cocastic
JF-Expert Member
- Nov 30, 2019
- 123,324
- 202,767
Hatimaye heka heka za vizimba vya mahakama kwa mwaka mzima zimetamatika hii leo.
Kila mtu amesikia na ameona mwenendo mzima wa case toka mwanzo hadi sasa, kila kitu kiko wazi pasi na shaka, kila upande utapata haki na stahiki yake, pasipo upendeleo wowote.
Kwenu majaji, tunategemea usomi na weledi wenu ktk kupitia hii case kwa umakini na usahihi, pasipo kuingiliwa wala kuyumbishwa na yoyote wala chochote, tunategemea kuona hukumu iliyo ya haki na ukweli halisi.
Binafsi yangu, nitoe rai kwenu majaji, hii case imebeba hatma ya mustakabali wa muenendo na maisha ya mtu baada ya hukumu yenu, sio hivyo tu imebeba dhamana ya heshima na hekima kwenu majaji na taasii ya mahakama km muhimili huru na unaojitegemea, km katiba inavyosema wazi.
Hukumu yenu itaakisi kile kilicho/kinacho sikika kwa umma, kuwa mahakama ni ya simu, na ili kukanusha kwa umma kuwa maneno Yale sio sahihi na ilikua bahati mbaya, basi toeni hukumu ya haki na ukweli kulingana mlolongo mzima wa shauri, ushahidi na case nzima kwa ujumla, vinginevyo umma utaamini yale maneno ni ya kweli, itapelekea mahakama kupoteza uaminifu, heshima na hekima mbele ya umma.
Niwatakie kila la kheri ktk jukumu lenu hilo kubwa na nzito ktk kutoa hukumu juu ya case hii.