residentura
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 10,348
- 15,205
Sasa ni rasmi.Katuga pia anataka mahakama ikinusa tu harufu ya kesi basi iwe imeshashiba kwa kula. Maana yake anataka Isiende kwenye kuthibitisha pasipo na shaka maana ikifanya hivi itakuwa inawaachia wakosaji.
Yan kina Yericko Nyerere nitakuwa nawaita makatuga badala ya vilaza. Tumepata msamiati mpya mjini.
Baada ya Lissu jana kuonyesha panapo vuja kwenye hii kesi ya kupikwa.. ndipo katuga leo anajaribu kuziba ziba kwa kuokotezaokoteza maneno..Mpaka sasa sijaona kama kagusa kiini cha kesi yenyewe kisheria.
Inategemea na nia. mfano nikisemaKutamka ni kutenda kweli jamani? Hata kama hatujaenda shule, hapa Katuga katulisha matango pori😅🤣😂
Sio aonekane, ni layman kiuhalisia.Ila katuga hii kesi imemburuza haswa, imemfanya aonekane ni layman wa sheria.
😄😄Sio aonekane, ni layman kiuhalisia.
Katuga ni katuga (kihiyo/kilaza) mkubwa wa sheria.
Aisee...ku- publish"...unaifahamu Berne Convention?SEHEMU YA 4.
Nassoro Katuga anaendelea:
Hata kwenye Penal Code kuna makosa ya neno “utter”.
Neno “utter” ni kitendo.
Kitendo cha kusudio lake nini?
“Utter” ni verb, haiwezi kusimama peke yake katika tafsiri ya sheria; it’s not a noun.
“By his deed of uttering.”
Kwa hiyo, tafsiri rahisi, kutoa maneno ni kitendo cha kutamka maneno.
Ndiyo maana kuna kosa linalotokana na uttering.
Kwa tafsiri ya sheria, uttering ni kitendo.
Waheshimiwa Majaji, tunalichukua hili kwa kuzingatia kwamba mens rea na actus reus ndiyo chanzo cha kosa.
Kifungu cha 89(1)(a) cha sheria, Kanuni ya Adhabu.
Shitaka limekamilika kwa kuzingatia mens rea na actus reus, kwamba kuna kosa la kutoa maneno.
Yapo makosa mengi ambayo ni ya kutoa maneno, hata vitisho.
Kama maneno ni kitendo, basi jibu ni ndiyo.
Hati ya mashitaka inasema pamoja na kutoa maneno, lakini aliyasambaza.
Waheshimiwa Majaji, kifungu cha 39 kimetumia “publication” kwa sehemu mbili.
Waheshimiwa Majaji, tafsiri ya “publish”, according to Oxford Advanced Learner’s Dictionary, inasema:
“Publish is to make known information to the public.”
Synonym, kwamba taarifa fulani ijulikane kwa umma.
Haya ndiyo maneno labda Mahakama hii Tukufu ingependa kujiuliza yalivyotumika katika hati yetu ya mashitaka.
Waheshimiwa Majaji, kwenye hiyo hiyo hati ya mashitaka Mahakama yenu ingependa kuyaona.
Kwa kifupi, yalilenga kuitishia Serikali, ukiangalia kuna kufunga na kufungua semi yalivyotumika.
Jukumu la kuchambua maneno yapi yalitishia Serikali katika maneno laki moja siyo dhumuni la kifungu cha 5.
Tumechagua maneno machache yanayotishia Serikali kati ya maneno mengi.
Waheshimiwa Majaji, swali la kujiuliza: Haya maneno ni sentensi zilizokamilika kuleta maana?
🤣🤣Inshaalah next tym kikinuka Katuga na genge lake tutawaembelea!
Na hawezi kugusa kwa sababu hakuna chochote atakachokigusa na kikaonekana valid ni hatia.Mpaka sasa sijaona kama kagusa kiini cha kesi yenyewe kisheria.
usichanganye mambo hapa, hizo maana zingine ni baada ya kuongezeka neno kwenye public.“Public” ina maana pana zaidi ya watu pekee.
Expression Meaning Public people Watu wa umma Public property Mali ya umma Public service Huduma ya umma Public information Taarifa za umma Public meeting Mkutano wa wazi kwa umma Public interest Maslahi ya umma Public sector Sekta ya umma
Acha uongo, kusema sio kutenda, nikisema "nitakuua" na ikiwa sijakuua itakuaje nimetenda??Inategemea na nia. mfano nikisema
''nitakuua......'' hapa kama nia yangu ni kukutisha basi tendo la kukutisha limetendeka. Lajini kama nia ni kukuua basi tendo halijatendeka mpaka kuwe na nyongeza ya mimi kuchukua siraha na kukufuata.
Kwa kesi ya Lisu kuna muunganiko mwingine labda tusubiri tuone.
Mpaka hii kesi iishe utakuwa umeachana na engineering unapepea kwenda law school 🤣🤣🤣🤣Unajua mie nachoka kabisa, bafala wao waliofungua case waweke uthibitisho na ushahidi usio na shaka juu ya shauri lao. Eti wanawapa kazi mahakama iangalie makosa hayo km ni kweli ya kihaini au laah?
Huyu Katuga ni mzima kweli kichwani?
Ni kama mkalimani tu , hakuna kesi hapoAna ungaunga hatari...
Kwa muktadha wa hii kesi “serikali” haijathibitisha kuwa ilitishika….Inategemea na nia. mfano nikisema
''nitakuua......'' hapa kama nia yangu ni kukutisha basi tendo la kukutisha limetendeka. Lajini kama nia ni kukuua basi tendo halijatendeka mpaka kuwe na nyongeza ya mimi kuchukua siraha na kukufuata.
Kwa kesi ya Lisu kuna muunganiko mwingine labda tusubiri tuone.
Waliotakiwa kuthibitisha kutishika kwao waliogopa/waligoma/walikacha/waliidharau mahakama na kutofika kuthibitisha hilo(wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama),huyo "mkatuga" atathibitisha kwa niaba?Inategemea na nia. mfano nikisema
''nitakuua......'' hapa kama nia yangu ni kukutisha basi tendo la kukutisha limetendeka. Lajini kama nia ni kukuua basi tendo halijatendeka mpaka kuwe na nyongeza ya mimi kuchukua siraha na kukufuata.
Kwa kesi ya Lisu kuna muunganiko mwingine labda tusubiri tuone.
Mahi ujue majuzi tu nikawa najisemea sijui kwanini sikuchukua masomo ambayo Degree ningekua hapo LLB, na LS najiona nikifit hapo kabisa.Mpaka hii kesi iishe utakuwa umeachana na engineering unapepea kwenda law school 🤣🤣🤣🤣
Anasafisha nini sasa anatafutiza kosa kwa kuondoa kuondoa manenohakusikii, tulia katuga anasafisha uchafu wa lissu,