Makamu wa Rais, Samia Suluhu amtembelea Tundu Lissu hospitalini Nairobi

Makamu wa Rais, Samia Suluhu amtembelea Tundu Lissu hospitalini Nairobi

Mama Samia Suluhu ni Muislam safi, hayupo katika kundi la wanafiq, mama Samia Suluhu ni mcha Mungu mzuri. Hawezi kwa namna yoyote, kwa jinsi anavyoiheshimu imani yake akahujumu chochote kuhusiana na afya ya Lissu. Nina amani kwa hili. Ni ishara njema kama taifa tukiwa na ushirikiano
Mimi ni Mkristo ila tumezidi kwa Roho mbaya na kudhuru .. Waisilamu Swafi wana utu na wanachukia sana kumhudumu mtu..wanapenda haki na wanathamini sana wengine.. Nilikuwa Pemba nilijifunza mengi sana..
 
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Novemba 28, 2017 amemtembelea mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi nchini hapa.

Msafara wa Samia umefika hospitalini hapa saa 11.43 jioni akiwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk Pindi Chana.

Mwananchi lililokuwapo hospitalini hapo wakati Mama Samia, Balozi Chana na maofisa wengine wakiwasili hospitalini hapo.

Lissu amelazwa hospitalini hapo akiuguza majeraha ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 aliposhambuliwa Septemba 7 akiwa nyumbani kwake, Area D mjini Dodoma.

Makamu wa Rais amefika hospitalini akiwa njiani kurudi Tanzania baada ya asubuhi kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta.

Samia anakuwa kiongozi mkuu wa kwanza wa Serikali ya Tanzania kumtembelea Lissu hospitali tangu alipolazwa usiku wa Septemba 7.
Msilogwe kumuamini mwanaccm yeyote hata awe na cheo gani , Huyu mama aliyoyafanya kwenye BMK hatuwezi kuyasahau .
 
I wish niione sura ya gari letu font ford baada ya dereva wetu kuonana uso kwa uso na Mama Suluhu!!!

Btw Mama kacheza baada ya ukakasi wa kupokelewa na balozi wetu na huku kwenye uzi pale Nyayo stadium kufanywa kama nobod!!
Aisee kwa hiyo Gari letu brand name yake ni Sizonje na Dereva wetu ni Lissu The Great?
 
Pindi Chana mnafiki sana. Muda wote yupo Nairobi hakuweza kwenda. Now ndio kajipendekeza na Mama
 
..mama Samia anajua sana mchango na potential kubwa ya Lissu kwa nchi hii....maana alifanya nae kazi kwenye bunge la katiba akiwa spika...na yeye na nchi nchi ya tz wanajua mchango wa Lissu kwenye bunge lile.....nawaza tu mchango wa JPM kwenye bunge lile... Maana kila mtu anajua mchango wa Lissu... Akiwemo mama Salmia aliyekuwa spika wa bunge lile...
 
Hivi huyo Barozi amewahi kwenda kumuona au kagongea lifti ya mama?

Kama hajawahi kwenda kilichompeleka leo ni nn?
Ukienda nchi yeyote cha kwanza unatakiwa kuripoti ubalozini na kujiandikisha akina mbowe na hilo group LA dereva na hao wala ruzuku ya Chadema na michango ya kuuguza Lisu walipofika walienda ubalozi kuripoti? Na kujisajili passport zao na uwepo wao na uwepo wa mgonjwa Nairobi kama sheria zinavyotaka?
 
wale tomaso picha hiyo hapo

24068467_1406319476145689_8782610672797143368_o.jpg
23926375_1406319432812360_4318115825758643684_o.jpg
 
Anaenda kinyume na "mtakatifu". Ngoja tusubiri , kuna mmoja aliambiwa 'anavipele'
 
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Novemba 28, 2017 amemtembelea mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi nchini hapa.

Msafara wa Samia umefika hospitalini hapa saa 11.43 jioni akiwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk Pindi Chana.

Mwananchi lililokuwapo hospitalini hapo wakati Mama Samia, Balozi Chana na maofisa wengine wakiwasili hospitalini hapo.

Lissu amelazwa hospitalini hapo akiuguza majeraha ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 aliposhambuliwa Septemba 7 akiwa nyumbani kwake, Area D mjini Dodoma.

Makamu wa Rais amefika hospitalini akiwa njiani kurudi Tanzania baada ya asubuhi kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta.

Samia anakuwa kiongozi mkuu wa kwanza wa Serikali ya Tanzania kumtembelea Lissu hospitali tangu alipolazwa usiku wa Septemba 7.
Kuna wakati huwa nawakubali sana waislamu, in short siyo waoga!.......sijasema Bakwata nimesema waislamu nieleweke vizuri hapo!
 
Back
Top Bottom