Makundi ya wanaopinga ndoa na maisha ya ndoa

Makundi ya wanaopinga ndoa na maisha ya ndoa

Kuna mshkaji wangu mmoja tulikuwa tunakaa naye vikao mara kwa mara, sasa majuzikati kajichanganya akaoa! Hivi sasa kila weekend lazima aje kwangu anipe sim niongee na mke wake nimuombee ruhusa!!!
Nimemwambia weekend hii ndo mwisho atafute njia nyingine ya kutoka kwake au atulie na familia yake aenjoy (kama mnavyodanganyana) maana ndo maisha aliyochagua.
Kuomba ruhusa? 😂 Kumaanisha nini yaan niombe ruhusa mwanaume niombe ruhusa kwenye mji wangu? Ameoa au ameolewa?
 
Mkuu mwanaume huwa anaaga na sio kuomba ruhusa.

Mwanaume kabla ya kuondoka nyumbani unamuaga mkeo kuwa unaenda sehemu fulani kwenda kufanya jambo fulani ili ukipata tatizo iwe rahisi kujua na namna ya kukusaidia na sio kuomba ruhusa.
Wanawake wakishaolewa wanageuka kua wababe wanaume wengi wanapigwa na wake zao Ila hawasemi wanaogopa aibu, kuna mzee alidhoofu kwa msongo wa mawazo sababu ya kipigo na mdomo mkewe anarap vibaya yaan akianza kurap anabwata anafokafoka mzee akili zinaruka anapoteza amani ya moyo

Wakishaolewa wanataka wammiliki mwanaume kabisa yaan awe km mtoto akitaka kwenda popote aombe ruhusa akikataliwa basi hakuna kwenda hata kazini mwanamke anaweza akaamka na amri tu leo hakuna kwenda kazini mwanaume unatakiwa kutii ukigoma tu kivumbi kinaanzia hapo,
 
Diamond Elon mask , lily wine Newton , Ronaldo , Messi Michael Jackson na wengne wengi hawana na hawajawahi kuwa na ndoa na hawana mpngo wa ndoa , wanaume wengi hawapendi ndoa kwa sababu kwa sasa hazina faida kwa mwanaume, bali zinamlinda tu mwanamke tena kiukandamizaji bila haki kutendeka, mshana ww ni mtu wa zamani, tena makin mno ila umeshindwa kutambua mapungufu yaliyopo kwa watoto wenu wa kike hasa wa sasa wanapo kuwa wanahitaji ndoa, hawajua wanafuata nini kwenye ndoa zaidi wanataka tu wasionekane huko njee hawana ndoa, wakishapata ndoa wamepata utulivu wakupiga matukio yao huku wakijua mambo yao yakiharibika ndoa itamlinda atapata chochote kitu haturud nyumbani kwao kwa aibu., ukitaka wapnga ndoa watulie , waambie wanaume wenye ndoa wafungue nyuzi za kuonyesha mazuri wanatopata kwenye ndoa kwa idadi swa na mabaya na lawama tunazoona kwenye jukwaa la mapenzi.
 
Wanaume kama huyo rafiki yako ndo wanafanya ndoa zidharaulike mwanaume unaanzaje kuomba ruhusa kwa mwanamke pumbavu kabisa huyo rafiki yako.
Mwanaume anatakiwa aondoke na kurudi nyumbani muda wowote anao utaka
Nakazia.
 
Ndoa ni muunganiko kati ya mwanamume na mwanamke, walio amua kwa ridhaa yao wenyewe kuishi pamoja kama mke na mume mpaka mwisho wa maisha yao ya ndoa.

Aina za ndoa kwa mujibu wa sheria

Kuna aina mbili tu za ndoa zinazotambulika na sheria ya ndoa Tanzania

Ndoa ya mke mmoja na mume mmoja tu.
Ndoa ya wake wengi.
Ndoa hizo zinaweza kusheherekewa kufuatana na misingi na taratibu za kidini, kimila au kiserekali, kushuhudiwa na watu wasiopungua wawili na kusajiliwa kwa mujibu wa sheria.

Hatua za kuchukua kabla ya ndoa kufungwa

Lazima taarifa ya nia ya kufunga ndoa itolewe siku 21 kabla ya ndoa kufungwa, kama kutakuwa na mwenye pingamizi budi litolewe itoe kabla ya ndoa kufungwa
Majina ya wale wanaotarajia kufunga ndoa, umri, majina ya wazazi wao na mahali wanapoishi yatajwe.
Tamko kwamba wanaotarajia kufunga ndoa hawana uhusiano unaokatazwa kisheria kufunga ndoa
KUSAJILI NDOA

Ndoa inaweza kufungwa Kiserikali au kwa madhehebu ya Kikristo au Kiislam au kufuatana na mila na desturi za wale wanaofunga ndoa.

Msajili wa ndoa atatoa cheti cha ndoa. Kila Ndoa inapofungwa lazima iwe na mashahidi wawili

Mambo ambayo sheria ya ndoa inakataza katika suala zima la kuoa au kuolewa

Mwanamke na au mwanaume kuolewa/kuoa bila ridhaa yake mwenyewe
Mwanamke na mwanaume wenye undugu wa damu kuoana
Mwanamke na mwanaume kuoana kabla ya kutimiza umri unaoruhusiwa kisheria (kwa mwanaume miaka 18 na kwa mwanamke miaka 18 au 15 kwa idhini ya wazazi/mlezi wake)
Kuoana watu wa jinsia moja
Mwanamke na mwanaume kutaka kuoana kwa mkataba wa kipindi maalum.
Haki za mume na mke katika ndoa

Wote wana haki ya kumiliki mali kama nyumba, shamba n.k. kwa majina yao binafsi;
Wote wana haki ya kutoa idhini katika uuzaji au kwa pamoja kuweka dhamana mali yoyote ya familia;
Wote wana haki ya kuishi katika nyumba ya familia iwapo mume/mke amemkimbia;
Mke ana haki ya kupewa matunzo yake na ya watoto wakati wa ndoa au iwapo mume amemkimbia, wameachana kwa amri ya mahakama. Na mume ana haki ya kupewa matunzo iwapo ana ulemavu hawezi kujiingizia kipato kutokana na ulemavu au ugonjwa wake;
Wote wana haki ya kutokupigwa na au kufanyiwa ukatili wa aina yoyote;
Wote wana haki ya kupeana unyumba;
Wote wana haki ya kutumia mali ya ndoa;
Wote wana haki kuomba amri ya talaka.
Ukomo wa ndoa Ukomo wa ndoa uko wa aina mbili:

Kifo cha mwanandoa mmoja wapo
Talaka ambayo imetolewa na Mahakama pekee pale inapojiridhisha kwamba kuna sababu ya msingi kufanya hivyo.
Baraza la usuluhishi la Ndoa

Baraza la usuluhishi la Ndoa, ni baraza lililoanzisha na kifungu 102 cha Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, sura ya 29 kama sheria zilizopitiwa mwaka 2002, kwa madhumuni ya kusuluhisha wanandoa ambao wanaingia kwenye migogoro ya Ndoa. Kazi za Baraza la Usuluhishi la Ndoa:-

Kusuluhisha Wanandoa walioko kwenye Ndoa baada ya kupokea lalamiko toka kwa mmoja wapo wa Wanandoa
Kutoa hati maalum kuthibitisha kuwa suluhu imeshindikana na kuelekeza wanandoa kwenda Mahakamani kwa amri zaidi.
MUHIMU: Mahakama peke yake ndiyo ina mamlaka ya kutoa amri ya kutengana au talaka

Sababu zinazopelekea au kuishawishi mahakama kuvunja ndoa:-

Uzinzi kati ya wanandoa
Ukatili kati ya wanandoa au watoto wa ndoa
Dharau au kupuuza kulikokidhiri dhidi ya mwenzi
Kumtelekeza mwenzi kwa zaidi ya miaka mitatu Pale mwenzi anapofungwa kifungo cha maisha au kwa kipindi kisicho pungua miaka miaka mitano
Ikiwa mwenzi ameugua ugonjwa wa akili na imedhibitishwa na daktari kwamba hakuna uwezekano wa kupona.
Kubadili dini baada ya ndoa kufungwa pale wanandoa wote walikuwa wakifuata imani ya dini moja.
Haki za wanandoa zinazoambatana na amri ya talaka

Mgawanyo wa mali za ndoa /familia
Matunzo ya mke Hifadhi na matunzo ya watoto
Kizuizi cha kutobugudhiwa
Kuoa/Kuolewa tena
Fidia ya uzinzi
Gharama za kuendesha Shauri la Talaka
Haki ya Mgawanyo wa mali za familia/ ndoa Mali yoyote ambayo imepatikana wakati wa uhai wa ndoa na kwa nguvu na au machango wa pamoja wa wanandoa.

Iwapo mali iliyopatikana na mwanandoa mmoja wapo kabla ya ndoa au kwa nguvu zake mwenyewe lakini imeboresha/imetunzwa na mwanandoa mwingine mali hiyo itatambulika kama mali ya ndoa.

Lakini kama kuna mali yoyote ambayo mwanandoa mmoja amempa mwanandoa mwenzake kama zawadi, mali hiyo itakuwa ya yule aliyepewa pekee.

Aina za mchango

Kutekeleza kazi nyumbani hasa kutunza familia; mfano kuosha vyombo, kupika, kufua nguo, kubeba maji na kazi zingine zinazofanana na hizo kwa maslahi ya familia.

Kutunza mali za ndoa: mfano kufyeka, kulima, kuvuna shamba, kufanya marekebisho ya mali za ndoa kwa maslahi ya familia.

Mchango wa fedha wa mwanandoa katika kununua mali.

Haki ya Matunzo ya mwanandoa

Jukumu la kutoa matunzo kwa mke na watoto ni la mume, jukumu hilo litatekelezwa wakati wa uhai wa ndoa na baada ya talaka.

Haki ya Hifadhi na matunzo ya watoto

Hifadhi ya watoto hutolewa kwa mume au mke au mtu baki (mlezi) hasa kwa kuzingatia ustawi na maslahi ya wale watoto. Zaidi ya hayo, mahakama pia inaweza kuzingatia yafuatayo:

Umri wa wale watoto, mfano, watoto walio chini ya miaka saba kipaumbele cha hifadhi hupewa mama mzazi; labda kama kutakuwa na sababu za msingi za kuto fanya hivyo. Mfano kama mama mzazi ana matatizo ya kiakili, anaishi katika mazingira hatarishi.

Mazingira ya mahali watakapoishi watoto, mfano, kama mazingira ya upande mmoja ni hatarishi kwa ustawi wa mtoto, basi haki ya hifadhi atapewa mzazi mwingine bila kujali umri.

Matakwa ya wazazi wa mtoto nani kati yao angependa kupewa hifadhi ya watoto

Mila na desturi za jamii ambayo wanandoa wametokea.

Kama mtoto anaumri zaidi ya miaka saba na ana uelewa wa kutoa mapendekezo yake, basi matakwa/maoni yake yatasikilizwa zaidi.

Haki ya hifadhi ya mtoto haimnyimi mzazi mwenza haki ya kumuona na au kumtembelea mtoto/watoto. Haki ya hifadhi ya mtoto haiondowi jukumu la baba kutoa matunzo.
Tunacho kataa ni hicho kitendo mkuu , mababu zetu walikubali kufunga ndoa , kuna faida walizipata , mimi kijana wa sasa nitajie faida tano zenye maana nikifunga ndoa , heshima naipata nikiwa na pesa mingi na bado wanawake na wake za watu wanatka kuwa na mimi
 
Wanaopinga ndoa ni watoto wa masingle mother ,mtoto aliye lelewa na wazazi wake wawili hawezi kusema ndoa haina maana.
Kwa taarifa utakapo endelea kuhamasisha ndoa kwa kizazi cha sasa unahamisha watoto wa single mother waoane ,kwa sababu ulipo kwenye ndoa watoto wako ni watoto wa single mother watarajiwa kumbuka ya dr mwaka
 
Tunakataa ndoa kwa lengo la kupinga sheria kandamizi zilizopo kwenye ndoa , mwanamke akichepuka kwenye ndoa, ukivunja hyo ndoa mwanamke anapata faida ya mgawanyo wa Mali na mtoto anabaki kwa mama kma leseni ya tra lazima ulipie ushuru wa yeye kubaki na mtoto , fuatilia kisa cha dr mwaka huku jf hasa kwenye comments za wadada tu wa huku, ndo utajua kwa nini tunakataa ndoa tena kwa herufi kubwa KATAA NDOA kama ndoa ni mbususu tu mbona mbususu zipo kwa mafungu
 
Unaoa dunga embe unategemea nini ? Mwanamke amechakazwa na wanaume zaidi ya 20 halafu wewe unajipeleka kuoa!!
Oa bikra ufurahie mema ya nchi
Bikra wa bikra ipi mkuu kwa dunia ya sasa
 
Binafsi siungi kampeni ya kataa ndoa,kwasababu ninaamini familia bora lazima iwe ya baba na mama,

ila hizo sababu ulizoziandika hapo juu itakuwa ni mtazamo wako tu,maana haujaandika kwa kuchambua kwa kina,umeandika kiushabiki ule wa simba na yanga,tegemea wapingaji wengi kwenye huu uzi wako tena kwa hoja za uzito,

kama kweli ulikuwa na nia ya kuwaelimisha watu kuhusu umuhimu wa ndoa hukupaswa kuandika kimipasho hivo kwa kutegemea uungwaji mkono kwa member wengi ambao wanaunga mkono kuhusu ndoa,

ulipaswa uelezee umuhimu na faida za kuwa kwenye ndoa pia ungeelezea hasara ya kutokuwa na ndoa
Hii ni mada ya tano ama ya sita naandika kuhusu ndoa.. Na muktadha ulikuwa kuyataja makundi na si kufanya uchambuzi wa faida na hasara za ndoa.. Kama ungezingatia kichwa cha habari usingeandika haya
 
Walio kwenye ndoa wanatamani kutoka, ndoa haina kitu cha ziada zaidi ya ngono. Nje ya ngono ni stress tupu, mifano tunayo mingi tu ( Manara, Dr.Mwaka n.k)
#KATAANDOA #NDOANIUTAPELI
Wanaotamani kutoka ni waliokosea kuoa ama kupata wenza sahihi
 
Couples ambazo zinaishi pamoja unazitofautishaje na mfumo wa ndoa?

Au tuseme ndoa ni kile kiapo?
Kiapo ni nyaraka za kisheria tu na hapa nfio tunapokosea kuhusu ndoa japo iko kwenye uchambuzi mrefu hapo juu
 
Huu ni uzi wa waliooa kufarijiana maana si kwa stress walizonazo[emoji1787]
Pambaneni na mdoa zenu, hakuna aliyewalazimisha kukimbilia ndoa.
#KATAANDOA
Katikati hali ya ujana wengi watakubaliana na wewe
 
Nafkiri umelenga kuwaumiza kihisia ama naweza sema umeamua "kujibu mapigo" maana hoja zao ni kama haujazijibu kabisa.
Ni kawaida sana kwa Binti kuonywa kuwaepuka wanaume kwamba wanaweza haribu maisha yake na hii imefanywa na jinsia zote kwa Miaka mingi lakini kwa Vijana wa kiume hali hua ni tofauti.
Hii kampeni ya Vijana kukataa ndoa haimaanishi wanaogopa mwanamke au majukumu.. wanahofia madhara yanayotokana na "Ndoa rasmi". Sheria za Ndoa zinambana Mwanamume na kumpendelea Mwanamke bila sababu za kueleweka. Na hii inafanya wanawake kutumia mwanya huu kuwafanyia ukatili Wanaume.. huenda Sheria na taratibu zikiwa updated Kampeni kama hizi hazitosikika.. Vijana wa kiume wana haki ya kujilinda kama wenzao.. usiwe ambassador wa Harmful masculinity Amigo. Change is inevitable
Muktadha wa mada ulikuwa kutaja makundi na si vinginevyo[emoji1545]
 
Kuna mshkaji wangu mmoja tulikuwa tunakaa naye vikao mara kwa mara, sasa majuzikati kajichanganya akaoa! Hivi sasa kila weekend lazima aje kwangu anipe sim niongee na mke wake nimuombee ruhusa!!!
Nimemwambia weekend hii ndo mwisho atafute njia nyingine ya kutoka kwake au atulie na familia yake aenjoy (kama mnavyodanganyana) maana ndo maisha aliyochagua.
Usio kwa kukurupuka
Usioe kama hujajiandaa kuishi maisha ya ndoa
Usioe kama bado una maisha ya kwenda vijiwweni utaona ndoa ni chungu na utateseka sana
Halafu ndoa ni ya wawili ishu ya kumpa mshkaji simu aongee na mkeo sio ukomavu wa akili ni kutojiamini na ku expose maisha binafsi kwa wengine
 
Back
Top Bottom