Makonda huna mamlaka juu ya Mawaziri na Wakuu wa Mikoa

Makonda huna mamlaka juu ya Mawaziri na Wakuu wa Mikoa

Kilio au watu wanapaza sauti kuwa muovu wa utawala wa magufuli karudishwa kwenye madaraka?
Watu wanafki tu hao, hao ndio walitaka Fisadi Lowassa awe rais wa hii nchi kisa alisema elimu elimu elimu.

Hawako serious.
 
Yani hata mseme nini, ndio kashatoa maelekezo. Na sisi wananchi leo tumefarijika sana kumuona kafika kwenye kiti hicho. Na Mungu ni Mwema, atafika mbali zaidi tunapopataka.

Hold it there, ni ww usiseme sisi maana hujui wengine wanafikiria nini
Kisheria mwenye mamlaka hayo ni rais pekee
Yeye ni nani?
Kama kiongoz kuna kauli za kuchunga kuongea. Jua mipaka yako
 
Umesikika katika hotuba yako ya leo kuwa utawarukia mawaziri na wakuu wa mikoa. Nakutahadharisha wewe ni kama Ahmed Ally wa Simba au Ali Kamwe wa Yanga,
Au kama speaker kwenye gramaphone
 
Yani hata mseme nini, ndio kashatoa maelekezo. Na sisi wananchi leo tumefarijika sana kumuona kafika kwenye kiti hicho. Na Mungu ni Mwema, atafika mbali zaidi tunapopataka.
Kwa hiyo unafarijika kuona tu ametoa maelekezo?

Kweli ujinga kipaji!
 
Yani hata mseme nini, ndio kashatoa maelekezo. Na sisi wananchi leo tumefarijika sana kumuona kafika kwenye kiti hicho. Na Mungu ni Mwema, atafika mbali zaidi tunapopataka.
Kweli mimi nataka mganga wa Makonda lazima nimjue, yaani jamaa amekaa miaka mitatu kimyaaa kaja na hotuba moja kabadilisha dance badala ya mapigo ya katiba mpya/Bandari yetu tumegeukia midundo ya Makonda.
Makonda heshima yako hili game unaliwezaaaaaa.
 
Mkuu hujamuelewa Makonda, ametuma ujumbe mapema kwa mawaziri, wabunge, viti maalum, wakuu wa mikoa, wakuu wa Wilaya kujiandaa kumuona mapema maana kwenye uchaguzi ujao yeye ndiye mwenye chujio!

Miaka mitatu ya kusota sio mchezo, kasota sana, anataka kufidia na kujijenga. Kama hawatamuelewa mapema wajiandae kwa vilio!
Hana impact bana!! Msimpe ukuu ambao hastahili. Katibu Mwenezi anahusika vipi kuchagua RC au Mbunge
 
How?, chama ndicho kinachounda serekali, msemaji ndani ya Chama ni mwenye nguvu ya ushawishi kwa hali ya juu,.
Hiyo nguvu anaitoa wapi? Msemaji ni "mtumwa wa Katibu Mkuu". Hakuna taarifa atatoa bila kuidhinishwa na Katibu Mkuu.

Hawezi kwenda hata Kolomije bila kuomba bajeti ya mafuta, gari na per diem kwa Katibu Mkuu.

Hivi nyie vichwa vyenu vina kazi gani?
 
Ila i don't know why nafurahi sana nikianza kumsikia huyu jamaa akiongea... He, deserve to lead hata kama anaweza kuwa na mapungufu yake ila kiti kinamuenea vyema
Yeah kiti kinamuenea vyema....Elewa maneno "Kinamuenea vyema"[emoji848]
 
Acha ujinga wewe unajua cheo cha katibu wa halmashauri kuu ya taifa itikadi na uenez??

NapitaKamaRadi
Usimwite mwenzio mjinga kwa kumuuliza mawaswali, Muite mjinga kwa kuanisha majukumu ya seccretariate ya sisasa na uenezi ya chama cha mapinduzi kama ilivyoanishwa katika katiba ya chama cha mapinduzi ya mwaka 1977 na marekebisho yake ya mwaka 2018. Hayo madaraka juu ya mawaziri hana kasome ibara ya 107 ibara ndogo ya 2 sehemu a,b,c,d,e,f utaona majukumu wa katibu wa secretaiate hiyo. kama hujasoma kasome ndugu acha uzwazwa
 
Tulia wewe hujui chochote
 
Hiyo nguvu anaitoa wapi? Msemaji ni "mtumwa wa Katibu Mkuu". Hakuna taarifa atatoa bila kuidhinishwa na Katibu Mkuu.

Hawezi kwenda hata Kolomije bila kuomba bajeti ya mafuta, gari na per diem kwa Katibu Mkuu.

Hivi nyie vichwa vyenu vina kazi gani?
Hawa wanaojiita wanachama wa ccm sio wanachama maana mikononi mwao hawana kadi za chama, katiba ya chama, kanuni za utekelezaji wa katiba ya chama, ilani ya uchaguzi na katiba ya nchi. Walichojaa ni ushabiki wa mtu fulani kutokana na kuwa na tabia wanazozipenda lakini si kutokana na kaliba ya uongozi au karama ya uongozi, naomba uwaongoze katika katiba ya ccm ibara ya 107(2)a,-f
 
Tulia wewe hujui chochote
Eleza unachojua unless otherwise utulie wewe, hii tabia ya kuvunja katiba ndani ya chama ndio imezaa viongozi wanaovunja katiba ngazi ya serikali, kanisomee katika katiba ya chama na kanuni zake wapi secretariate ya siasa, itikadi na uenezi inakua na nguvu juu ya mawaziri walioko chini ya Rais ambaye ni Mwenyekiti wa Chama na Serikali.
 
Hiyo nguvu anaitoa wapi? Msemaji ni "mtumwa wa Katibu Mkuu". Hakuna taarifa atatoa bila kuidhinishwa na Katibu Mkuu.

Hawezi kwenda hata Kolomije bila kuomba bajeti ya mafuta, gari na per diem kwa Katibu Mkuu.

Hivi nyie vichwa vyenu vina kazi gani?
Anaushawishi /au anaweza kupendekeza wazo lake kwa Katibu Mkuu, do you catch me!
 
Eleza unachojua unless otherwise utulie wewe, hii tabia ya kuvunja katiba ndani ya chama ndio imezaa viongozi wanaovunja katiba ngazi ya serikali, kanisomee katika katiba ya chama na kanuni zake wapi secretariate ya siasa, itikadi na uenezi inakua na nguvu juu ya mawaziri walioko chini ya Rais ambaye ni Mwenyekiti wa Chama na Serikali.
CCM ina nguvu kuliko miimili yote ya serikali sababu bila chama huyo waziri hayupo na makonda kama katibu wa uenezi ana impact kubwa sana kwenye chama.
 
Back
Top Bottom