Habari Wakuu!
Bila kupoteza wakati.
1. Unamwomba mpenzi/ Mkeo Ngono.
Ukiona Mkeo au mpenzi wako anakupimia michezo ya kitandani na wewe unamwomba ujue wewe ni mwanaume uliyekata tamaa, usiye na lolote la maana, uliyekwisha. Mwanaume dhaifu.
2. Unatumia nguvu kubwa hasa ya pesa kumhudumia ili huyo mwanamke abaki na wewe.
Hiyo ni dalili kuu nyingine inayoonyesha kuwa wewe huna lolote la Maana, mwanaume dhaifu na uliyekata tamaa.
Mwanamke ndiye anatakiwa atumie nguvu kubwa kuwa na kubaki na wewe na sio wewe umeng'ang'ania.
3. Unaogopa Kumpoteza au unaogopa kuachana naye.
Ukitaka ujue kuwa wewe ni mwanaume wa aina gani, Moja ya vipimo katika Mzani wa kisaikolojia ni pamoja na kuogopa kumpoteza au kuachana na mwanamke.
Mwanaume dhaifu na asiye na lolote huogopa kuachana na mwanamke.
Mwanaume kamili na Halisi haogopi kuachana na mwanamke na wanawake hujua waziwazi wanapokuwa mbele ya wanaume waaina hiyo.
Mwanaume dhaifu hutishiwa na mwanamke kuachana nao huteseka Sana lakini kosa Hilo mwanamke hawezi kujaribu kulifanya kwa kumtishia mwanaume Kamili kuwa atamuacha hata kwa utani kwa Sababu wanawake hujua maamuzi ya wanaume Halisi yakoje.
4. Mwanamke kukukosea heshima, kukufokea na mwanaume anakuwa Hana chakufanya.
Hiyo ni dalili kuwa wewe ni weak man,usiye na mbele Wala nyuma, uliyekata tamaa.
Mwanamke anajiamulia mambo, anondoka bila kibali Wala ruhusa yako, anarudi atakavyo, na wewe huna chakufanya. Wewe ni mwanaume dhaifu.
5. Anakuwekea Sheria na standards zake ALAFU wewe unafuata.
Wanaume dhaifu na waliokata tamaa na wasio na MBELE Wala Nyuma ndio huwekewa Sheria na standards na Wanawake na wao hufuata.
Wanaume dhaifu ni wafuasi wa Wanawake. Hufuata matakwa ya Wanawake.
Ni wanaume waliojidharau na waliodharaulika.
Mfano, mwanamke anakuambia bila pesa au bila kumpa kitu Fulani huwezi kuwa naye au hakupi papuchi nawe kama mbuzi unafuata Sheria na standards zake. Ingawaje kisaikolojia wanaume dhaifu ni emotional entity, na hawawezi kujidhibiti hisia Zao za ngono.
6. Unashindwa kufanya maamuzi Mpaka umuulize.
Yaani yeye ndiye anakuwa kama mwanaume wewe unakuwa Demu. Kila kitu Mpaka umuulize sasa Nani mwanaume hapo. Mwanaume Kamili hayupo hivyo.
7. Muda wote unamfikiria Yeye.
Kwanza huo ni utoto na ulimbukeni. Unashindwa kufanya mambo ya msingi Muda wote unamuwaza yeye.
8. Unapigana na watu na kuzuia watu wasiongee naye huko mabarabarani.
Unaogopa kuachwa.
Unawivu wa kijinga. Unagombana na watu Kisa mwanamke. Unamchunga mtu uliyemuambia akikucheat ataondoka hivi uko Sawa kichwani?
Mwanaume Kamili hayupo hivyo.
9. Anakusaliti na umemfumania na bado unamsamehe mnaendelea kuishi wote.
Wewe ni mwanaume dhaifu, uliyeshindwa kila kitu, usiyejiamini.
Mwanaume Kamili na anayejiamini hata siku Moja hawezi kuishi na mwanamke msaliti hata kwa namna yoyote hata angeambiwa asiende Mbinguni yupo tayari kwa Hilo.
Vijana, mapenzi huwaumiza zaidi wanaume dhaifu kwa Sababu kiasili wanaume dhaifu hawanaga Akili, huendeshwa na Mihemko, na hisia, hushindwa kudhibiti hisia na Mihemko Yao. Hawajui wao ni wanaume hivyo ni kusema hawajitambui.
Na mwanaume asiyejitambua ni Weakman na finished Man.
Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam