Dogo alikuwa kajichokea, dini imebadilisha kabisa maisha yake. Ana tembelea Gari, Mercedes Benz G Guard ya zaidi ya bilioni moja.
Sasa kaja kivingine, anahama pale Millennium Tower Phase 2 na kuhamia rasmi Mwenge alikonunua eneo kwa mabilioni ya FEDHA, pale ilipokuwa Century Cinema.
Washikaji, tutafute upako ili tutoboe
Ni biashara poa sana, maana wengi wetu bado wajinga,kama Mungu kakupa kipaji cha kuongea, upo charismatic, eloquent, una ka degree, na uelewa kidogo, fungua kanisa tu, watu kama Dokta Mwaka, Masoud Kipanya, Oskar Oskar, Sugu,wakifungua makanisa, mpunga nje nje,
Huwa nawasikiliza Kuhan Musa, na Mwamposa, nabaki natabasamu tu!
Tangu kipindi hicho, cha miaka ya, 90,mikutano ya injili ilipoanza pale Jangwani, Sijawahi kukutana na kilema, aliyepona ninaye mjua kitaa nilipokuwa naishi, wengi tunaowaona wakitupa magongo, na kunyooka viungo, kwa sababu moja au nyingine huwa sio wakazi wa kitaani eneo Hilo!
Ukiwa dar, utaaambiwa wametoka kigoma, kagera, mkutano ukienda singida, watoa ushuhuda, watatoka mtwara! Miujiza hii!