Nimekaa na kutafakari na hii hali inavyo enda jambo moja limenijia nikuwakumbuka mashujaa wetu ktk tansinia ya usalama wa taifa.
Neno au wazo limenijia nikuwaambia macho yenu yafunguweni tena yafunguweni vizuri.
Mchwa sio mdudu mzuri. Anakula chini kisha anaibuka juu unapo muona amesha maliza kazi.
Ndoto yangu inasema mchwaa ako chini ya mihimili ya meza kitu kitawashituwa nakujuwa meza imeshaliwa siku pakiwekwa kitu kizito meza ita anguka.
Wazee andaeni watu wenye brain ktk maeneo nyeti ya taifa, msiangalie mtoto wa nani andaeni vichwa tunaenda kuangushiwa kitu kizito kama hatutojindaa jirani wameshaujuwa mchezo pia wazungu wameshajuwa mchezo na wanaucheza hapa kwenye ardhi yetu.
Narudia tena andaeni watu narudia tena andaeni watu. Narudia tena andaeni watu fanyeni alichokifanya hayati baba wa Taifa ndugu zangu Hayati alitafuta vichwa akavipeleka shule akavipa nafasi ndugu zangu huko duniani hawaangali mtoto wa nani wanatafuta brain unapo ona Bush Baba na mtoto wanakuwa Marais yaani sio mchezo huyu mzee alikuwa na brain na mtoto pia na wote wamenusurika kufa vitani. Angalia mataifa yenye uwezo wa ajabu kama Israel yani hawa jamaa hujafanya mission yeyote kwa ajili ya taifa lao huna nafasi yani hawa jamaa ni wanachaguwa elite unapo muona Mtu kama Benjamin Netanyauh sio kiumbe cha kawaida yani yule kwanza ni genius pia nikomando and last is among Israel Elite group... Ni ninsi gani tuna andaa watu kwa ajili ya kesho nikiza kinene God help us. Maana ni mwendo wa mtoto wa dada, shangaz, wakwe marafiki na makada. Ndugu zangu we will failed acheni ukada acheni ujomba na ubinamu tuchaguwe viongozi who are elite, achen habari ya gender chaguweni vichwa vilivyo simama. Taifa hili lenye zaid ya ++900k m sq ardhi tusipo kuwa makini tutaumiza vizazi vijavyo.
Ndugu zangu hii mchezo inataka kushika kasi baba anamuingiza mtoto na mtoto anakuwa brain ndogo anabebwa nataka kuwaambia italiacha taifa likicheka chooni mtu kama Lissu niwakumpa high position asaidie taifa hata kama ana ubaya gani maana kile kichwa sio chakawaida.
Nimetoa mfano. Taasisi za vyama ziwe na uhuru kuwafanya wenye uwezo na brain kupata urais jamani leo tumpate Rais kama Prof Muhongo hivi tutakuwa wapi as a nation.
Waziri mkuu awe Mzee Prof Issa Shivji italiwaje hili taifa waziri wa ulinzi tunamchukua jasusi ndani ya jeshi ndio waziri wa ulinzi sasa chezeni na gender wenzenu wanajenga nchi imara gender wameweka pembeni na wanajuwa siri nyuma ya gender. Mataifa makubwa na yenye chumi imara haya gender take from me. Na ukitaka proof angalia China, Marekani, Brazil, France, Singapore nk.
Tunafanya masihara ila tuwe makini. Nimemaliza