Makundi ya wanaopinga ndoa na maisha ya ndoa

Makundi ya wanaopinga ndoa na maisha ya ndoa

Kuna baadhi humu uelewa wenu ni mdogo sana muktadha wa mada ni kutaja makundi... Na sio uchambuzi, kama ni uchambuzi nimeshafanya kwenye mada zilizotangulia.. Muwe mnaelewa mada kabla ya kuchangia
 
Hali inazidi kuwa mbaya kwa vijana wetu hasa hawa wa kiume wanahamasishana kila kona na kampeni yao yenye hashtag #KATAA NDOA

Sababu wanazotoa zinachekesha mno na kwakweli hazina mashiko.. Kubwa ikiwa ni kuogopa kusalitiwa lakini pia kuna la uchoyo na kukwepa majukumu ila haya hawayasemi kwa uwazi

Hili jambo ni kama fasheni yenye mass hallucination ndani yake! Itapita lakini inaweza kuacha madhara kwa wengine hivyo hatuwezi kukaa kimya

Haya ndio makundi yao

1. Wasiojiamini..
Hawaamini kama wanaweza kutunza mke kutokana na story za vijiweni
Hawaajiamini kama wanaweza kumridhisha mwanamke kitandani
Hawajiamini kama wanaweza kutulia kwenye ndoa bila kuwa na vimada
Hawajiamini kwamba watapendwa na hawawezi kusalitiwa!


2. Wenye kasoro za kimaumbile
Wanaojihisi ni vibamia
Wanaojihisi hawawezi kumpa mwanamke ujauzito
Wasiotahiriwa
Wagumba kwa ithibati

3. Waathirika kisaikolojia
Kutokana na makuzi mabaya
Kutokana na malezi mabovu
Waliolelewa na walezi katili
Walioathirika na punyeto
Walioumizwa kimapenzi
Waliosalitiwa

4. Wasela na wakaa geto
Maisha hayajasimama
Wanaishi kwa kuungaunga
Wasiopenda majukumu

5. Wenye kasoro za kijinsia
Mashoga wa kujificha (mchicha mwiba)
Madomo zege
Wenye ulemavu uliojificha

6. Wapenda kitonga, dezo
Wanaolelewa na wake za watu
Wanaotunzwa na mashangazi
Wanaopenda vya bure toka kwa yeyote
Wapenda shortcut
Wavivu wasipenda kujishughulisha
Wapenda starehe

7. Bendera fuata upepo
Wanashadadia tu kwasababu fulani kasema
Wanafuata mkumbo kwakuwa fulani yumo
Wanadhani ndio usasa na ndio ujanja

Washauri wao wakuu
Walioshindwa kuhimili changamoto za ndoa
Walioachwa, waliopigwa kibuti
Walioharibu kwenye ndoa zao
Wapotoshaji

Nisiandike sana ngoja niweke kituo hapa
Watu wawe huru na maamuzi yao kama unapenda kuoa ingia kwenye hiyo taasisi na kama hupendi kaa kando. Hamna sheria ya nchi inavunjwa ukiamua kati ya hivyo viwili.
 
Ni ujinga wa hali ya juu sana kujivunia ndoa. Kila mtu anajua madhara na uharibifu wa ndoa katika maisha ya watu kwa sasa, kwa hiyo usitupigie kelele.

KATAA NDOA
 
Wanaopinga ndoa ni watoto wa masingle mother ,mtoto aliye lelewa na wazazi wake wawili hawezi kusema ndoa haina maana.
Hijafikiria vizuri. Waza tena juu ya ndoa.
 
Sema nn mm siwez kuwalaumu sababu hawana kosa sasa kama naona ndoa za watu zinavyovunjika hovyo kila siku nasikia ugomvi kwenye ndoa kila siku naona wake za watu wanavyochepuka unadhani nitakuwa na moyo wa kwenda.

Kitu kingne mfano hali yangu sio nzuri najua kabisa mm mwenyew kula kwa shida then uniambie nioe ni heri kufa single kuliko watoto kuishi hali niliyoishi mm.

Kitu kingne mfano najijua mm ni mgumba naend kuoa mke wa kazi gani ili niwe nasikia tukisemwa mtaani kuwa hawana uwezo wa kuzaa ya nn kumtesa mke wangu si bora aolewe na wenye uwezo wa kumzalisha.

Kitu kingine umeandika walioathiriwa na punyeto sijajua unamaanisha nn ila kwa nilivyoelewa kama mm najijua punyeto imeniharibu na uume upo legelege pengne hata bao moja ni kazi asa nikaoe mke wa nn kama sio kuliwa tu hapo labda nipate dawa ya kunitibu nd hvy watu wahuni madoctor fake.

Inshort kuoa sio lazima hata biblia imesema (“Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo.“Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe, maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa,Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza,wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe.)

Kwahiyo ukiona huwez kujizuia ndio uoe.
 
Sema nn mm siwez kuwalaumu sababu hawana kosa sasa kama naona ndoa za watu zinavyovunjika hovyo kila siku nasikia ugomvi kwenye ndoa kila siku naona wake za watu wanavyochepuka unadhani nitakuwa na moyo wa kwenda.

Kitu kingne mfano hali yangu sio nzuri najua kabisa mm mwenyew kula kwa shida then uniambie nioe ni heri kufa single kuliko watoto kuishi hali niliyoishi mm.

Kitu kingne mfano najijua mm ni mgumba naend kuoa mke wa kazi gani ili niwe nasikia tukisemwa mtaani kuwa hawana uwezo wa kuzaa ya nn kumtesa mke wangu si bora aolewe na wenye uwezo wa kumzalisha.

Kitu kingine umeandika walioathiriwa na punyeto sijajua unamaanisha nn ila kwa nilivyoelewa kama mm najijua punyeto imeniharibu na uume upo legelege pengne hata bao moja ni kazi asa nikaoe mke wa nn kama sio kuliwa tu hapo labda nipate dawa ya kunitibu nd hvy watu wahuni madoctor fake.

Inshort kuoa sio lazima hata biblia imesema (“Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo.“Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe, maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa,Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza,wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe.)

Kwahiyo ukiona huwez kujizuia ndio uoe.
Asante kwa mchango mzuri wenye uwazi na unaoakisi uhalisia ambao wengi hawataki kuusema bali wanakimbilia sababu nyingine tofauti kabisa
 
Ndoa imara hujenga familia bora na jamii bora.

Wanaokataa ndoa wana agenda zao zinazotaka tuwe na taifa la hovyo.
 
Ndoa ni muunganiko kati ya mwanamume na mwanamke, walio amua kwa ridhaa yao wenyewe kuishi pamoja kama mke na mume mpaka mwisho wa maisha yao ya ndoa.

Aina za ndoa kwa mujibu wa sheria

Kuna aina mbili tu za ndoa zinazotambulika na sheria ya ndoa Tanzania

Ndoa ya mke mmoja na mume mmoja tu.
Ndoa ya wake wengi.
Ndoa hizo zinaweza kusheherekewa kufuatana na misingi na taratibu za kidini, kimila au kiserekali, kushuhudiwa na watu wasiopungua wawili na kusajiliwa kwa mujibu wa sheria.

Hatua za kuchukua kabla ya ndoa kufungwa

Lazima taarifa ya nia ya kufunga ndoa itolewe siku 21 kabla ya ndoa kufungwa, kama kutakuwa na mwenye pingamizi budi litolewe itoe kabla ya ndoa kufungwa
Majina ya wale wanaotarajia kufunga ndoa, umri, majina ya wazazi wao na mahali wanapoishi yatajwe.
Tamko kwamba wanaotarajia kufunga ndoa hawana uhusiano unaokatazwa kisheria kufunga ndoa
KUSAJILI NDOA

Ndoa inaweza kufungwa Kiserikali au kwa madhehebu ya Kikristo au Kiislam au kufuatana na mila na desturi za wale wanaofunga ndoa.

Msajili wa ndoa atatoa cheti cha ndoa. Kila Ndoa inapofungwa lazima iwe na mashahidi wawili

Mambo ambayo sheria ya ndoa inakataza katika suala zima la kuoa au kuolewa

Mwanamke na au mwanaume kuolewa/kuoa bila ridhaa yake mwenyewe
Mwanamke na mwanaume wenye undugu wa damu kuoana
Mwanamke na mwanaume kuoana kabla ya kutimiza umri unaoruhusiwa kisheria (kwa mwanaume miaka 18 na kwa mwanamke miaka 18 au 15 kwa idhini ya wazazi/mlezi wake)
Kuoana watu wa jinsia moja
Mwanamke na mwanaume kutaka kuoana kwa mkataba wa kipindi maalum.
Haki za mume na mke katika ndoa

Wote wana haki ya kumiliki mali kama nyumba, shamba n.k. kwa majina yao binafsi;
Wote wana haki ya kutoa idhini katika uuzaji au kwa pamoja kuweka dhamana mali yoyote ya familia;
Wote wana haki ya kuishi katika nyumba ya familia iwapo mume/mke amemkimbia;
Mke ana haki ya kupewa matunzo yake na ya watoto wakati wa ndoa au iwapo mume amemkimbia, wameachana kwa amri ya mahakama. Na mume ana haki ya kupewa matunzo iwapo ana ulemavu hawezi kujiingizia kipato kutokana na ulemavu au ugonjwa wake;
Wote wana haki ya kutokupigwa na au kufanyiwa ukatili wa aina yoyote;
Wote wana haki ya kupeana unyumba;
Wote wana haki ya kutumia mali ya ndoa;
Wote wana haki kuomba amri ya talaka.
Ukomo wa ndoa Ukomo wa ndoa uko wa aina mbili:

Kifo cha mwanandoa mmoja wapo
Talaka ambayo imetolewa na Mahakama pekee pale inapojiridhisha kwamba kuna sababu ya msingi kufanya hivyo.
Baraza la usuluhishi la Ndoa

Baraza la usuluhishi la Ndoa, ni baraza lililoanzisha na kifungu 102 cha Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, sura ya 29 kama sheria zilizopitiwa mwaka 2002, kwa madhumuni ya kusuluhisha wanandoa ambao wanaingia kwenye migogoro ya Ndoa. Kazi za Baraza la Usuluhishi la Ndoa:-

Kusuluhisha Wanandoa walioko kwenye Ndoa baada ya kupokea lalamiko toka kwa mmoja wapo wa Wanandoa
Kutoa hati maalum kuthibitisha kuwa suluhu imeshindikana na kuelekeza wanandoa kwenda Mahakamani kwa amri zaidi.
MUHIMU: Mahakama peke yake ndiyo ina mamlaka ya kutoa amri ya kutengana au talaka

Sababu zinazopelekea au kuishawishi mahakama kuvunja ndoa:-

Uzinzi kati ya wanandoa
Ukatili kati ya wanandoa au watoto wa ndoa
Dharau au kupuuza kulikokidhiri dhidi ya mwenzi
Kumtelekeza mwenzi kwa zaidi ya miaka mitatu Pale mwenzi anapofungwa kifungo cha maisha au kwa kipindi kisicho pungua miaka miaka mitano
Ikiwa mwenzi ameugua ugonjwa wa akili na imedhibitishwa na daktari kwamba hakuna uwezekano wa kupona.
Kubadili dini baada ya ndoa kufungwa pale wanandoa wote walikuwa wakifuata imani ya dini moja.
Haki za wanandoa zinazoambatana na amri ya talaka

Mgawanyo wa mali za ndoa /familia
Matunzo ya mke Hifadhi na matunzo ya watoto
Kizuizi cha kutobugudhiwa
Kuoa/Kuolewa tena
Fidia ya uzinzi
Gharama za kuendesha Shauri la Talaka
Haki ya Mgawanyo wa mali za familia/ ndoa Mali yoyote ambayo imepatikana wakati wa uhai wa ndoa na kwa nguvu na au machango wa pamoja wa wanandoa.

Iwapo mali iliyopatikana na mwanandoa mmoja wapo kabla ya ndoa au kwa nguvu zake mwenyewe lakini imeboresha/imetunzwa na mwanandoa mwingine mali hiyo itatambulika kama mali ya ndoa.

Lakini kama kuna mali yoyote ambayo mwanandoa mmoja amempa mwanandoa mwenzake kama zawadi, mali hiyo itakuwa ya yule aliyepewa pekee.

Aina za mchango

Kutekeleza kazi nyumbani hasa kutunza familia; mfano kuosha vyombo, kupika, kufua nguo, kubeba maji na kazi zingine zinazofanana na hizo kwa maslahi ya familia.

Kutunza mali za ndoa: mfano kufyeka, kulima, kuvuna shamba, kufanya marekebisho ya mali za ndoa kwa maslahi ya familia.

Mchango wa fedha wa mwanandoa katika kununua mali.

Haki ya Matunzo ya mwanandoa

Jukumu la kutoa matunzo kwa mke na watoto ni la mume, jukumu hilo litatekelezwa wakati wa uhai wa ndoa na baada ya talaka.

Haki ya Hifadhi na matunzo ya watoto

Hifadhi ya watoto hutolewa kwa mume au mke au mtu baki (mlezi) hasa kwa kuzingatia ustawi na maslahi ya wale watoto. Zaidi ya hayo, mahakama pia inaweza kuzingatia yafuatayo:

Umri wa wale watoto, mfano, watoto walio chini ya miaka saba kipaumbele cha hifadhi hupewa mama mzazi; labda kama kutakuwa na sababu za msingi za kuto fanya hivyo. Mfano kama mama mzazi ana matatizo ya kiakili, anaishi katika mazingira hatarishi.

Mazingira ya mahali watakapoishi watoto, mfano, kama mazingira ya upande mmoja ni hatarishi kwa ustawi wa mtoto, basi haki ya hifadhi atapewa mzazi mwingine bila kujali umri.

Matakwa ya wazazi wa mtoto nani kati yao angependa kupewa hifadhi ya watoto

Mila na desturi za jamii ambayo wanandoa wametokea.

Kama mtoto anaumri zaidi ya miaka saba na ana uelewa wa kutoa mapendekezo yake, basi matakwa/maoni yake yatasikilizwa zaidi.

Haki ya hifadhi ya mtoto haimnyimi mzazi mwenza haki ya kumuona na au kumtembelea mtoto/watoto. Haki ya hifadhi ya mtoto haiondowi jukumu la baba kutoa matunzo.
Men were meant to build.

Build skills, build businesses, build functional relationship and family dynamics.

A man who isn’t building loses a part of himself and becomes a shell of his former self.

Don’t fall victim to the appeal of overconsumption, become a creator.
 
zamani ukioa ilikuwa ni fahari ila kwa nyakati hizi hadi kuku watakushangaa
Men were meant to build.

Build skills, build businesses, build functional relationship and family dynamics.

A man who isn’t building loses a part of himself and becomes a shell of his former self.

Don’t fall victim to the appeal of overconsumption, become a creator.
 
Unaoa dunga embe unategemea nini ? Mwanamke amechakazwa na wanaume zaidi ya 20 halafu wewe unajipeleka kuoa!!
Oa bikra ufurahie mema ya nchi
Nadhani kampeni ingeelekezwa "Kataa Malaya oa bikra" na ubikra wenyewe uwe unathibitishwa na Daktari mwaminifu na mienendo safi, na rekodi za binti, hili lingejenga hofu kwao na wangeanza kujitunza,akifahamu akicheza hovyo ndoa haipo na atakuwa amejizalia toto lake!
 
Back
Top Bottom