Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewaita kazini vijana 1,453 kati ya 2,100 baada ya kupata kibali cha Rais Samia

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewaita kazini vijana 1,453 kati ya 2,100 baada ya kupata kibali cha Rais Samia

Habari wakuu, nimeona taarifa kadhaa kwenye mtandao hasa kwenye page ya HabariLeo ya kwamba TRA wameshaita vijana kazini. Hii inaukweli wowote? Na kama ni kweli wanawezaje kuita kimya kimya bila kutoa pdf?

======

#HABARINJEMA: Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewaita kazini vijana 1,453 kati ya 2,100 baada ya kupata kibali cha Rais Samia Suluhu Hassan kuajiri vijana 1,000 zaidi ya idadi ya awali.

TRA ilipewa kibali cha kuajiri vijana 1,100 hata hivyo Rais Samia aliongeza idadi ili kuotoa msukumo mpya wa ukusanyaji mapato.

Kaimu Katibu Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Samwel Tanguye ameiambia Daily News Digital kuwa idadi ya watumishi wengine wa TRA wataajiriwa hivi karibuni. TRA sasa inafikisha idadi ya watumishi 5000.

Alisema katika ajira za TRA vijana takribani 66,000 walituma maombi na baada ya kuchujwa kulingana na vigezo vijana 13,800 waliitwa kwenye usaili na 8,586 ndio waliofika kwenye usaili uliofanyika Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar.

Imeandaliwa na Idd Mwema

Rais Samia EWURA wamekalia mkeka Tangu mwaka 2021 hadi leo vijana wako mitaani na interview vijana hawaitwi kisingizio wanamzingiza January makamba kakataa wasiitwe.​

 
Hongereni sana wapambanaji.

Hakika kila mtu ana riziki yake,Sisi ambao hatujabahatika huenda riziki yetu bado, kwahiyo hatuna budi kukomaa.

Inshallaaah!! Kila mpambanaji Mungu atampa riziki yake..

Oya mtaani sio poa wazee..🥱[emoji3064]
 
Ila vijana wana mikwara eti 2.3 M ni ndogo wakati mlikuwa mnajitolea miaka mitano hata hela ya kula hampewi hamjapewa hata check number mshaanza mashauzi mkija kupewa pesa za kujikimu si mtakuja kututukana aisee kweli mwenye njaa .
 
Back
Top Bottom