Makamu wa Rais, Samia Suluhu amtembelea Tundu Lissu hospitalini Nairobi

Makamu wa Rais, Samia Suluhu amtembelea Tundu Lissu hospitalini Nairobi

Huu ndio utu na ubinaadamu, Mungu ambariki sana huyu mama.

Yaani huyu balozi wetu Dr. Pindi Chana, she used to be a very confident lady, sijui confidence yake imepotelea wapi hadi kushindwa kumtembelea Lissu siku zote hizi, lazima Balozi ajisikie aibu, yeye yuko Nairobi kumtembelea Mtanzania, Mbunge, Rais wake wa TLS (Pindi ni Lawyer), Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, ni mpaka VP aje ndipo na yeye aende kumuona Lissu!.

All and all, better late than never.

Wamefanya uungwana mkubwa.

Paskali.
Hakuna uungwana wowote wa Pindi Chana !! Bali unafki uliopitiliza.

Labda Samia ametumia nafasi hiyo, kumuonyesha bosi wake na Ndugai uungwana ni kitu gani!!
 
Akihojiwa na gazeti la Financial Times Lissu amemtaja Rais Magufuli ndiye mhusika mkuu wa kushambuliwa kwake mwisho wa kunukuu.
Na hapo hapo amemshukuru sana kupitia Mama Samia. Amemuomba amfikishie Mh. Rais asante zake za dhati. Nyie makarai endeleeni kuuguza maumivu ya kata moja na kumsikiliza dada yenu Mange.
 
Huyu mama mimi huwa namuelewaa sana anajari utu kwanza siasa tupa kule
 
Ukiachilia mbali cheo chake cha u-makamo wa u-Rais...

Wamama wana huruma sana...


Cc: mahondaw
 
Hivi balozi huyo ndiyo Mara yake ya kwanza kwenda hapo kumtembelea lissu!

Ova
Balozi hakwenda kumtembelea bali amemsindikiza VP(by order)angeshatumbuliwa kama angethubutu.Uzuri VP Samia haiwezekani kutumbuliwa kwakuwa ila inawezekana Balozi(just thinking loudly) akawa ameponzwa though my imaginations might be wrong.
 
Siri imevuja, ndio maana alisema hataenda kwa sababu zake binafsi...
Ninaimani kabisa endapo kama angeenda asingeweza kamwe kufanya alichofanya huyo mama..
Na ni lazima suala hilo lingezua mjadala mkubwa na mzito sana...
 
Back
Top Bottom