? wangekuwa na adabu wasingechoma vituo vya mafuta, mabasi, nyumba, ofisi wangeuliwa?

..Na waliouwawa kabla ya hapo walikosea nini?

..Magu na JK walihusika na mauaji walipokuwa madarakani.

..Ccm uwezo wa kushinda uchaguzi bila kutumia mabavu mnao, tatizo hamjiamini.

..Watupeni mkono wauwaji ktk chama chenu.
 
..Na waliouwawa kabla ya hapo walikosea nini?

..Magu na JK walihusika na mauaji walipokuwa madarakani.

..Ccm uwezo wa kushinda uchaguzi bila kutumia mabavu mnao, tatizo hamjiamini.

..Watupeni mkono wauwaji ktk chama chenu.
wakati wa magu na jk nani alichoma mabasi, stendi, nyumba nk?

kwahiyo serikali iliamua kuua bila sababu?
 
Back
Top Bottom