Mahakamani 29 Septemba 2026: Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

SEHEMU YA 16.

Nassoro Katuga:

Waheshimiwa Majaji, hoja nyingine ilikuwa kwamba hawa Mashahidi ambao ni Police Officers na wale Mashahidi ambao walichocheka, P5, P6, P7 na P9, ni Mashahidi ambao wana maslahi.

Ni Mashahidi ambao mara ya kwanza walikamatwa kama Watuhumiwa na baadaye wakageuzwa kuwa Mashahidi.

Waheshimiwa Majaji, tukianza na Mashahidi ambao walikuwa washitakiwa na baadaye wakaja kuwa Mashahidi, Kifungu cha 151 cha Sheria ya Ushahidi, Sura ya 6 na marekebisho ya 2023, kinasema kwamba kama washitakiwa walikuwa wamechocheka na kufanya vurugu ya uchaguzi, ni washitakiwa wenza.

Walikuwa na maslahi katika kesi hii baada ya kufutiwa kesi zao.

Kwa mujibu wa kifungu hiki, Waheshimiwa Majaji, hawa wapo competent na wapo sawa kutoa ushahidi.

Waheshimiwa, principle ya ushahidi wenye maslahi inataka kuonyesha kwamba shahidi huyu, kwa kuwa ana maslahi, anaiongopea Mahakama?

Hoja ya msingi: waliona video, hawakuiona? Walichocheka au hawakuchocheka?

Waheshimiwa, maneno haya yapo katika kesi ya Basildi John Mlayi Vs Jamhuri, Criminal Appeal Number 306 ya mwaka 2008, imepandishwa TanzLII October 2022, Waheshimiwa.

Katika ukurasa wa 25, Mahakama ya Rufani ilisema, “the concept of witness...”

Waheshimiwa, kikubwa hapa, you have to prove they have lied.

Haiishii tu kulalamika kwamba wana maslahi.

Tunamalizia kauli yetu: “This court is not yours, Mother.”

Waheshimiwa Majaji, naomba nimalizie hoja ya mwisho kabisa.

Hoja ya mwisho ilikuwa ni malalamiko kuhusiana na maelezo yaliyopo katika Police Statement dhidi ya yaliyopo Mahakamani.

Maelezo haya yakitolewa chini ya Kifungu cha 163 cha Sheria ya Ushahidi.

Lakini kilichofanyika kwa kiasi kikubwa ni kuonyesha omission, hata pale ambapo kulikuwa na contradiction, ilikuwa ni minor.

Kwa mfano, kwenye statement uliweka dini yako ni Muislamu, halafu hapa unasema Mkristo. Hilo ni jambo dogo.
 
Mo29 haihusiki hapa, Lisu alikuwa ndani. vinginevyo thibitisha mana wakuu wa usalama walikula kona.
 
wakati wa magu na jk nani alichoma mabasi, stendi, nyumba nk?

kwahiyo serikali iliamua kuua bila sababu?

..JK na Jpm waliuwa ili kuwatisha na kuwadhoofisha wapinzani na wanaharakati.

..Mama alianza vizuri na 4R lakini baadae akakumbatia mbinu chafu za watangulizi wake.

..Mauaji ya OCT 29 ni matokeo ya vyombo vyetu kufundishwa, na kuzoeshwa, kuwa wakatili kwa raia wa kawaida, na sio jambo lililotokea kwa ghafla.
 
Katuga banah. Hivi unaweza kupima kuchocheka kwa mtu kama hajatenda? Huyu jamaa ningekuwa huko mahakamani angechezea ngumi za kutosha mbele ya hao majaji wake. Alipeleka upuuzi mtupu mahakamani.

Yani unawezaje wewe Katuga ku prove kwamba mimi nina ugwadu wakati sijaku......a ukajionea?
 
Huyu mpumbavu Katuga aache ujinga wake, mtu anadanganya wazi dini yake ndio jambo dogo? Kwa case km hii? Halafu anasema makosa yote yalikua ni madogo madogo, akumbuke dini iko ndani ya kiapo na aliapa nayo km shahidi.

Hiyo submissions yake ya ku unga unga na kuokoteza vijifungu uchwara ambavyo havipo ni ukiritimba wa wazi kabisa mbele ya mahakama, leo kazi yake kutafsiri maneno kwenye kamusi tu, hakuna cha maana alichokisema kuhusiana na case, na kashindwa kuthibitisha kosa la uhaini.
Mpuuzi huyu na hilo bichwa lake, khaaah
 
Halafu huyo "katuga" mbona hamalizi hiyo submission wakati alisema atachukua muda mfupi au ameenda kusikiliza maoni kutoka CCM?
Lissu aliongea kwa siku NNE mfululizo Asubh na mchana.
 
Badala ya kufanya submision anatoa tafsiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…