Mambo Mengi muda mchache, kijana aende wapi kati ya diploma ya CLINICAL MEDICINE NA PHARMACY

Mwambie aende Clinical Medicine, coz clinical medicine kwa uelewa wangu anaweza fanya pharmacy pia ila pharmacy hawezi kazi za clinical medicine

Nani alikudanganya ?? Clnical officer haruhusiwi kufanya kazi za Pharm.tech and vice versa is true.
 
Bado nakueleza kuwa CO bado ni wachache kulinganisha na Pharmacy. Hii inatokana na kuwa vijana wengi wanafeli Physics kwani Co inahitaji Physics. Changamsha ubongo kidogo uone kuwa Co ni superior ya hizo kozi.

Nakupa mfano, watu hao wanne wawe nyumbani kwao. Nani atafuatwa kama kuna mgojwa nyumbani. Je, atafuatwa CO au Nurse, au Pharmacist au Lab Tech? Atafuatwa mtu anayeitwa mganga. Na sasa ambapo upimaji ni kutumia Rapid Test, Co anamaliza kila kitu, huhitaji Lab tech. Nyie ndiyo mnadanganya watu kuwa CO imejaa, je wagonjwa wameisha?

Tuangalie Lab Tech, je kwa siku anaona wagonjwa wangapi? Hivi zahanati za vijijini wanahitajika? Technology inawatupa nje na haya ma Urine Analysers etc Niachie hapo, mtu kama alipata angalau D ya Physics atakuwa ni mpuuzi asipojiunga na CMT
Mkuu kufalu physics sio kwamba lazima usome C.O wengine hawapo interested na kusoma C.O na pia sio kila ambaye ajasoma C.O akufaulu physics.
 
Acha tamaa,famasi nayo inamaketi sana usiangalie serikalini tu,mie nina dada yangu anacheti cha famasi aliajiriwaga kariakoo uko kwa wahindi,baada ya muda akaacha kazi akafungua duka lake la famasi kiukweli anasema hajutii kusomea iyo kazi,kaajiri watu wengine yeye sasaivi anamishe zingine.........So mie naamini tu hakuna kitu kisicholipa maishani ni kuwa na subira tu na icho unachokifanya........ama mfano mwingine huu kuna jamaa alimazaga six kipindi kile cha kikwete mwishoni mwishoni alipataga 1 tena Pcm akaona ujinga kusomea uinginia,akaenda kusomea mambo ya Petrolium and gas baada ya kusikia serikali inaingia kwenye sekta iyo......sasaivi yupo tu kitaa so wewe ukitaka kusomea kitu somea kile kilichopo damuni mwako,kwa sie waislamu tuna kitu tunatakiwa kufanya katika kuchagua mambo,so na mungu pia ananafasi katika kukuchagulia cha kusomea
Kweli mkuu nimekuelewa ngoja tuone mbeleni hapo maana nasikia pharmacy ukisoma ufi njaaa
 
Kwa maana hiyo bora niachane na mapharmacy nipige hiyo medical lab technology mkuu maana naona kama serikali hawana habari na mambo ya pharmacy kabisa
Soma kitu unachokipenda. Nyakati hubadilika
 
Mkuu kufalu physics sio kwamba lazima usome C.O wengine hawapo interested na kusoma C.O na pia sio kila ambaye ajasoma C.O akufaulu physics.
Nimeelewa naongea na mtu gani. Kwani kitendo cha kutojua H kinanionesha kumbe najiangusha. Hajasoma na Hakufaulu. Kwaheri
 
Njia panda! Nisaidieni aende wapi , with reason.
Vyote ni vyuo vya serikali amechaguliwa.
Swali Kati ya hizo kozi,ipi inakuvutia kiasi kwamba usipoifanyia kazi maisha yako yatakosa furaha,mfano Mimi napenda uhandisi,engineering,siwezi kuishi bila kufanya engineering,hata nikipewa kazi nyingine mfano udereva na nilipwe mara Tano,nitafanya lakini Kuna kitu kitakuwa kinamisi kwenye maisha yangu,kwangu uhandisi ni passion,ni wito wangu,
Am wired to do engineering,wewe upoje,jiulize kutoka moyoni,
 
Ndo mawazo yako hayo....Mimi nimehitimu hiyo kozi 2019 tena chuo cha serikali na nikiwa na ufaulu mzuri tu mzee baba.
Huelewi unachokisema au ulifeli Physics kwa hiyo unawaonea gere waliofaulu
 
Nimeelewa naongea na mtu gani. Kwani kitendo cha kutojua H kinanionesha kumbe najiangusha. Hajasoma na Hakufaulu. Kwaheri
Mkuu ishu hapa sio kukosoa lugha bali kueleweshana tu basi umeshinda mkuu
 
Ndo mawazo yako hayo....Mimi nimehitimu hiyo kozi 2019 tena chuo cha serikali na nikiwa na ufaulu mzuri tu mzee baba.
Ni ujinga kusema umehitimu chuo cha serikali wakati mtihani hata wa Private wanafanya huo huo. Kama ulifaulu vizuri mwaka 2019 kwanini hujachukua MD. Inaonesha hukuwa na first class bwashee
 
Mzee kwa GPA ya 3.9 ninavyo vigezo vya kusoma...ila ushindani mkubwa sana siku hizi na private sina huo uwezo.Aliyesoma C.O serikalini na aliyesoma Private kuna utofauti japo mitihani ile ile hasa mitihani ya ndani hubebwa sana ndo maana hata GPA zao zao ni balaa lakini bado ukitaka kwenda MD tuliopita C.O chance ipo ndogo mno.

Nakiri wazi hapa C.O ni mkubwa kwa wote hao kielimu kwa ngazi hiyo hasa kwani anafanya vitu karibu vyote wanavyofanya wengine..ila nimejaribu kuangalia market kwa sasa C.O ipo chini japo utasavaivu kitaa kimtindo na kama huna pesa ya kujiendeleza huko mbele ni gumu kusoma digrii kutokana na ushindani now kila mtu anataka kua tabibu au daktari hivyo namba kubwa.

Mtoa mada jaribu kuchungulia na huku pako poa na hatojuta huyo ndugu yako iwapo tu kama ana vigezo.
1.Radiology
2.Dental
3.Medical lab

Hasa hiyo 1&2 ziangalie kwa jicho la 3 ziko poa na kujiendeleza hakuna ushindani mkubwa.
Ni ujinga kusema umehitimu chuo cha serikali wakati mtihani hata wa Private wanafanya huo huo. Kama ulifaulu vizuri mwaka 2019 kwanini hujachukua MD. Inaonesha hukuwa na first class bwashee
 
Bado nakueleza kuwa CO bado ni wachache kulinganisha na Pharmacy. Hii inatokana na kuwa vijana wengi wanafeli Physics kwani Co inahitaji Physics. Changamsha ubongo kidogo uone kuwa Co ni superior ya hizo kozi.

Nakupa mfano, watu hao wanne wawe nyumbani kwao. Nani atafuatwa kama kuna mgojwa nyumbani. Je, atafuatwa CO au Nurse, au Pharmacist au Lab Tech? Atafuatwa mtu anayeitwa mganga. Na sasa ambapo upimaji ni kutumia Rapid Test, Co anamaliza kila kitu, huhitaji Lab tech. Nyie ndiyo mnadanganya watu kuwa CO imejaa, je wagonjwa wameisha?

Tuangalie Lab Tech, je kwa siku anaona wagonjwa wangapi? Hivi zahanati za vijijini wanahitajika? Technology inawatupa nje na haya ma Urine Analysers etc Niachie hapo, mtu kama alipata angalau D ya Physics atakuwa ni mpuuzi asipojiunga na CMT
Hujui unachoandika wewe watu wa nyumbani hawana habari hata na hao maCO wanachojua wao ni DLDM tu..........pale wanapoumwa.

Pili.......kozi nzuri kwa nchi yetu kwa sasa ni ile ambayo unaweza kuajiriwa wakati huo unaweza kujiajiri kiwepesi......sasa wewe kasome hiyo CO uje kusugua gaga na wenzako huku mtaani na walivyowengi kama kumbikumbi.

Tatu......hakuna CO anayeweza kumaliza issue ya kumhudumia mgonjwa bila kuwepo watu wa lab, nurse na pharmacist labda kama huyo CO ni mganga wa kienyeji.....ko usijidaganye kwamba CO anaweza kufanya kazi za hao watu.....never.

Note....diploma za lab na nurse physics ni lazima ili usome......maana naona physics ndo imekuwa point yako kubwa na umeing'ang'ania kweli kuidefense hiyo CO.....ahaaaa.

Kama huna mtaji wa kituo cha afya ambacho pia kitahitaji watu wa lab,nurses,pharmacist.....achana na CO........UTANISHUKURU.

ASANTE.
 
Nakupinga hapo kwenye C.O kufanya kazi za Lab na Pharmacy,Nurse

Tuliopokua mwaka wa kwanza semista ya kwanza tulifundishwa Microbiology na tulisoma vimelea vya magonjwa sifa zao na jinsi wanavyoleta magonjwa,semista ya pili tulisoma Clinical Laboratory hapa tukafundishwa jinsi ya kuchukua vipimo na kupima vipimo mbali mbali theory na Maabara japo si deep kama mtu wa Lab ila C.O aliyeiva anajua kupima na kufanya kazi karibu zote za Maabara zile basic.

Mwaka wa kwanza semista ya pili tulisoma Patient care hili somo tulijifunza jinsi ya kumuhudumia mgonjwa kama nesi afanyavyo japo wao wapo deep kwenye hilo.

Mwaka wa pili semista ya kwanza tulisoma Pharmacology na Pharmacy ..hapa tulifundishwa madawa yote makundi yao,sifa na jinsi zinavyofanya kazi(japo sio deep kama mtu wa pharmacy) hivyo C.O aliyeiva anajua dawa zinavyofanya kazi,makundi mbalimbali na magonjwa yanayotibu bila kusahau side effect hatukusoma tu jinsi ya kutenegeneza.

So C.O anaweza kufanya mambo mengi wayafanyayo hao wote na ili uwe tabibu lazima ujue kuchukua history,kudiagnose,kupima,kutibu(pamoja na kuandika na kutoa dawa) bila kusahau kumuhudimia mgonjwa...C.O yeye ni full package ya hao wote na hao wengine wao hubobea kwenye sehemu moja kumsaidia tabibu au daktari.

Binafsi naona kijana aende pharmacy kwanini kwa sababu
pharmacy ni kozi yenye mwanya mpana sana katika kujiajiri mfano unaweza kufungua duka la dawa baridi kwa ganzi ya diploma pia ukiwa na degree utapiga pesa sana hasa ukifungua pharmacy au hata labaratory pharmacy kam ile ya laicent medical industry katika ushalishaji dawa na vifaa tiba lakin pia diploma kwenda Bpharm ni rahisi zaidi kuliko CO to MD kwa sababu ya ushindani pia kama ukiajiriwa kwenye vituo vya afya mafamasia wanaitajika sana kuliko hata ma clinical unaweza uka kuta zahanati ya kijiji ma co wako wawili lakin mafamasi ni zaidi ya +
yote kwa yote good luck.
 
Kitu hujui acha, nani kakataza mtu wa GPA 3.5 asisome MD?
iv mkuu umesoma mwaka gani??... anyway acha ubishi mambo yamebadilik C.O usipokua na GPA ya 4+ na kwen kusipokua na ela za kutosh basi maish yako ndo yameishia hapo
 
  • Thanks
Reactions: p2k
Nakupinga hapo kwenye C.O kufanya kazi za Lab na Pharmacy,Nurse

Tuliopokua mwaka wa kwanza semista ya kwanza tulifundishwa Microbiology na tulisoma vimelea vya magonjwa sifa zao na jinsi wanavyoleta magonjwa,semista ya pili tulisoma Clinical Laboratory hapa tukafundishwa jinsi ya kuchukua vipimo na kupima vipimo mbali mbali theory na Maabara japo si deep kama mtu wa Lab ila C.O aliyeiva anajua kupima na kufanya kazi karibu zote za Maabara zile basic.

Mwaka wa kwanza semista ya pili tulisoma Patient care hili somo tulijifunza jinsi ya kumuhudumia mgonjwa kama nesi afanyavyo japo wao wapo deep kwenye hilo.

Mwaka wa pili semista ya kwanza tulisoma Pharmacology na Pharmacy ..hapa tulifundishwa madawa yote makundi yao,sifa na jinsi zinavyofanya kazi(japo sio deep kama mtu wa pharmacy) hivyo C.O aliyeiva anajua dawa zinavyofanya kazi,makundi mbalimbali na magonjwa yanayotibu bila kusahau side effect hatukusoma tu jinsi ya kutenegeneza.

So C.O anaweza kufanya mambo mengi wayafanyayo hao wote na ili uwe tabibu lazima ujue kuchukua history,kudiagnose,kupima,kutibu(pamoja na kuandika na kutoa dawa) bila kusahau kumuhudimia mgonjwa...C.O yeye ni full package ya hao wote na hao wengine wao hubobea kwenye sehemu moja kumsaidia tabibu au daktari.
Kutibu mgonjwa wala hakuhitaji hizo basics kijana ndo maana kuna hao watu wanasoma three(3) years kitu ambacho wewe umesoma miezi mitatu tena na vipindi vingine ulidoji........ahaaa......kutibu mgonjwa kungekuwa kunahitaji hiyo miezi yako mitatu basi serikali na wizara ya afya ingefuta hizo kozi zingine then ingebana bajeti......ahaaa

Pili......umesoma hizo basics unazosema kukurahisishia wewe kumganga mgonjwa tu.....na sio kufanya hivyo vitu vya lab au nurse na pharmacist.......(tatizo CO wengi mnajuaga watu wa lab au lab kule ni kupima tu hizo rapid test na UPT.....ahaa)

Tatu......issue ya kujiongeza sio kwa CO tu kada zetu hizi za afya zipo hivi.....ukikaa muda fulani kwa field hata kama ulikuwa hujawahi soma kitu fulani chuo unakuta unakiperform vizuri tu na mtu asishtuke kwamba wewe huhusiki......nina mifano mingi hapo....ngoja nikupe huu tena kwa hospitali kubwa tunaona......Manurse kibao wanafanya surgery huko mahospitalini.......ndo kajiongeza hapo japo haruhusiwi.

Mtaani huku DLDM ndo linatoa diagnosis....lab test na drugs na mgonjwa anapona japo hawaruhusiwi.

So......CO anasoma hizo basics miezi hyo minne sio akafanye huko lab au akawe pharmacist.

ASANTE.
 
Hujui unachoandika wewe watu wa nyumbani hawana habari hata na hao maCO wanachojua wao ni DLDM tu..........pale wanapoumwa.

Pili.......kozi nzuri kwa nchi yetu kwa sasa ni ile ambayo unaweza kuajiriwa wakati huo unaweza kujiajiri kiwepesi......sasa wewe kasome hiyo CO uje kusugua gaga na wenzako huku mtaani na walivyowengi kama kumbikumbi.

Tatu......hakuna CO anayeweza kumaliza issue ya kumhudumia mgonjwa bila kuwepo watu wa lab, nurse na pharmacist labda kama huyo CO ni mganga wa kienyeji.....ko usijidaganye kwamba CO anaweza kufanya kazi za hao watu.....never.

Note....diploma za lab na nurse physics ni lazima ili usome......maana naona physics ndo imekuwa point yako kubwa na umeing'ang'ania kweli kuidefense hiyo CO.....ahaaaa.

Kama huna mtaji wa kituo cha afya ambacho pia kitahitaji watu wa lab,nurses,pharmacist.....achana na CO........UTANISHUKURU.

ASANTE.
Bado hujakomaa kimaisha kijana! Mpang
iv mkuu umesoma mwaka gani??... anyway acha ubishi mambo yamebadilik C.O usipokua na GPA ya 4+ na kwen kusipokua na ela za kutosh basi maish yako ndo yameishia hapo
Hiyo ni MUHAS kijana, vyuo vya Private kama Kairuki ni 3.5, acheni kudanganya wadogo zenu
 
Bado hujakomaa kimaisha kijana! Mpang

Hiyo ni MUHAS kijana, vyuo vya Private kama Kairuki ni 3.5, acheni kudanganya wadogo zenu

Hata bugando 3.0 unasoma...SHIDAAA NI HADI UTANGULIZE MPUNGA NDIO UPATE NAFASI........yaaaan issue ni competition.
 
Bado hujakomaa kimaisha kijana! Mpang

Hiyo ni MUHAS kijana, vyuo vya Private kama Kairuki ni 3.5, acheni kudanganya wadogo zenu
Iyo kairuk mtt wa mtanzania wa maish ya kawaid anayawez ada ya 7millions kumbuk iyo kairuk ata ukipat div 2 form six unasom muhim ni ela yako
 
Bado hujakomaa kimaisha kijana! Mpang

Hiyo ni MUHAS kijana, vyuo vya Private kama Kairuki ni 3.5, acheni kudanganya wadogo zenu
Labda nikwambie kitu najua karibia kila kitu kuhusiana na hizi kada za afya ndo maana huwa sipendi kuwaona wadogo zangu wanakurupuka eti kisa udaktari hasa hawa familia sawa na mimi........halafu huko kukomaa kimaisha kumekujaje na hunijui.....mbona wewe uliyekomaa umeshindwa kuleta point ya msingi hapo unaleta kukomaa kimaisha pindi hunijui.......narudia tena hunijui mkuu.

Pili.......yawezekana umekomaa kimaisha kama unavyojiona lakini si kwa upande huu pia unaonekana haupo updated na haya mambo wewe........kijana amekueleza vizuri tu hapo juu bado kwa vile haupo updated unabisha tu......unaleta story za muhas.....ngoja nikueleweshe kidogo.

Mkuu hapo juu amekueleza vizuri tu kwamba kwa sasa CO usipokuwa na GPA ya 4+ MD utaisikia kwa wenzako akaongeza na kitu kingine kikubwa sana ukiwa mtoto wa masikini ndo kabisa MD utaisikia.....sasa hapo alikuwa na maana gani hapo.....twende sasa wewe uliyekomaa kimaisha.

less than or equal to 50 students kutoka ordinary diploma in clinical medicine ndo pekee wanaruhusiwa kudahiliwa kwa kila chuo kikuu tanzania kwa ngazi ya MD nchi nzima.

I.e MUHAS-only 20 students from CO
KCMC-only 30 students
BUGANDO-only 30 students.....n.k

Sasa nini namanisha hapo.....MUHAS mtu aliyebahatika kuingia hapo na inabidi akatoe sadaka unakuta ana GPA ya 4.7 yeye huyo ndo wa mwisho wengine 5.0,4.9 na 4.8......hata UDOM the same.......sasa vinabaki hvyo vyuo ambavyo usipokuwa na pesa utabaki nyumbani unatangatanga tu.........ndo pointi aliyekupa kijana hapo juu.....kairuki unayosema wewe mtoto wa mkulima hagusi pale MD.........hata hvyo vyuo vilivyobaki bado capacity yake ni ndogo then tunarudi kwa competition.......na hawa maCO walivyowengi kama kumbikumbi vyuo vya private GPA za 4.4+ zakutosha.........unakuta wewe na GPA yako ya 3.5 hata hiyo kairuki unaikosa na unakosa kweli.

ASANTE
 
Back
Top Bottom