Mambo Makuu yanayoonyesha kuwa wewe ni mwanaume dhaifu na uliyekata tamaa

Mambo Makuu yanayoonyesha kuwa wewe ni mwanaume dhaifu na uliyekata tamaa

Nyie ndio mnazaa hovyo mtaani na kutelekeza watoto, Mmekengeuka Watibeli gani nyie wa hovyo

Hatutelekezi watoto Watibeli
Lakini hiyo haimaanishi tutang'ang'ania watoto kwa Wanawake tuliozaa nao
Au hatuwezi kung'ang'ania mtoto ambaye hatutaki never ever
 
Hata siku moja usikubali kuishi na mwanamke mpumbavu kisa watoto!

Watoto hawawezi kuwa wa mhimu kuzidi WEWE.

Unaakili Sana
Kama huyo mwanamke ataona umuhimu wa watoto kuwa na maadili na ndoa ni muhimu lazima awe mtiifu na Mke Bora full stop
 
Na Siku zote wanawake wanaposema kuwa wewe ni MME Bora , sijui baba Bora wa watoto inamaanisha anauwezo wakukutawala..mwanaume halisi lazima mwanamke akuite mbwa..!!wanawake wakishindwa kukutawala unakuwa tishio kwao..hacha waje tuvaaneView attachment 3282173
Actually umeongea kinyume chake siku zote wanaume wakishindwa kuwatawala wanawake ndio huwaona kama tishio, wanawake wanachotaka ni kujitawala wenyewe wamechoka kutawaliwa kwa sababu za kipuuzi, hiyo inferiority complex yenu ndio inafanya muone kama wao kukataa kutawaliwa basi maana yake wanataka kuwatawala
 
Unajifanya kungwi
Nakumbuka kuna father mmoja alikimbiwa na mke wake for 4 years 97-2001 kule kaenda kadhaa watoto wawili, baadae kurudi kwa mme wake wa kadhaa watoto watatu. Hadi leo wako pamoja
Huyo sasa ndio Mwanaume aliyejikatia tamaa, Hohe hahe hata kichwani hana kitu
 
Habari Wakuu!

Bila kupoteza wakati.

1. Unamwomba mpenzi/ Mkeo Ngono.
Ukiona Mkeo au mpenzi wako anakupimia michezo ya kitandani na wewe unamwomba ujue wewe ni mwanaume uliyekata tamaa, usiye na lolote la maana, uliyekwisha. Mwanaume dhaifu.

2. Unatumia nguvu kubwa hasa ya pesa kumhudumia ili huyo mwanamke abaki na wewe.
Hiyo ni dalili kuu nyingine inayoonyesha kuwa wewe huna lolote la Maana, mwanaume dhaifu na uliyekata tamaa.
Mwanamke ndiye anatakiwa atumie nguvu kubwa kuwa na kubaki na wewe na sio wewe umeng'ang'ania.

3. Unaogopa Kumpoteza au unaogopa kuachana naye.
Ukitaka ujue kuwa wewe ni mwanaume wa aina gani, Moja ya vipimo katika Mzani wa kisaikolojia ni pamoja na kuogopa kumpoteza au kuachana na mwanamke.

Mwanaume dhaifu na asiye na lolote huogopa kuachana na mwanamke.

Mwanaume kamili na Halisi haogopi kuachana na mwanamke na wanawake hujua waziwazi wanapokuwa mbele ya wanaume waaina hiyo.

Mwanaume dhaifu hutishiwa na mwanamke kuachana nao huteseka Sana lakini kosa Hilo mwanamke hawezi kujaribu kulifanya kwa kumtishia mwanaume Kamili kuwa atamuacha hata kwa utani kwa Sababu wanawake hujua maamuzi ya wanaume Halisi yakoje.

4. Mwanamke kukukosea heshima, kukufokea na mwanaume anakuwa Hana chakufanya.
Hiyo ni dalili kuwa wewe ni weak man,usiye na mbele Wala nyuma, uliyekata tamaa.

Mwanamke anajiamulia mambo, anondoka bila kibali Wala ruhusa yako, anarudi atakavyo, na wewe huna chakufanya. Wewe ni mwanaume dhaifu.

5. Anakuwekea Sheria na standards zake ALAFU wewe unafuata.
Wanaume dhaifu na waliokata tamaa na wasio na MBELE Wala Nyuma ndio huwekewa Sheria na standards na Wanawake na wao hufuata.

Wanaume dhaifu ni wafuasi wa Wanawake. Hufuata matakwa ya Wanawake.
Ni wanaume waliojidharau na waliodharaulika.

Mfano, mwanamke anakuambia bila pesa au bila kumpa kitu Fulani huwezi kuwa naye au hakupi papuchi nawe kama mbuzi unafuata Sheria na standards zake. Ingawaje kisaikolojia wanaume dhaifu ni emotional entity, na hawawezi kujidhibiti hisia Zao za ngono.

6. Unashindwa kufanya maamuzi Mpaka umuulize.
Yaani yeye ndiye anakuwa kama mwanaume wewe unakuwa Demu. Kila kitu Mpaka umuulize sasa Nani mwanaume hapo. Mwanaume Kamili hayupo hivyo.

7. Muda wote unamfikiria Yeye.
Kwanza huo ni utoto na ulimbukeni. Unashindwa kufanya mambo ya msingi Muda wote unamuwaza yeye.

8. Unapigana na watu na kuzuia watu wasiongee naye huko mabarabarani.
Unaogopa kuachwa.

Unawivu wa kijinga. Unagombana na watu Kisa mwanamke. Unamchunga mtu uliyemuambia akikucheat ataondoka hivi uko Sawa kichwani?
Mwanaume Kamili hayupo hivyo.

9. Anakusaliti na umemfumania na bado unamsamehe mnaendelea kuishi wote.
Wewe ni mwanaume dhaifu, uliyeshindwa kila kitu, usiyejiamini.

Mwanaume Kamili na anayejiamini hata siku Moja hawezi kuishi na mwanamke msaliti hata kwa namna yoyote hata angeambiwa asiende Mbinguni yupo tayari kwa Hilo.

Vijana, mapenzi huwaumiza zaidi wanaume dhaifu kwa Sababu kiasili wanaume dhaifu hawanaga Akili, huendeshwa na Mihemko, na hisia, hushindwa kudhibiti hisia na Mihemko Yao. Hawajui wao ni wanaume hivyo ni kusema hawajitambui.

Na mwanaume asiyejitambua ni Weakman na finished Man.

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam

Nafikiri ukiwa na watoto kuanzia 2 na mwanamke, mliye na ndoa, na unaishi naye, kutokuwa na ujasiri na kujaribu kuisitiri ndoa yako kwa kiwango fulani, ni maturity na sio udhaifu, Kuwa considerate pia ni strength, mambo hayako straight hivyo!

Kwani una umri gani Mkuu?
 
Mnatelekeza kwa kushindwa majukum huku mnajibanza kwenye umwamba usio na tija

Nafikiri protocol za utawala zinakupiga chenga Mkuu. Na IPO hivyo kwa Wanaume wengi dhaifu.

Baba anajukumu la kulinda watoto wake. Zingatia neno watoto wake.
Kuwatunza, kuwalea na kuwahudumia.

Lakini kamwe kiutawala Baba huyohuyo hawezi kufanya wajibu huo kwa watoto wake wakuwazaa walioasi au walioungana na Muasi ili kumuangamiza yeye au kuvunja heshima na Mamlaka ya Baba.

Hata serikali IPO hivyo
Hata kwenye Dini tumesoma hivyo kwa Yule aitwaye Mungu Baba. Hiyo ni protocol za kimamlaka na kiutawala
 
Mtibeli

Mwanamke yupo loyal 100% kwa kiumbe mmoja tu ambaye ni mtoto wake.

Kwa hiyo mwanamke anaweza kuwa mke malaya kwako Ila akawa ni mama bora kwa watoto wako. The same way, mwanaume anaweza asiwe mume bora yani mlevi, mzinzi na hajali hisia za mwanamke Ila kwenye kuangalia watoto wake akawa perfect.

Na kumbuka Hapa sizungumzii ule ushwetani wa wazi wa kuwaongoza watoto vibaya. Ila nazungumzia madhaifu ya kila siku ambayo wazee wetu waliyaficha chumbani ili kuwapa watoto malezi ya baba na mama wanayostahili.

Kama hujawahi kuishi na mama wa kambo, single parent au ukatelekezwa kwa ndugu baada ya familia kuvunjika. Pengine unaweza usielewe uzito wa hili kwa kuchukulia malezi ni chakula na mavazi Ila kama ulionja joto la jise. Utawaelewa hao wazee na wamama kwa sacrifise walizozitoa kwa ajili ya watoto wao
Mimi ninaamini katika mitara na sio kuachana,toa competition pale unapoona ameshiba nankukinai!Hali ya kushiba na kukinai mwisho dharau inawapata sana wanawake hasa mambo yakiwa sawa au wakishafikisha malengo Yao ndani ya ndoa!!

Mwanamke yeyote ni msaliti au mhaini in nature was utawala wa mume ni muda TU ndio utaamua!akishatimiza malengo TU atataka kujitawala na ukiona mwanamke anakutii Santa ujue malengo hayajatimia yakitimia ataanza kukaidi pole pole maagizo Yako hata kama ukimuacha ndio atashangilia kuachwa!!

Tawala ndani ya familia zimegawanyika kutokana na nyakati 1.Mume 2.mama 3.watoto!

Mume ataanza kutawala Kwa muda mrefu coz yeye ndio mtoa mkate!

Mke ataanza kutawala baada ya mine kupoteza ushawishi sababu ya uzee au kastaafu KAZI au kishatimiza wajibu wake na kuonekana Hana maana au hahitajiki tena!

Refer Suleiman kova na kikwete !kikwete anasema "Ruge(Mmiliki was clouds fm) alikua loyal kwake kabla na baada ya uongozi wake"

Kova anasema"Baada ya kustaafu hata marafiki na juniors hawaiisikilizi tena"

Kwahiyo zipo zama za baba kupoteza ushawishi na kuonekana mzigo Kwa mama na watoto!hata kama ulifanya Nini Cha maana!!

Utawala wa watoto huanza baada ya baba na mama kupoteza ushawishi!itategemea upendo ambao mliwafunza wakati mnawalea!!
 
Mwanaume Automatic unatakiwa upewe heshima yako bila kujari una pesa au huna una kazi au hauna.

Acha wa kudharau huko mtaani ila nyumbani heshima yako ibaki palepale.

Ukikoswa msimamo ni sawa na kukoswa Dira yaani umekuwa bendera. Mwanamke kukupangia ratiba za kumtoa out yeye ni moja ya dalili kubwa sana kuwa yeye ndo kashika remote ya kichwa chako.

Daima mwanaume mambo ya kumfurahisha mkeo au mwanamke yyte yafanyike kama surprise tu awe amejiandaa au hajajiandaa akisema umemshitukiza piga chini mwambie haya wakati mwingine....

Inakuwaje mwanamke akuambie umfanyie Happy birthday yake alike na marafiki zake nawewe ukubalu kirahisi eti usipofany vile badi itaonekana humpendi!!

Mwanaume acha ujinga bana ninyi ndo mnatufanya wanaume halisi tuonekane sisi ni wakoloni kwa sababu ya upuuzi wenu.

Stage ya mwanamke kukufananisha na wanaume wa shost zake basi jua your useless man. Mwanaume ukifikia stage mkeo anasema jamani wewe ni baba bora ni mwanaume makini najivunia kuwa nawewe jutathimini sana kuna sehemu umepwaya. Mwanaume kamili hatabiriki kama ni wabaridi au wa moto kuna muda anakuwa wa vuguvugu au moto kabisaa akipoa kuwa bardi haichukui muda tena sensor Zina change.....
 
Nafikiri ukiwa na watoto kuanzia 2 na mwanamke, mliye na ndoa, na unaishi naye, kutokuwa na ujasiri na kujaribu kuisitiri ndoa yako kwa kiwango fulani, ni maturity na sio udhaifu, Kuwa considerate pia ni strength, mambo hayako straight hivyo!

Kwani una umri gani Mkuu?

Mkuu mwanamke anakukosea heshima unyamaze Kisa ndoa. Hiyo kwa Sisi Watibeli haipo Mkuu.

Familia IMARA inajengwa kwa Baba kuwa IMARA na Jasiri na mwenye uwezo wa kufanya Maamuzi magumu kwa Maslahi ya kizazi chake.

Hata ukiwa na watoto sita na mke Mmoja lazima kama Baba ujue namna ya kushughulikia matatizo ya familia kwa namna sahihi ili watoto na kizazi chako kijifunze.

Ukinyamaza kama Baba unakuwa Weakman na hiyo itafundisha watoto kuwa dhaifu.
Watoto wakiume watafanyiwa dharua na ujinga na wake Zao na wataona ni Jambo la kawaida kumbe wanadhalilika.

Binti zako nao watawapelekesha waume Zao kama wewe Baba Yao ulivyopelekeshwa na mama Yao. Wataona ni Jambo la kawaida

Ndio maana Sisi Watibeli tukienda kuoa Jambo la Kwanza lazima tuangalie Mama Mkwe ni mtu WA Aina gani kisha Baba Mkwe alikuwa mtu wa namna gani.

Hatuwezi kuoa kwenye familia ambayo Baba alikuwa Dhaifu. Tunajua Baba dhaifu hawezi kumlea binti yake akawa Mke Bora.
 
Mwanaume Automatic unatakiwa upewe heshima yako bila kujari una pesa au huna una kazi au hauna.

Acha wa kudharau huko mtaani ila nyumbani heshima yako ibaki palepale.

Ukikoswa msimamo ni sawa na kukoswa Dira yaani umekuwa bendera. Mwanamke kukupangia ratiba za kumtoa out yeye ni moja ya dalili kubwa sana kuwa yeye ndo kashika remote ya kichwa chako.

Daima mwanaume mambo ya kumfurahisha mkeo au mwanamke yyte yafanyike kama surprise tu awe amejiandaa au hajajiandaa akisema umemshitukiza piga chini mwambie haya wakati mwingine....

Inakuwaje mwanamke akuambie umfanyie Happy birthday yake alike na marafiki zake nawewe ukubalu kirahisi eti usipofany vile badi itaonekana humpendi!!

Mwanaume acha ujinga bana ninyi ndo mnatufanya wanaume halisi tuonekane sisi ni wakoloni kwa sababu ya upuuzi wenu.

Stage ya mwanamke kukufananisha na wanaume wa shost zake basi jua your useless man. Mwanaume ukifikia stage mkeo anasema jamani wewe ni baba bora ni mwanaume makini najivunia kuwa nawewe jutathimini sana kuna sehemu umepwaya. Mwanaume kamili hatabiriki kama ni wabaridi au wa moto kuna muda anakuwa wa vuguvugu au moto kabisaa akipoa kuwa bardi haichukui muda tena sensor Zina change.....
Haya Bwana,wale wakubeba watoto na kuwaogesha wasemeje?
 
Haya Bwana,wale wakubeba watoto na kuwaogesha wasemeje?

Baba kumwogesha mtoto au kumbeba mtoto wake aliyemzaa sio tatizo MKUU.
Hapa tunazungumzia heshima ya Mwanaume, Nafasi ya Mwanaume na majukumu yake.

Sio mtoto tuu hata Mke unaweza kumuogesha
Nafikiri kuna sehemu tunapishana
 
Back
Top Bottom