Mbona mnafikiri kama watoto wadogo vile ambao hata chekechea hawajafika...?
Ni huyu huyu muhusika kwa maagizo ya boss wake aliyekuwa Rais hayati John P. Magufuli...!
Ushahidi ni mlolongo wa matukio yasiyo ya kiungwana wala kubeba utu wa binadamu aliyotendewa victim (Tundu Lissu) na serikali ya Rais Magufuli (mtuhumiwa namba 1) wa unyama huo...
Aidha wote tunajua kuwa huyu jamaa (Paul Makonda) ndiye alikuwa "toto pendwa" wa Mwendazake na ndiye alikuwa anatumiwa kwenye kazi chafu chafu za viongozi wa serikali akiwemo Rais Magufuli...
Siku hiyo tukio hili linstokea, ndani ya mkoa wake (akiwa RC - DSM), kulikuwa na tukio Ikulu ya Rais kupokea taarifa/ripoti ya makinikia ya almasi. Ilikuwa ni ajabu "toto pendwa" huyu kutoonekana kwenye tukio hilo. Kumbe alikuwa Dodoma akiongoza kikosi cha mauaji ya Tundu Lissu bwanaπππ!!!!
Sasa angalia mlolongo wa matukio ya ushahidi wa kimazingira kuonesha uhusika wake na Rais wake (Mwendazake Magufuli...)ππ»ππ»ππ»
1. Kauli za Hayati Rais John P. Magufuli mwenyewe kuwa "....Watu wote wanaoipinga serikali wakati ikiwa ktk vita ya kiuchumi, nyie askari mnajua huwa wanafanywa nini. Obviously, hawastahili kuishi...." Dakika chache baada ya kauli siku hiyo tarehe 7/9/2024, Dodoma eneo la AREA D, makazi ya viongozi, jamaa akamwagiwa risasi zaidi 37 akiwa ndani ya gari lake...
2. Eneo hilo la makazi ya viongozi ambalo huwa na ulinzi 7days & 24hrs mwaka mzima, siku hiyo na muda wa tukio hilo hakukuwa na mlinzi hata mmoja kwenye mageti yote..!
Swali rahisi tu ni hili: Hivi ni nani mwenye nguvu za kimsmlaka na uwezo wa kuondoa walinzi (askari polisi wote) kwenye lindo lao siku hiyo..???? Akili kichwani mwako...
3. Jengo - Apartment aliyokuwa akiishi Tundu Lissu alikuwa akiishi pia Waziri wa Nishati na Madini by then Meadard Kalemani na Waziri wa Afya (by then) Dr Haji Mponda. Aidha apartment hiyo ilikuwa na CCTV Cameras. Baada ya tukio, polisi walizichukua na mpaka leo polisi wanazo na hawataki kusema waliona nini...!!
4. Kunyimwa stahili na haki zake za matibabu huku akiwa mtumishi wa umma (mbunge....)
5. Kuvuliwa ubunge wake kwa sababu eti ni "mtoro kazini, hajulikani aliko..."
6. Job Ndugai (Spika wa Bunge by then) aliamuriwa na Rais Magufuli kuwa, akifa hata asiingizwe kwenye jengo la Bunge kuagwa na wenzake na badala yake maiti usiku kwa usiku ipelekwe kijijini kwao Singida na kuzikwa. ..
Duuh, hiyo βπ»βπ»βπ» ni chuki na unyama uliopitiliza viwango vya shetani mwenyewe...!!
7. Wananchi kuzuiliwa na kupigwa marufuku na serikali ya CCM chini ya Hayati John P. Magufuli ku - sympathize na victim, familia yake, ndugu zake, wanachama na chama chake, mashabiki na wapenzi wake (kina sisi) hadharani kuvaa t-shirt za "GET WELL TUNDU LISSU", kufanya maombi kwenye viwanja vya wazi, kuchangia fedha za matibabu nk. Waliofanya haya, basi ilikuwa ni kwa kificho sana....
8. Wabunge wa CCM kupigwa marufuku na serikali na chama chao kwenda kumuona na kumsalimu hospitalini Nairobi na Ubelgiji. Waliofanikiwa kwenda ni kwa kuwa walikuwa na roho ngumu tu na badae baadhi walitoka CCM e.g Lazaro Nyalandu...
9 Funga kazi ni DRAMA za serikali kupitia Jeshi la Polisi, kukataa kutenda wajibu wao wa kuchunguza tukio hili la kihalifu (political attempted assassination) kwa vusingizio vya mara dereva kakimbia, mara Tundu Lissu mwenye kakimbia na hataki kutoa ushirikiano na ujinga mwingine mwingi kuanzia polisi wenyewe, Rais, mawaziri, bunge na,mamlaka zingine...
##Mpaka hapo na kwa circumstantial evidences hizi tunakosaje kuwajua wahusika? Na serikali ni kwanini ilikuwa inataka kumuua Tundu Lissu kijinga na kishamba kiasi hiki..??