Binafsi siungi kampeni ya kataa ndoa,kwasababu ninaamini familia bora lazima iwe na msingi wa baba na mama,
ila hizo sababu ulizoziandika hapo juu itakuwa ni mtazamo wako tu,maana haujaandika kwa kuchambua kwa kina,umeandika kiushabiki ule wa simba na yanga,tegemea wapingaji wengi kwenye huu uzi wako tena kwa hoja za uzito,
kama kweli ulikuwa na nia ya kuwaelimisha watu kuhusu umuhimu wa ndoa hukupaswa kuandika kimipasho hivo kwa kutegemea uungwaji mkono kwa member wengi ambao wanaunga mkono kuhusu ndoa,
ulipaswa uelezee umuhimu na faida za kuwa kwenye ndoa pia ungeelezea hasara ya kutokuwa na ndoa