Makampuni ya Marekani ya kutengeneza semiconductors waitaka serikali ya Marekani kuiondolea vikwazo China

Makampuni ya Marekani ya kutengeneza semiconductors waitaka serikali ya Marekani kuiondolea vikwazo China

Mzee wa kupambania

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2022
Posts
21,111
Reaction score
53,092
17 July 2023,
Washington

20230717_192029.jpg


Umoja wa makampuni ya kutengeneza semiconductor (chips) nchini Marekani US-based Semiconductor Industry Association (SIA), umeitaka serikali ya Biden kuondoa vikwazo ilivyoiwekea China katika kuiuzia baadhi ya semiconductors na katazo la kutoruhusu makampuni ya Marekani kuwekeza katika uzalishaji wa chips nchini China.

Viongozi wakuu wa makampuni hayo wameutaka uongozi wa Biden kuiondolea vikwazo China kwa sababu China ndilo soko kuu la semiconductors duniani.

Viongozi wakuu wa makampuni makubwa ya Marekani ya kutengeneza chips ya Intel Inc, Qualcomm na Nvidia wamekutana leo Washington na maafisa wa biashara, uchumi na ulinzi wa serikali ya Marekani ili kuzungumzia athari wanazopata kutokana na sera ya Marekani kwa China dhidi ya kuiuzia chips.

Hizi ni sababu kuu mbili za viongozi wakuu wa makampuni hayo kutaka serikali ya Marekani kuondoa vikwazo kwa China;

(1)Kushuka kwa mauzo ya semiconductors kadiri Washington inavyozidi kuiwekea Beijing vikwazo. Hivyo wanashindwa kuelewa hatma ya biashara hiyo.

(2)China kuweka vikwazo vya kuiuzia Marekani madini ya gallium na germanium ambayo ni muhimu sana katika utengenezaji wa semiconductors
.

Baada ya kutathmini changamoto hizo viongozi wakuu wa kampuni hizo kubwa za utengenezaji wa chips kwa pamoja wameutaka uongozi wa Biden kuondoa vikwazo kwa China.


 
Tatizo wengi wamejawa ushabiki wanashindwa kuelewa kuwa ile ni biashara

Na China ndio soko kubwa la chips kutokana na kuwa na viwanda vingi vya electronic devices
Changamoto wanazokumbana nazo ni kubwa kwa sababu haya tuseme mzigo mnao kwenye stock unadoda kwa sababu soko lenu kubwa limepigwa pin. Mtalipaje gharama za operating cost

Ok haya wakisema wafanye uzalishaji wamepigwa pin na China kupata madini muhimu

Ndio maana mwisho wa siku hao viongozi wanabaki kusema hawaelewi hatma yao
 
Changamoto wanazokumbana nazo ni kubwa kwa sababu haya mzigo mnao kwenye stock unadoda soko lenu kubwa limepigwa pin. Mtalipaje gharama za operating cost

Ok haya wakisema wafanye uzalishaji wamepigwa pin na China kupata madini muhimu

Ndio maana mwisho wa siku hao viongozi wanabaki kusema hawaelewi hatma yao

🤣🤣🤣
Hili ni pigo kwa Biden na ukizingati uchaguzi unakarribia na hili linaweza kugusa ajira za watu linaweza kumpunguzia credit kwa wapiga kura
 
Hili ni pigo kwa Biden na ukizingati uchaguzi unakarribia na hili linaweza kugusa ajira za watu linaweza kumpunguzia credit kwa wapiga kura
Katika nchi za kibepari ogopa sana sera zako ziumize masuala ya biashara au ajira yaani mapema tu mpinzani wako anakugaragaza chini kwenye uchaguzi
 
Ndio maana sikuzote Xi Jinping ameitaka Marekani kuwe na ushirikiano wa win win situation kati ya mataifa hayo makubwa kiuchumi
Hakuna kipindi cha historia ambacho China na Marekani zilikuwa na uhusiano mzuri sana wa kiuchumi kama wakati wa tawala za hawa maraisi Obama, Hu Jintao, Bush, Jiang Zemin, Clinton
 
Back
Top Bottom