Nadhani ujamuelewa.

Kuna magari yanasimamishwa muda mrefu hata masaa 4 wakati hata msafara aujaanza kuondoka.

Kuna siku nilishangaa tulisimamishwa kwenye highway kwa masaa 2 sababu ya mwenge wa uhuru alafu mwenge wenyewe ulikuwa unatokea kwenye barabara ya vumbi unakwenda kama mita 500 kutoka kona ya barabara ya vumbi kuingia kwenye highway hadi kwenye jengo nadhani kulikuwa na uzinduzi.

Wale askari niliwashangaa sana, nikasema uwezo wao wa kufikiri na kufanyakazi ni finyu.
 
Huo ni unafiki wao wa kutukana masikini
Kama amesema hivyo basi ni msemo wa kukejeli masikini

Wakati mwingine mnawapuuza hata wakisimama mnatawanyika tu
Hizo ndio zao ooh mtoto wa masikini
Wanajua umasikini ni laana na wanatuchora tu
Ana umasikini gani si atembee kwa miguu sasa
 
Mtoa mada, ulitaka kujenga hoja mzuri,
Ila ulivyochomekea ishu ya barakoa na njanjo nimekudharau Sana!
Lini Taifa lilizuia watu wasivae barakoa na wasipate chanjo?
Nani alikamatwa na polisi kwa kutafuta barakoa yake au chanjo yake?
Unataka uveshwe barakoa kwa nguvu ndio uone kuwa serikali haizuii kuvaa barakoa!
Je, serikali inakamata watu kuwavesha kondom?
Wangapi wameshakufa kwa Ukimwi?

Watu walivaa barakoa na watu walichanja!


Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 

Kiongozi mwizi wa kura akifa hakuna tatizo lolote boss.
 

Mkuu hakuna askari hapa Tanzania, kuna robot zilizovaa nguo za polisi.
 
Dokta wa uchumi anazeeka na umasikini, tena akiwa kiongozi namba mbili wa kitaifa, Waziri wa miaka mingi
 
Nchi Ina amani, lakini haiondoi ukweli kwamba Mdude Nyagali alishawahi kuahidi mitandaoni kwamba ana hamu ya kujilipua kama Al-Qaeda au Al-Shaabab, na kwamba anatafuta timing tu
 
Kwahyo unataka kusema yeye kaongea bila kuyajua yote hayo?!
 
Hujui ulisemalo ngoja nikusamehe tu
 
Nakaziaaaa
 
Umaskini wa akili inaigharimu sana Afrika.
 
Dokta wa uchumi anazeeka na umasikini, tena akiwa kiongozi namba mbili wa kitaifa, Waziri wa miaka mingi
Inashangaza sana mkuu, mtu ana uhakika wa kuhudumiwa yeye na familia yake, kwa kodi zetu mpaka anakufa,

Leo anajiita mtoto wa masikini? Hata kama alizaliwa katika familia masikini, ina maana muda wote aliofanya kazi, tena msomi wa PhD, alishindwa kuondoa umaskini kwao?

Kuitwa masikini, au mnyonge sio sifa nzuri hata kidogo,

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Mimi niseme tu kuwa nchi hii kila kitu ni ku exaggerate. Kuanzia dini(ulokole) ni kukuza mambo tu tofauti na uhalisia na maandiko, magonjwa(Afya) , Ushoga/Usagaji na hata suala la Usalama ni too much exaggerated tofauti na uhalisia. Yaani ni kutiana hofu tu kuwa kuna tatizo kuuuuuubwa. Ndio maana mnaweza kusimama masaa manne kusubiri msafara.
 
Dokta wa uchumi anazeeka na umasikini, tena akiwa kiongozi namba mbili wa kitaifa, Waziri wa miaka mingi
Mshahara haumfanyi mtu kuwa tajiri, labda awe mwizi.

By being employed, you will never become rich. Because what makes someone rich is the profit. If you are employed, profit and loss go to your employer. You right is only your wage. Unless your convert your wage into capital so that you generate profit.

Dr. Mpango kama hafanyi biashara yoyote, na hajawekeza kqenye mradi wowote, na siyo mwizi, ni sahihi kuwa siyo tajiri. Na asiye tajiri ni maskini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…