PakiJinja
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 11,689
- 25,848
Mitaani kwetu enzi hizo ilikua mwizi akikurupushwa watu wanaanza kumkimbiza na kumpigia kelele za mwizi, akipigiwa kelele hizo mwizi hupata matumaini ya maisha yake kuokolewa. Maana kati ya wakimbizaji watajitokeza makatili, pia wana usalama na hata viongozi wa mtaa. Hapo lazima asalimike.Katibu wa itikadi na Uenezi CCM bwana Paul Makonda amesema tangu ameanza kufanya mikutano ya kisiasa na kwenda kwa wananchi hawaoni watoa taarifa wakifanya mikutano!
Anasema amechoka kufanya mikutano peke yake anauliza eti watoa taarifa wanafanyia mikutano wapi? Mbona wanamuacha anatamba peke yake?
Anasema watoa taarifa kama wamekwama popote na kushindwa kufanya mikutano waseme wasaidiwe.
L
Siku moja aliibuka mwizi watu wakaanza kumkimbiza kimyakimya, hakuna filimbi wala kelele za mwizi.
Kuona anakimbizwa kimyakimya mwizi akachanganyikiwa, akikatisha uchochoro watu wananong'onezana, kapita hapa, mkatishieni kwa pale mbele...kwa kifupi ingekua ni miaka hii basi tungesema wanamkimbiza kwa kutumia 'whatsapp group'.
Mwizi alipoona ukimwa wa wale watu ikabidi aanze kujipigia kelele mwenyewe na badala kukimbilia vichochoroni akaanza kuelekea eneo lenye watu wengi huku akioiga kelele "Jamani mimi ni mwizi, nimeiba lakini hawa wanakimbiza kimyakimya". Watu wakamshika na kumuuliza kulikoni, hapo wale wanaomkimbiza wakawa wameshafika, wakawa wanamchukua, jamaa anakataa, wasikubali wamchukue. Wale jamaa wakasema huyu wala siyo mwizi ni ndugu yetu huyu sema amepata matatizo ya akik8 ndiyo tunamkimbiza tumkamate tumpeleke hospitali.
Sitamalizia ilivyoishia sababu si lengo la mimi kusimulia.
Nikionacho hapa huyo Makonda ameshikwa na hofu kama yule mwizi.