Makamu wa Rais, Samia Suluhu amtembelea Tundu Lissu hospitalini Nairobi

Makamu wa Rais, Samia Suluhu amtembelea Tundu Lissu hospitalini Nairobi

vipi yamani ? of course Rais atakuwa anajua kama aatapita kumuangalia Lisu
Lazima itakuwa kapewa go ahead
 
Hakika Makamu Wa Rais Mama Yetu SAMIA SULUHU ameonyesha UCHUNGU Wa Mama Kwa mtoto .Nakupongeza sana Mama Yetu Kwa roho ya HURUMA uliyotuonyesha Watanzania Kwa KUMTEMBELEA Kijana wako Mh.Tundu Lissu Mungu akubariki Mama.
 
Ni jambo laheri kutembelea Wagonjwa Mama Samia umefanya vizuri sana Mheshimwa
 
Serikali imekosea sana wangemwacha huyo Lisu apambane mwenyewe na hali yake

Totally disappointed with this information
 
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Novemba 28, 2017 amemtembelea mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi nchini hapa.

Msafara wa Samia umefika hospitalini hapa saa 11.43 jioni akiwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk Pindi Chana.

Mwananchi lililokuwapo hospitalini hapo wakati Mama Samia, Balozi Chana na maofisa wengine wakiwasili hospitalini hapo.

Lissu amelazwa hospitalini hapo akiuguza majeraha ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 aliposhambuliwa Septemba 7 akiwa nyumbani kwake, Area D mjini Dodoma.

Makamu wa Rais amefika hospitalini akiwa njiani kurudi Tanzania baada ya asubuhi kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta.

Samia anakuwa kiongozi mkuu wa kwanza wa Serikali ya Tanzania kumtembelea Lissu hospitali tangu alipolazwa usiku wa Septemba 7.
Huu ndio utu na ubinaadamu, Mungu ambariki sana huyu mama.

Yaani huyu balozi wetu Dr. Pindi Chana, she used to be a very confident lady, sijui confidence yake imepotelea wapi hadi kushindwa kumtembelea Lissu siku zote hizi, lazima Balozi ajisikie aibu, yeye yuko Nairobi kumtembelea Mtanzania, Mbunge, Rais wake wa TLS (Pindi ni Lawyer), Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, ni mpaka VP aje ndipo na yeye aende kumuona Lissu!.

All and all, better late than never.

Wamefanya uungwana mkubwa.

Paskali.
 
Hakika mama ana busara sana .. Wanawake hongereni kwa upendo na huruma... , Mungu ampe maisha marefu
 
Katika hali ya kawaida huwa namuona Mama Samia kama anasifa nyingi sana za kuwa ni Top Tz maana hakuna sehemu anayopwaya ikifika kutumia busara. Nategemea kumuona 2020 akitupigania baada ya kuongozwa na mzalendo wa kweli JPm.
Kweli huyu maza huwa ana upendo na busara sana sema mfumo unamfanya kuonekana wa ajabu,same to Kassim Majaliwa!!!
 
Pindi Chana mnafiki tu, siku zote yuko Nairobi hajaenda akiogopa kutumbuliwa Leo kajikinga kwenye mgongo Wa Samia ili ionekane hakwenda rasmi ila alimsindikiza mkubwa wake. Tunakuchana Wewe Pindi Chana mnafiki mkubwa.
 
Miezi mitatu na nusu Lissu yuko katika hospitali hiyo. Balozi kipi kilichomshinda muda wote huo kwenda kumuona lissu? Maagizo toka mamlaka ya juu kwa jamaa yule mwenye chuki za kutisha!?

Ina maana kumbe tuna balozi huko? mbona sikuzote hakwenda?
tena pindi chana huyu si mtu w asingida huyu na lissu si ndugu yake kabisa au ?
 
Hivi huyo Barozi amewahi kwenda kumuona au kagongea lifti ya mama?

Kama hajawahi kwenda kilichompeleka leo ni nn?
 
Ilikuwa ni lazima aende sizonje kaamua hivyo

Je huyo lissu angekufa juzi ingekuwaje

Shame on u ziro brain siyo mtoa mada
 
Back
Top Bottom