Mzee wa kupambania
JF-Expert Member
- Aug 14, 2022
- 21,111
- 53,092
17 July 2023,
Washington
Umoja wa makampuni ya kutengeneza semiconductor (chips) nchini Marekani US-based Semiconductor Industry Association (SIA), umeitaka serikali ya Biden kuondoa vikwazo ilivyoiwekea China katika kuiuzia baadhi ya semiconductors na katazo la kutoruhusu makampuni ya Marekani kuwekeza katika uzalishaji wa chips nchini China.
Viongozi wakuu wa makampuni hayo wameutaka uongozi wa Biden kuiondolea vikwazo China kwa sababu China ndilo soko kuu la semiconductors duniani.
Viongozi wakuu wa makampuni makubwa ya Marekani ya kutengeneza chips ya Intel Inc, Qualcomm na Nvidia wamekutana leo Washington na maafisa wa biashara, uchumi na ulinzi wa serikali ya Marekani ili kuzungumzia athari wanazopata kutokana na sera ya Marekani kwa China dhidi ya kuiuzia chips.
Hizi ni sababu kuu mbili za viongozi wakuu wa makampuni hayo kutaka serikali ya Marekani kuondoa vikwazo kwa China;
(1)Kushuka kwa mauzo ya semiconductors kadiri Washington inavyozidi kuiwekea Beijing vikwazo. Hivyo wanashindwa kuelewa hatma ya biashara hiyo.
(2)China kuweka vikwazo vya kuiuzia Marekani madini ya gallium na germanium ambayo ni muhimu sana katika utengenezaji wa semiconductors.
Baada ya kutathmini changamoto hizo viongozi wakuu wa kampuni hizo kubwa za utengenezaji wa chips kwa pamoja wameutaka uongozi wa Biden kuondoa vikwazo kwa China.